Hivi ujamaa bado ni relevant?

Red Giant

JF-Expert Member
Mar 9, 2012
15,658
20,885
Wakuu nchi yetu ni ya kijamaa, hivi hii ideology bado ni relevant(kama imewahi kuwa)?

Je, tuliingia chaka kufuata siasa za ujamaa?
 
Naam!

Nchi hii tokea inasibishwe na Ujamaa na mtu mmoja hadi leo imeshindwa kujiondoa moja kwa moja hadi leo, japo kwa wakati huu naandika haya nchi hii haijulikani imeshika wapi sio Ujamaa, Ubepari wala Uliberali.

Sio Chaka tu bali Takataka bila kujua misingi ya falsafa, uchumi, majongeo na hata dhihaka. Ni kosa kubwa sana linaloitafuna nchi hii kiujumla.

Ujamaa kwa Afrika ni umaskini bila kijujua, wengi udhani ni ukarimu lakini ni hali tegemezi vibaya mno.

Mfano wa aina za Ujamaa ni kama ifuatavyo;-
- Kuombana Chumvi na Viberiti
- Kukusanyika ndani mwako kutazama runinga
- Kupigiana watoto ambao hukuwazaa wala hutoi malezi
- Kupanga mstari kusubiri dawa, sukari au sabuni
- Kutokuwepo utofauti kati ya wanafunzi na wafungwa

Kwa muktadha huu unaweza kupima na kujipatia majibu pia kujiridhisha kutokana na utofauti wa Masaki, Oysterbay // Tandale, Manzese. Chamberbay, Soldierfield // Uswahilini, Nshambya

Alaumiwe!
 
Ujamaa asili ulidhakufa na kuzaliwa kitu kipya ujamaa mamboleo

Sent using Jamii Forums mobile app
Ni kweli umebadilika sana lakini bado unaathiri maisha yetu ya kila siku, Mfano huwezi kuwa na sheria ya uzembe naa uzururaji bila ujamaa. Pia huwezi weka vikwazo vingi kwa raiaa wako kupata passport bila ujamaa. Unafikiri nchi inayofuata ujamaa 'asili' inaweza fanikiwa?
 
Hahahaa, eti kupigiana watoto, Kama mbaya hivyo kwanini tunaufuata? labda unamazuri yake.
Unsfuatwa kwa sababu tayari watu walinyimwa elimu halisi juu yao na hao waliowanyima wanaabudiwa.

Hakuna mazuri sana sana ajabu.... Raia hawana utambulisho rasmi karne ya 21

Propaganda tu
 
Wakuu nchi yetu ni ya kijamaa, hivi hii ideology bado ni relevant(kama imewahi kuwa)?
Je tuliingia chaka kufuata siasa za ujamaa?
Ingependeza kidogo kama ungetueleza wewe unavyoufahamu 'ujamaa'.
Hapo nasi tungepata mwanzo mzuri wa kujadili mada yako hii.

Ulivyoileta mada ni kana kama unatafuta darasa hivi ili ufundishwe maana ya 'ujamaa'; huku tayari ukionyesha kuukandia.

Hata kama unaelewa maana ya 'ujamaa', na kwa uelewa huo ukakufanya usiupende, tueleze basi mfumo badala unaoona wewe ndio dawa sahihi kwa maendeleo yetu.

Huenda nikasomeka kama ninakukandamiza vile. Hapana, hiyo sio nia yangu. Na kama utahisi hivyo, naomba kunradhi.
 
Kalamu1,
Mkuu nchi yetu inafuata siasa za ujama. Hivyo ujamaa ni level za wimbo wa taifa au bendera yetu. Ni kitu kinachojulikana sana nasi. Nafikiri sitakosea nikianzisha majadiliano bila kuanza kuuelezea.
 
Mkuu nchi yetu inafuata siasa za ujama.
Hapana.
Labda tuseme, serikali ya CCM inajitangaza hivyo, lakini kiuhalisi sivyo.

Unajua, China nako wanacho chama chao cha Kikomunisti kinatawala, lakini maisha mitaani siku hizi huwezi kutambua kwamba nchi hiyo bado inasimamia mfumo wa kikomunisti.

Labda pia nikupeleke upande wa pili. Wakuu kabisa wa mfumo wa 'ubepari' Marekani, hata huko utakuta kwamba kuna mambo yanayofanywa tofauti na matakwa ya mfumo huo.

Hivi nchi za 'Scandinavian' Sweden na wenzao, wao mfumo wao hasa uliowaletea mafanikio ni mfumo upi, Ujamaa au Ubepari?

Maana yangu hapa ni kwamba, dunia sasa imekwishaondoka huko kwenye huo mgawanyiko uliokuwa unapiganiwa na pande hizo mbili,
Hard nosed Capitalism and Socialism regimes have never worked in society anywhere in the world! (kalamu1)... maana sijaliliokota kokote. Ni wazo langu halisi.
 
Nchi za scandinavia zinafuata social decmoccracy. Huu wengi wanabisha siyo kama ujamaa wa Cuba au N.Korea. Huu unafanana zaidi na ubepari maana sehemu kubwa ya uchumi ipo kwa watu binafsi. China kila siku wanafanya reforms, bado hawajatoka moja kwa moja kwenye ujamaa bado wanamakampuni makubwa ya serikali yanayojiendesha kizembe na kwa kulindwa na pia bado suala la property rights hawajaliweka sawa. Wataalamu wanasema ili iendelee kuendelea inahitaji mabadiliko mengi zaidi kutoka ujamma, hivyohivyo kwa Vietnam. Kwasasa ujamaa na ubepari ni spectrums , viko tofautitofauti sehemu na sehemu ila kujinadi tu kuwa mimi mjamaa au mbepari kuna athari kubwa.
 
Lililo la mhimu katika yote hayo kwa baadhi yetu mkuu 'Red Giant' ni hili: maslahi ya wananchi wa kawaida.

Je, wananchi wanafaidika na kupata haki katika juhudi zao na mali zao?

Kama ni 'ujamaa' au 'ubepari' unaweza kufanya hivyo basi na usifiwe.

Lakini historia inaonyesha wazi kwamba hakuna mfumo pekee unaoweza kufanya hivyo kwa ukamilifu wake.
 
Hakuna nchi ni wabepari 100% au wajamaa 100%
asilimia 50% ya nchi za ulaya ni social democracy (The same na Tanzania)

Mfano Israel ni socialist country

Mleta mada unatakiwa ujue kuna aina 3 za Capitalism

1. Free economy
2. Socail Capitalism (Huduma za afya kusimimamiwa na Serikali, mfano ni Tanzania na Sera za Democrats wa Marekani)
3. Government Capitalism (Serikali kufanya biashara mfano Serikali ya China)

So ukielewa hizi tofauti utaona relevancy ya socialism na kwa nini Marekani haijawahi kuiletea fyoko fyoki nchi ya Saudi Arabia
 
Wakuu nchi yetu ni ya kijamaa, hivi hii ideology bado ni relevant(kama imewahi kuwa)?

Je, tuliingia chaka kufuata siasa za ujamaa?
Rais wangu WA majukwaani saizi ni muda wa kitembea na Pacha lako ili kupunguza stress za watu Tutahakikisha tunamjazia strategies za kuboresha maisha ya watanzania...

Saizi Maprinter tayari ndege ikitua Tu na dhana ya ujamaa itatumika ni Raha tupu kuanzia na serikali ya VIWANDA kufufua vyote Kwa fedha zetu wenyewe wenye viwanda vya stress watatujoin wenyewe..

Saizi ni kuchota hela (BOT/HAZINA) kila MTU alipwe laki 500000 Kwa mwezi fungua viwanda vyote vilivyokufa walipe Kodi na gawio KAZI imeisha pokea mishahara usifanye KAZI umetaka mwenyewe..

Ujamaa kwisha habari yake. Kilichobaki ni fantasy tu.

Sent using Jamii Forums mobile app
Ukiangalia utagundua ujamaa ulikuwepo toka mwanzo kuumbwa kwa dunia,tunatakiwa tuishi kwa kufanya kazi bila kumiliki,tukusanyre na kutumia kwa pamoja bila kuhodhi,yaani tuishi kama wanyama wa porini kina simba,na nyani,kama ndege na samaki.Ila kwa asili binadamu ni mchoyo,wengi wanafurahia na kuona sofa wanapokuwanacho ili hali wengine hawanacho,hebu fikiria wakati majirani hawana hata kikombe cha uji mmoja ana magunia elfu ghalani,wakati wengi hawana thumuni mwingine mwenye umri w miaka sabini anaiba matrilioni ya fedha za umma.mule China na urusi ya Leo ndio kina matajiri mabepari wakutupwa. Binadamu alianza maisha stahili wakusanyaji wakaenda stahili ya kumliki MTU mwingine kama Mali ,akaena stahili kumiki ardhi,akaenda stahili ya kumiliki rasilimali na kutoa ajira kwa watu wengine,ilitegemewa mifumo hii ya kinyojnyaji ingejifia na kuibuka mfumo was ujamaa ,bahati mbaya ujamaa na ukomunisti imekufa kifo cha mende.UJAMAA Kwisha..
 
Rais wa China Deng Xioping aliwahi sema ''Tuache wachache wawe matajiri kwanza". Leo China na Urusi zenye matajiri wa kutupwa zina maisha bora kuliko zilizokuwa zinafosi kuwa watu wote ni sawa. Cuba iliyong;ang;ania ujamaa leo watu wanalipwa cigars badala ya mishahara.
 
Hakuna nchi ni wabepari 100% au wajamaa 100%
asilimia 50% ya nchi za ulaya ni social democracy (The same na Tanzania)

Mfano Israel ni socialist country

Mleta mada unatakiwa ujue kuna aina 3 za Capitalism

1. Free economy
2. Socail Capitalism (Huduma za afya kusimimamiwa na Serikali, mfano ni Tanzania na Sera za Democrats wa Marekani)
3. Government Capitalism (Serikali kufanya biashara mfano Serikali ya China)

So ukielewa hizi tofauti utaona relevancy ya socialism na kwa nini Marekani haijawahi kuiletea fyoko fyoki nchi ya Saudi Arabia
Mkuu usichanganye welfare states na ujamaa.
 
Watu wengi hawajui ujamaa katika aina au mifumo yake mbalimbali ulitoka wapi na kwa ajili ya nini.

Ukweli ni kwamba watu wengi hawajui walioanzisha ujamaa walikuwa na malengo gani.

Ujamaa katika mifumo yake mbalimbali haiwezi kuwafanya watu waendelee.

Bahati mbaya sana walioanzisha mfumo huu wamefanikiwa kufanya ujamaa kwa watu wengi ni imani, itikadi, mawazo na falsafa.

Ninaweza kusema kwa hakika kwamba mifumo mingi ya maisha ni UTAFITI DHIDI YA UWEPO WA MUNGU. Hii yote inatafiti ukweli wa kile lifundishavyo Kanisa.

Ujamaa ni mfumo ovu kabisa. Aina au mfumo wowote wa ujamaa ni ovu kwa maisha ya watu kiakili na kimwili.

Watu, hasa sisi Wafrika tumekuwa sample za kitafiti dhidi ya Kanisa lifundishavyo juu ya Mungu. Mifumo ya kijamaa na mingine ya aina hiyo ipo katika kupinga dini yenyewe. Hii inajaribu kuelewa kwa namna yake na Kanisa lifundishavyo.

Watu wengi kwa sababu ya kukosa elimu sahihi tunaingia na kutumikia mifumo hii na hivyo tunateketea kiakili -maadili, kimwili - kiuchumi.

Waanzilishi wa mifumo hii wana malengo yao. Hayo yaweza kuwa: kwanza Utafiti juu ya Mungu na lifundishavyo Kanisa. Pili, sababu za kiuchumi na kiutawala.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom