Hivi ujamaa bado ni relevant?

Wakuu nchi yetu ni ya kijamaa, hivi hii ideology bado ni relevant(kama imewahi kuwa)?

Je, tuliingia chaka kufuata siasa za ujamaa?
Mifano ya ujamaa Ndiyo hufanya KAZI saizi ni kama EWURA, TRA, Halmashauri, TANROAD, TPDC na mifumo ya kijamii, Tanzania investment centre n.k na ndio ulioshinda Africa
 
Ingependeza kidogo kama ungetueleza wewe unavyoufahamu 'ujamaa'.
Hapo nasi tungepata mwanzo mzuri wa kujadili mada yako hii.

Ulivyoileta mada ni kana kama unatafuta darasa hivi ili ufundishwe maana ya 'ujamaa'; huku tayari ukionyesha kuukandia.

Hata kama unaelewa maana ya 'ujamaa', na kwa uelewa huo ukakufanya usiupende, tueleze basi mfumo badala unaoona wewe ndio dawa sahihi kwa maendeleo yetu.

Huenda nikasomeka kama ninakukandamiza vile. Hapana, hiyo sio nia yangu. Na kama utahisi hivyo, naomba kunradhi.
Kaleta mada kinafiki kwa nia ya kuchonganisha wachangiaji.
 
Back
Top Bottom