Nyerere hakumkataa Lowassa ila alikuwa hawataki Mabepari lakini akaja kushangaa kukuta Mkapa anaukubali Ubepari!

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
84,018
142,058
Wengi wanadhani Nyerere alimkataa Lowasa kama Lowasa, hapana Nyerere hakuwakubali wote wenye fikra za kibepari kuanzia akina Tuntemeke Sanga, Edwin Mtei nk

Nyerere aliukumbatia aina ya Ujamaa alioubuni yeye Mwenyewe na kila aliyeenda Kinyume naye alimuona ni adui

Hata ukiangalia Azimio la Arusha ni Kweli tulitaifisha viwanda lakini viko wapi leo hii? Tunawafuata wale wale tuliowapora tukiwaomba waje wawekeze tena

Nyerere alimleta Mkapa akiamini ataendeleza Siasa ya Ujamaa na Kujitegemea lakini ikawa tofauti na Mkapa akamchukua Lowasa kwenye Baraza la Mawaziri

Tunakumbushana tu
 
Bwashee hao walioshindwa kuendeleza viwanda ni ndugu na jamaa zako wa CCM, kama vile viwanda wangepewa wapinzani, leo kila mmoja wetu angekuwa anafurahia matunda yake.

Hicho alochokifanya Mkapa kwa Nyerere ndicho kilisababisha Nyerere akan'gatuka, alishaona hana mtu wa kuendana na falsafa yake tena huko CCM, matokeo yake hata yule Mkapa aliyeaminiwa kidogo na Nyerere, nae akaja kumthibitishia Nyerere hayupo nae baada ya kuukwaa Urais.

Sent from my SM-G900H using JamiiForums mobile app
 
Hivi Nyerere ndiyo alikuwa na hati miliki ya Tanzania kuliko mtanzania yoyote? tumemchoka muda wake haupo tena, taifa lisonge mbele
 
Back
Top Bottom