Tabia Zako: Ufunguo wa Mafanikio au Kushindwa

Dr Arshavin

Member
Joined
May 14, 2024
Posts
26
Reaction score
80
Kitu kinachokufelisha wewe kuyafikia malengo yako na mafanikio yako ni TABIA ZAKO!

The Mind Game Control

Wengi wetu tunapenda kulaumu uchumi, serikali, ndugu zetu, au hata bahati mbaya pale mambo yanapoenda kombo.

Lakini ukweli mchungu ambao huenda hutaki kuusikia ni huu: Wewe ni matokeo ya kile unachofanya kila siku na Sio kile unachopanga kufanya, bali kile unachofanya kiuhalisia.

Twende sana hapa:

Ubongo wako hautaki ufanikiwe.

Ndio, umeisikia sawa. Kiasili, ubongo wako umeundwa kukulinda na kukuweka kwenye eneo lako la faraja na kujidai (comfort zone) na Kuokoa nguvu (energy conservation) ndio kazi yake kuu.

Kusoma kitabu, kuamka saa 11 asubuhi, kwenda gym, au kuanzisha mradi mpya... yote haya ni usumbufu na matumizi ya nguvu ambayo ubongo wako utapambana kuyazuia.

Mtego wa Cheap Dopamine (Raha ya Haraka)

Hapa ndipo tunapofeli zaidi. Kuscroll Instagram, TikTok au kuangalia series kunaupa ubongo wako raha ya haraka sana bila kutumia nguvu yoyote.

Na Ubongo wako unakuwa addicted na hii raha ya bure. Matokeo yake Ukija kwenye kazi ngumu inayohitaji umakini kama kusoma au kujenga biashara unajikuta unaona uvivu na kuchoka haraka kwa sababu haikupi ile raha ya haraka ambayo umeizoea.

Uongo wa Maandalizi (The Illusion of Action)

Kupanga sana sio kufanya. Kuangalia video 10 za YouTube za jinsi ya kutengeneza pesa sio kutengeneza pesa.

Unajipa hisia za uongo kuwa unafanya kitu cha maana, wakati kiuhalisia unajizungusha hapo hapo. Hii ni tabia hatari ya kuahirisha mambo ya Procrastination iliyojificha kwenye koti la kujifunza. Mtu anaangalia reel 100 za kujifunza kitu alafu unamuuliza alipoandika aliyojifunza ni hakuna!

Jinsi ya Kuchukua Usukani wa Akili Yako (The Mind Game Control):

Kama unataka kutoboa, lazima ucheze na akili yako (Mind Game) kwa akili. Hivi ndivyo unavyoweza ku-hack mfumo wako:

1. Sheria ya Sekunde 5 (The 5-Second Rule):

Ukipata wazo la kufanya kitu cha msingi au ratiba yako ikiwa imefika, hesabu kimoyomoyo 5, 4, 3, 2, 1, kisha inuka na uanze kufanya! Ukichelewa zaidi ya hapo, ubongo wako utatengeneza visingizio 100 vya kwanini usifanye.

2. Tengeneza Namna Ili Mazingira Yakulazimishe Kufanya KItu.

Acha kutegemea utashi (willpower). Kama mitandao inakupotezea muda, futa Apps zisizokua na maana, weka simu yako chumba kingine wakati wa kazi. Fanya iwe ngumu kufanya tabia mbaya na iwe rahisi kufanya tabia nzuri.

3. Fanya Dopamine Detox

Jinyime zile raha za haraka kwa makusudi. Punguza muda wa kuangalia TV, kucheza games, au kutumia sana mitandao ya kijamii doomscrolling. Lengo ni kurudisha ubongo wako kwenye hali ya kawaida ili uweze kufurahia mchakato wa kufanya kazi ngumu.

Motivation itakupa mzuka wa kuanza tu, lakini Tabia (Habits) ndizo zitakazokufikisha kwenye mstari wa ushindi. Zichunguze sana tabia zako.

Ukitaka kubadilisha maisha yako, anza kwa kubadilisha unachokifanya kwenye masaa yako 24. Acha kulalamika. Chukua usukani wa akili yako leo. Mchezo upo kwenye akili!
 
Wewe umejuaje haya.!? Au wewe ndio umetuunda.?
 
Upo sawa ila siyo sahihi sana.Usiwapange mnoo hadi wakachizika.
 
The more unavyotumia akili sana kwenye kufanya mambo ndio the more unavyojitoa kwenye uhalisia wako... Success ni default so hardworking au kinyume chake haiwezi kukupa guarantee ya kufanikiwa au kutokufanikiwa.

Just, enjoy na ufanye unachopenda muhimu uweke balance kati ya wewe na wewe mwenyewe.
 
yeah kweli
 
Umeongea vzr kiongozi

Ila Hardworking na ubunifu peke yake ingekuwa inakufanya uwe na mafanikio , kuna watu ni hardworking jamani... "Bahati" pia inahitajika plus imani yako /think in positive way.
 
Back
Top Bottom