MAHANJU
JF-Expert Member
- Aug 26, 2014
- 5,244
- 7,966
Mungu huyu ni mwenye huruma kuliko kiumbe chochote duniani, hili suala la kuwarudisha wasichana waliopata mimba mashuleni kwa mwenyewe hofu ya Mungu ataelewa nini namaanisha, wengine hawakufanya hivyo kwa akili za kawaida ispokua na kushawishiwa na kushindwa kukwepa mitego ya vishawishi hovyo maana wanaume wana mbinu lukuki za kumnasa mwanamke aliyekomaa na akili zake timamu sembuse huyu mtoto wa shule! Kuna wapo wanakutana na majanga haya kwa kubakwa au kufanya ngono kwa vitisho na sio kupenda.Serikali ilitakiwa kuwaonea huruma tu japo haileti picha nzuri na sio kuwasimanga na kuwanyanyapaa.
Pamoja na haya yote, kiongozi akisimama na kumpigia magoti Mungu amsamehe makosa yake atambue kua kuwanyanyapaa wasichana hawa ni dhambi kubwa sana na anamkasirisha Mungu sana. Mungu hupenda watu wenye huruma na wenye kujali utu wa wanadamu wenzao.
Tunashindwa vipi kupambana na watoaji mimba na vyanzo vingine hatarishi vinavyosababisha mpaka tumgeukie mtoto wa kike? Hivi ni mtoto wa kike ndiye anayemtongoza mwanaume ili alale naye? Mtoto Mdogo kama huyo anapata wapi ujasiri wa kumfuata fataki mzee mzima kumwomba afanye naye ngono kama sio kushawishiwa?
Yaani hata kama alikua na akili sana sana ikatokea bahati mbaya akatiwa mimba na hivyo ndoto zake zinaishia hapo? Hatujui ni nguvu kazi na hazina kiasi gani tunapoteza kama taifa mpaka wenzetu wanatushangaa.
Sio lazima wote warudi mashuleni, ispokua hata unaweza kuangaliwa utaratibu mwingine wa kuwasaidia na sio veta au kwenda kulima bustani. Kiangaliwe na chanzo na mazingira ambayo mtu alipata mimba mimba na sio kuwanyanyapaa kiasi hiki.