Hili suala ni gumu saaana.
Hatujitoshelezi wenyewe kwenye maisha haya, lazima tuhitaji watu wengine kushirikiana nao.
Itatokea tu uliowaamini watakuumiza katikati ya mashirikiano hayo. WALA USIUMIE maana ni mapito tuu, hata usikome maana kama hujapata wewe, basi kapata yeye.
Rafiki yangu saana, classmate toka primary mpaka chuo tulikuwa roommates, niliamini tunapendana sana nilimtegemea kuwa nina mtu wa kunisaidia ninapokuwa na shida. Baada ya chuo akawa anafanyia kazi sehem ambayo kila akiwa anaenda home lazima apitie mji niliopo, tena analala kwangu ndo kesho yake anaenda. Siku amepata msiba nyumbani, katikati ya mwezi, akaniomba nimkopeshe laki mbili tu mwisho wa mwezi atairejesha, kusema ule ukweli wa moyoni sikuwa na ile pesa Ila tuliitafuta wote, nilivaa lile tatizo kama langu, nikaipata nikampa ile hela. akaenda msiba wakati anarudi akapitia kwangu ndo akarudi kazini kwake..., sikuwahi kumwona tena imepita miaka 6 sasa. Nilipiga simu, nimeandika sms zote, mpaka nimetumia watu wengine hakuwahi kurespond, nikailipa ile hela.
Miezi kama miaka miwili tangu anikope, akaja kunitafuta, nilifurahi saana, maana niliona huenda urafiki wetu utarudi tena, sikuitaka ile hela tena mana niliona kama ilitutenganisha. Kumbe siku hiyo jamaa ana shida ya elfu 30, Kwa txt aliyonitumia niliona ana shida mno, nikampa tena. hiyo aliirudisha japo kwa mbinde lakin baada ya hapo akaingia mitini tena.
Nimemsamehe kabisa, lakin nafikiri hata yeye hajisikii vzr huko aliko, nataman itokee namna tulisahau hilo deni ili maisha yarudi kama mwanzo lakin imeshindikana.
Wapili rafiki wa ukubwani, huwa namkopa saana, tena naamini Mimi ndo niliyemkopa saaana kipindi flan cha maisha, siku amekuja na shida kubwa, na alikuwa anajua kuna project naifanya, akaniomba nimkopeshe kiasi flan, kwamba mpaka ifike stage flan ya project pesa itakuwa imesharudi ili niendelee na mambo yangu. Pesa aliyochukua alikuwa anatengenezea gari yake iliyokuwa inafanya biashara. Nilimpa, gari ikapona ikaendelea na biashara, lakini pesa haikuwahi kurudi.
Namwona kabisa pesa ya kunilipa anayo lakini hanilipi, nakasirika mpaka mwisho wa hasira lakin sina cha kumfanya maana hatukuwa na maandishi. Nimeona niache tuu.
Scenarios zipo nyingi, kwenye zote huwa napata amani moyoni ninapoikumbuka dhamiri yangu kipindi naitoa pesa.
Tabia za mtu Mimi zisinihusu, japo inaumiza lakin ukijifundisha kuachana nayo unaweza kusahau na kuendelea na maisha.
CHA KUSHANGAZA, HUACHI KUWA NA MARAFIKI WENGINE NA MNAENDELEA KUKOPESHANA.