Hivi tuna Jaji Mkuu na Mahakama nchi hii! Mbona Rais anavunja sheria hivi?

Hii nchi inavurugwa kwa makusudi kwa kisingizio cha kuleta maendeleo haraka!

Kwa hatua tuliyifikia hali imekuwa mbaya kabisa! Nchi inaendwshwa kwa matamko ya rais tu ambaye pia anaupeo mdogo sana wa kiuongozi!

Huyu tumemuendekeza wenyewe, anajiona mungu nyoka! Mambo anayofanya ilitakiwa aambiwe No! Na kila mmoja...!!!
 
"MENGELENI KWETU, post: 33002752, member: 178454"]
Kila nikikumbuka zile danadana za uteuzi wake na haya yanayotokea hivi sasa, naconclude kabisa kwamba he was first compromised before being confirmed..
Hili watu walilisema mwanzoni kabisa kwamba utendaji wake utapimwa na jinsi uteuzi wake ulivyokuwa.
Mkuu Pascal Mayalla alisimama kutetea sana akisema ana msimamo

CJ kila shuguli ya Ikulu hata ambazo hazimuhusu yupo pale na anapewa nafasi ya kuongea..CJ sio mtu wa kuwa hadharani-hadharani kila siku..ndio nature ya kazi yake.Naam, hata akitokea hadharani wananchi mnasema hapa kuna jambo na kweli linakuwepo..
Kumbuka enzi zile za Retired CJ Samatta,humuoni akitokea hadharani ni kwa jambo mahsusi linalomuhusu kiukweli..
Hapa niwaite walioyaona zama hizo akina JokaKuu Mag3 Pascal Mayalla . Nakumbuka ilikuwa kumuona CJ ni kitu nadra sana. Akitokea Nyalali ni katika shughuli kubwa za kitaifa. Ilikuwa kama ''mwiko'' kumuona CJ akichangamana katika shughuli, nyingine zikiwa za kisiasa.

Tatizo la CJ kujihusisha sana na shughuli hizi ni kutengeneza ''conflict of interest''
Kuna mambo ya kisheria yanayoweza kuelekea mahakamani, sasa kama yupo na anasikiliza kwa lugha nyingine anakuwa kama vile anapokea ''maagizo''

Mahakama ukiwa ''mhimili huru'' ni muhimu ukajitenga na shughuli nje ya zile za kisheria.

Niliwahi kusikia CJ akisema ''uchunguzi wa tukio fulani'' ni lazima ufanywe na vyombo vya ndani'' . Hii ni baada ya wanasiasa kusema ''uchunguzi utafanywa na vyombo vya ndani.


Nilijiuliza sana hivi kwanini CJ azungumzie suala hilo nje ya mahakama?
Tena anatoa msimamo kabisa kuwa uchunguzi lazima ufanywe na vyombo vya ndani.

Hivi mahakama haiwezi kukubali uchunguzi na ushahidi unaotoka ndani ya nchi hata kama umefanywa na mtu wa nje? Ilitatiza sana na sijui kama kauli ile ilikuwa sahihi kwa wakati, tukio na mazingira.

Suala hilo likiongelewa ndani ya mahakama hakuna tatizo, nje ya mahakama kuna tatizo

Kama ningalikuwa ''msaidizi'' wake ningemshauri aangalie shughuli za kuhudhuria au kuzungumza ili kuiacha mahakama na taswira isiyo na shaka, at least!
 
Hili watu walilisema mwanzoni kabisa kwamba utendaji wake utapimwa na jinsi uteuzi wake ulivyokuwa.
Mkuu Pascal Mayalla alisimama kutetea sana akisema ana msimamo

Hapa niwaite walioyaona zama hizo akina JokaKuu Mag3 Pascal Mayalla .
Mkuu Nguruvi3, asante kwa kuniita huku, mchango wangu kwenye hoja hii ni huu.
Tanzania tunaye Jaji Mkuu wa Tanzania jina lake anaitwa Prof. Ibrahim Hamisi Juma.
P
 
Suluhisho la kudumu na litakaloirejesha nchi kwenye mstari mnyoofu na wa heshima ni PEOPLES REVOLUTION. MAPINDUZI YA UMA.
Haya mapinduzi yanapaswa yaanzishwe na raia kwa dhati kabisa bila kujali gharama zake.
Kwa mfumo huu, hakuna mabadiliko yatakayoshuka kutoka kwa wanasiasa wanaopigania matumbo yao.
Ila naamini, IPO SIKU watu wataamua na watawala watasikiliza.
Nafikiri hili ni gumu kufanyika..
La kufanya nafikiri ni kumwomba Mungu wanaolifikisha taifa hapa.. Wapotee ktk uso wA dunia.
 
Unajua watu walizoea miteremko kila mahali, Rais Magufuli kaleta heshima za mifumo ukosoaji ndio unaanza? Naomba muelewe mfumo umeshabadilika, kamwe hatuwezi kurudia Madudu ya zamani
 
Kiukweli mihimili ya bunge na mahakama hapa kwetu ni dhaifu sana, ndo maana rais anafanya chochote awezacho na atakacho.kweli rais anapanga hata muda Wa kutoa watuhumiwa toka mahabusu, kwanini Rais asingesubiri wahukumiwe na mahakama kisha awatoe kwa msamaha wake kama katiba inavyotaka?

Nawashauri wabunge Wa upinzani waanzishe mchakato Wa kumshitaki rais kupitia bunge hata kama huko mbeleni watashindwa kupitia mchakato huo bungeni.

Wafanye hivo kwa sababu ya rais kavunja katiba yetu Na kushindwa kusimamia kiapo chake.wakifanya hivo watakumbukwa Na taifa letu huko mbeleni.
 
Jaji Mkuu alishatoa tamko hivi karibuni. Alisema ni vizuri kama Polisi wakifanya uchunguzi na ukishakamilika ndo wamkamate mshitakiwa badal sasa ambapo mtu anakamatwa halafu ndo uchunguzi ufanyike na wakati mwingine unachukua miaka kadhaa.
Yeye hatakiwi kuwa mwanasiasa anatakiwa kutenda, kama serikali inatenda mambo ya kuminya haki za watu kwa nn majaji wasitupilie mbali makes hayo? Yeye anaungana Na serikali kila Siku ikulu kushuhudia shughuli za ikulu.
 
Jaji Mkuu alishatoa tamko hivi karibuni. Alisema ni vizuri kama Polisi wakifanya uchunguzi na ukishakamilika ndo wamkamate mshitakiwa badal sasa ambapo mtu anakamatwa halafu ndo uchunguzi ufanyike na wakati mwingine unachukua miaka kadhaa.
Yeye hatakiwi kuwa mwanasiasa anatakiwa kutenda, kama serikali inatenda mambo ya kuminya haki za watu kwa nn majaji wasitupilie mbali makes hayo? Yeye anaungana Na serikali kila Siku ikulu kushuhudia shughuli za ikulu.
 
Tatizo ni moja tu. Huwezi kuwa huru wakati unachaguliwa na muhimili mmoja. mihimili miwili inachaguliwa na mmoja. Mahakama inachaguliwa na mkuu, Bunge na mzee. Speaker kwa maana mzee ndio rais wa chama tawala utakuwa chini yake tu. Vitu vitatu muhimu. Kiongozi wa mahakama asiteuliwe na mkuu. Huku bungeni Rais asiwe mwenyekiti wa chama huwezi kuwa mchezaji wakati huohuo wewe unafilimbi ya refa. tuchukuwe system za wenzetu Rais sio mwenyekiti wa chama haya utakuta Afr
Jaji Mkuu alishatoa tamko hivi karibuni. Alisema ni vizuri kama Polisi wakifanya uchunguzi na ukishakamilika ndo wamkamate mshitakiwa badal sasa ambapo mtu anakamatwa halafu ndo uchunguzi ufanyike na wakati mwingine unachukua miaka kadhaa.
"Ni vizuri kama polisi wakifanya" hilo lalamiko au ombi au ushauri. Toa muongozo na amri kwa mjibu wa sheria. Huo ndio udhaifu mkubwa na ndio maana watu kama hawajamsikia vile.
 
Kiukweli mihimili ya bunge na mahakama hapa kwetu ni dhaifu sana, ndo maana rais anafanya chochote awezacho na atakacho.kweli rais anapanga hata muda Wa kutoa watuhumiwa toka mahabusu, kwa nn rais asingesubiri wahukumiwe na mahakama kisha awatoe kwa msamaha wake kama katiba inavyotaka? Nawashauri wabunge Wa upinzani waanzishe mchakato Wa kumshitaki rais kupitia bunge hata kama huko mbeleni watashindwa kupitia mchakato huo bungeni.wafanye hivo kwa sababu ya rais kavunja katiba yetu Na kushindwa kusimamia kiapo chake.wakifanya hivo watakumbukwa Na taifa letu huko mbeleni.
Katiba..
 
Wewe mleta mada umezungumzia upande wako lkn kwa upande wetu sisi wanyenge au walala hoi tulio wengi ambao kwa kipindi kirefu tulikuwa hatuna haki, lakini ktk awamu hii ya 5 tunaona vyombo vyetu kama Mahakama n.k vinatenda haki kwa uwazi na kwa wakati, sioni kuingiliwa kokote hapo,.

Ukitoa mifano ya watu wawili au watatu ikawa ndo msimamo wako unakosea sana.

Nchi yetu inaenda vizuri sana ktk utawala wa sheria kuliko kipindi chochote kile.
 
Hatuna Chief Justice tuna Kikaragosi kimoja cha Jiwe kimewekwa pale kutii na kuenenda kwa matakwa ya Jiwe!
Fully obedient kwa Jiwe, Fully kujikunyata na kukosa kauli wakati haki za wananchi na misingi ya sheria za nchi hii Zikisiginwa
Somebody out there akamwambie huyu Chief Justice, Hivi anaelewa kweli maana ya kuwa Chief Justice au anadhani yupo pale kutenda hisani ya Jiwe?
 
Back
Top Bottom