Hivi tunapozuia Wasichana waliojifungua kurudi shule, tunataka tuombewe kwa Mungu yupi?

MAHANJU

JF-Expert Member
Aug 26, 2014
5,161
2,000
Mungu huyu ni mwenye huruma kuliko kiumbe chochote duniani, hili suala la kuwarudisha wasichana waliopata mimba mashuleni kwa mwenyewe hofu ya Mungu ataelewa nini namaanisha, wengine hawakufanya hivyo kwa akili za kawaida ispokua na kushawishiwa na kushindwa kukwepa mitego ya vishawishi hovyo maana wanaume wana mbinu lukuki za kumnasa mwanamke aliyekomaa na akili zake timamu sembuse huyu mtoto wa shule! Kuna wapo wanakutana na majanga haya kwa kubakwa au kufanya ngono kwa vitisho na sio kupenda.Serikali ilitakiwa kuwaonea huruma tu japo haileti picha nzuri na sio kuwasimanga na kuwanyanyapaa.

Pamoja na haya yote, kiongozi akisimama na kumpigia magoti Mungu amsamehe makosa yake atambue kua kuwanyanyapaa wasichana hawa ni dhambi kubwa sana na anamkasirisha Mungu sana. Mungu hupenda watu wenye huruma na wenye kujali utu wa wanadamu wenzao.

Tunashindwa vipi kupambana na watoaji mimba na vyanzo vingine hatarishi vinavyosababisha mpaka tumgeukie mtoto wa kike? Hivi ni mtoto wa kike ndiye anayemtongoza mwanaume ili alale naye? Mtoto Mdogo kama huyo anapata wapi ujasiri wa kumfuata fataki mzee mzima kumwomba afanye naye ngono kama sio kushawishiwa?

Yaani hata kama alikua na akili sana sana ikatokea bahati mbaya akatiwa mimba na hivyo ndoto zake zinaishia hapo? Hatujui ni nguvu kazi na hazina kiasi gani tunapoteza kama taifa mpaka wenzetu wanatushangaa.

Sio lazima wote warudi mashuleni, ispokua hata unaweza kuangaliwa utaratibu mwingine wa kuwasaidia na sio veta au kwenda kulima bustani. Kiangaliwe na chanzo na mazingira ambayo mtu alipata mimba mimba na sio kuwanyanyapaa kiasi hiki.
 
No Escape

JF-Expert Member
Mar 7, 2016
6,680
2,000
Kwani Mungu yupi aliwaruhusu kupata Mimba Bila kuolewa? Mungu Amekataza hata uzinzi ndio atakubali mimba zisizo na baba! Tuache kumshirikisha Mungu katika ufuska wetu.
 
Dr Akili

JF-Expert Member
Aug 21, 2011
3,899
2,000
Tangu mwamzo hawajawahi kuwa wanarudi shule baada ya kutimuliwa kwa kosa la kufanya mapenzi, achilia kupata mimba. Na hii inahusu wanafunzi wa jinsi zote mbili - wasichana na wavulana. Miaka ya hivi karibuni tukatunga sheria ya kuwafunga jela wale jinsia ya kiume iliyofanya mapenzi na jinsia jiyo ya kike. Jinsia ya kike ikahurumiwa kufungwa jela. Baada ya muda mfupi jinsia hiyo ya kike ikadiriki kuleta ombi kwa serikali kwamba iruhusiwe kurudi shule baada ya kuzaa. Yaani mwanafunzi wa kike akipata mimba aendele na shule hadi mwisho wa uja uzito, apumzike mwezi mmoja au wiki mbili baada ya kujifungua halafu arudi kuendelea na syllabus: asipitwe masomo maana future yake itaharibika wakati kale kavulana kyanafunzi chenzake kilichofanya naye mapenzi kinasota jela miaka 30. Sasa jibu la ombi hilo la visichana hivyo serikali ya awamu ya tano imelikataa. Labda wasubiri serikali za awamu zijazo labda zitalikubali. Katika awamu hii hakuna mzazi atakayesoma shule za msingi na secondari kwa utaratibu wa serikali kupitia NECTA as Secondary school candidates ila wanaweza kusoma kama private candidates kama ilivyo sasa. Yaani namba zao za mhihani hazitaanza na herufi S bali herufi P kama utaratibu ulivyo kwa sasa kwa watu wazima wanavyosoma. Ukisha kuwa mama wa watoto lazima ukubali kuwa umeshkuwa mtu mzima. Tatizo liko wapi?
 
Eja One

JF-Expert Member
Sep 29, 2011
1,141
1,500
Mungu huyu ni mwenye huruma kuliko kiumbe chochote duniani, hili suala la kuwarudisha wasichana waliopata mimba mashuleni kwa mwenyewe hofu ya Mungu ataelewa nini namaanisha, wengine hawakufanya hivyo kwa akili za kawaida ispokua na kushawishiwa na kushindwa kukwepa mitego ya vishawishi hovyo maana wanaume wana mbinu lukuki za kumnasa mwanamke aliyekomaa na akili zake timamu sembuse huyu mtoto wa shule! Kuna wapo wanakutana na majanga haya kwa kubakwa au kufanya ngono kwa vitisho na sio kupenda.Serikali ilitakiwa kuwaonea huruma tu japo haileti picha nzuri na sio kuwasimanga na kuwanyanyapaa.

Pamoja na haya yote, kiongozi akisimama na kumpigia magoti Mungu amsamehe makosa yake atambue kua kuwanyanyapaa wasichana hawa ni dhambi kubwa sana na anamkasirisha Mungu sana. Mungu hupenda watu wenye huruma na wenye kujali utu wa wanadamu wenzao.

Tunashindwa vipi kupambana na watoaji mimba na vyanzo vingine hatarishi vinavyosababisha mpaka tumgeukie mtoto wa kike? Hivi ni mtoto wa kike ndiye anayemtongoza mwanaume ili alale naye? Mtoto Mdogo kama huyo anapata wapi ujasiri wa kumfuata fataki mzee mzima kumwomba afanye naye ngono kama sio kushawishiwa?

Yaani hata kama alikua na akili sana sana ikatokea bahati mbaya akatiwa mimba na hivyo ndoto zake zinaishia hapo? Hatujui ni nguvu kazi na hazina kiasi gani tunapoteza kama taifa mpaka wenzetu wanatushangaa.

Sio lazima wote warudi mashuleni, ispokua hata unaweza kuangaliwa utaratibu mwingine wa kuwasaidia na sio veta au kwenda kulima bustani. Kiangaliwe na chanzo na mazingira ambayo mtu alipata mimba mimba na sio kuwanyanyapaa kiasi hiki.

Focus yetu ni kwenye kinga na sio tiba...kama una huruma sana wewe toa hata robo tu ya mshahara wako uwe unawasomesha private schools..ukiweza hilo uje hapa utushawishi kuibana serikali ibadirishe msimamo.
 
Sokoro waito

JF-Expert Member
Nov 21, 2014
2,205
2,000
Kwa logic yako hata mashoga na wabakaji plus wauaji na vibaka wa rangi zote hawatashughulikiwa na sheria bali utataka wahurumiwe, mwisho wa siku utataka na mahakama zifutwe ili uishi kwenye free world under the control of DEVIL. kuwa makini.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom