Hivi tuna Jaji Mkuu na Mahakama nchi hii! Mbona Rais anavunja sheria hivi?

Missile of the Nation

JF-Expert Member
May 24, 2018
13,439
50,961
Wana JF!

Nchi yetu ipo katika wakati mgumu sana tangu tupate uhuru.
Ni dhahiri utawala huu wa Magufuli umeamua kuingilia mhimili wa mahakama na mahakama yetu chini ya uongozi wa Jaji mkuu wa sasa inaonekana kuwa legelege mno kusimamia independence yake kitu ambacho kinaelekea kutufanya sisi wananchi tukose imani japo kiduchu iliyokuwa imebaki kwa chombo hiki.

Nchi hii ina Jaji mkuu ambaye dhamana kuu ya nafasi yake ni kuhakikisha chombo cha mahakama hakiingiliwi, hakinyang'anywi hadhi yake na kikubwa kabisa taratibu za kimahakama zinaheshimiwa.

Katika kipindi hiki cha utawala huu tumeona mahakama ikiingiliwa waziwazi kabisa lakini hatuoni Jaji Mkuu akisimama kidete kutetea hadhi na wajibu wa chombo hiki. kwa mfano

1.Tunaona mhimili wa serikali ukipeleka watu mahakamani, kuwafungulia kesi nzito za uhujumu uchumi, kisha wakati mwingine kuachana nazo bila maelezo yaliyonyooka huku watu wakiwa wameshasota rumande Je Jaji mkuu yuko wapi kuintervene katika mazingira kama haya?, Uko wapi muongozo wa mahakama katika kesi ambazo zinaletwa mahakamani bila ushahidi wa kutosha?

2.Tunaona leo Rais eti anashauri "Watuhumiwa wa makosa fulani waachiwe kwa kufanya kadha wa kadha", Halafu eti ushauri huo unaandaliwa siku maalum ya kuona umetekelezwa vipi, kisha mshauri anatoa siku nyingine saba ushauri wake huo utekelezwe!!, Hivi umewahi kuona wapi mshauri anatoa time limit ya ushauri wake kutekelezwa?

3. hivi karibuni pamekuwepo na kesi kadha wa kadha ambazo huhitaji kuwa genius kuona kuwa mhimili wa Serikali unaiendesha mahakama kwa remote control, Kesi ya Lissu na ishu ya Fatuma Karume. Kesi ya Lissu hakimu anadai hawezi kuingilia mhimili wa bunge, Ina maana Bunge lisipotenda haki mahakama haiwezi kulinda haki kwa ambaye hakutendewa haki?, Hii mahakama ya wapi inayojivua wajibu wake?, Si ni katiba ya nchi inayosema kuwa mahakama ndicho chombo kikuu cha utoaji haki nchini, sasa hii ya kutwambia wananchi kuwa mahakama ina hofu ya kuingilia bunge maana yake nini?.
Ishu ya Karume, sote tunajua kuwa hakupewa haki ya kusikilizwa, na kama tamko la TLS lilivyosema kwa precedence ya matukio ya nyuma mtuhumiwa wa makosa kama aliyoadhibiwa nayo Fatma hupaswa kusikilizwa ili haki itendeke maana hiyo kazi ndiyo kazi inayompatia rizki na pia kufanya kazi halali ni haki ya mtu kikatiba

4.Lakini pia wakati hayo yakiendelea kuna Masheikh wa uamsho wako Jela sasa tunakwenda mwaka wa tano, bado kesi yao inapigwa danadana, Je ni kweli mahakama imeshindwa kusimama hapa na kuiambia Serikali ilete kesi ya msingi dhidi ya wananchi hawa au la Iachane na kesi?, If there is no evindence it means it doesn't fit and if it doesnn't fit equit!!

Nchi hii ina Jaji mkuu, Je cheo chake ni ceremonial tu au ni Jaji mkuu kweli kweli wa kuhakikisha haki za wananchi katika kona za mahakama zinalindwa?

Kama Jaji mkuu ameshindwa kulinda haki za watu, na kama anaendelea kuona mienendo ya haki inaingiliwa na mhimili wa serikali huku akiangalia tu basi namshauri kuwa kabla wananchi hatujapoteza hako kachembe kadoogo sana ka imani juu ya mahakama basi pengine si vibaya akajiuzulu tu

HAKI HUINUA TAIFA BALI UDHALIMU NI AIBU YA WOTE!

Mheshimiwa JAJI Mkuu, Wananchi tunataka haki katika mahakama zako!
 
Hakuna bunge(spika) Wala mahakama(jaji mkuu)

Hakuna kabisaaaa....Kuna Jiwe tu

Hao wote wameshindwa kusimama kutetea hadhi na mamlaka ya vyombo vyao, yaani wamejikunyata kama makinda ya ndege na kujiweka kwenye fumbato la Jiwe kupata joto lake!
Hivi hao Watu wanafikiri kuwa kama wao ni matunda ya hisani ya Jiwe basi hata vyombo vyao wanavyoviongoza navyo vipo kwa hisani ya Jiwe?

Hivi hawajui haki ngapi za wananchi zinasiginwa kwa wao kujivutavuta kusimama kidete?
 
Mkuu unakumbuka kuwa Bw Yule alishasema yeye ndiye anaewateua na yeye ndiye anaewalipa mishahara na kuwapatia Magari? Je umesahau vitisho dhidi yao? Kwa ujumla Nchi yetu imeoza na hatuna wakutusafishia bali ni sisi wenyewe.
Tufanye nn basi? Kila mmoja wetu atafute jibu.
 
Hao wote wameshindwa kusimama kutetea hadhi na mamlaka ya vyombo vyao, yaani wamejikunyata kama makinda ya ndege na kujiweka kwenye fumbato la Jiwe kupata joto lake!
Hivi hao Watu wanafikiri kuwa kama wao ni matunda ya hisani ya Jiwe basi hata vyombo vyao wanavyoviongoza vipo kwa hisani. ya Jiwe?

Hivi hawajui haki ngapi za wananchi zinasiginwa kwa wao kujivutavuta kusimama kidete?
Wanajua Sana....Sasa unataka wakiugua wasipelekwe Apolo??
 
Hao wote wameshindwa kusimama kutetea hadhi na mamlaka ya vyombo vyao, yaani wamejikunyata kama makinda ya ndege na kujiweka kwenye fumbato la Jiwe kupata joto lake!
Hivi hao Watu wanafikiri kuwa kama wao ni matunda ya hisani ya Jiwe basi hata vyombo vyao wanavyoviongoza vipo kwa hisani. ya Jiwe?

Hivi hawajui haki ngapi za wananchi zinasiginwa kwa wao kujivutavuta kusimama kidete?
Mkuu hao wote uliowaorodhesha wameghubikwa na vitisho kupitia lile kundi maarufu la "Watu Wasiojulikana" (ingawa wanajulikana).
 
Wana JF! Hivi tuna Jaji Mkuu nchi hii?
Kwa wanaotaka kujua, hivi ndivyo ilivyokuwa wakati wa utawala wa Adolf Hitler...

The Third Reich was a police state characterized by arbitrary arrest and imprisonment of political and ideological opponents in concentration camps.

With the reinterpretation of "protective custody" (Schutzhaft) in 1933, police power became independent of judicial controls.

In Nazi terminology, protective custody meant the arrest—without judicial review—of real and potential opponents of the regime.

"Protective custody" prisoners were not confined within the normal prison system but in concentration camps under the exclusive authority of the SS, the elite guard of the Nazi state (wasiojulikana)
 
Sasa Je !tufanye nini !!??
Suluhisho la kudumu na litakaloirejesha nchi kwenye mstari mnyoofu na wa heshima ni PEOPLES REVOLUTION. MAPINDUZI YA UMA.

Haya mapinduzi yanapaswa yaanzishwe na raia kwa dhati kabisa bila kujali gharama zake.

Kwa mfumo huu, hakuna mabadiliko yatakayoshuka kutoka kwa wanasiasa wanaopigania matumbo yao.

Ila naamini, IPO SIKU watu wataamua na watawala watasikiliza.
 
Jaji mkuu amebweteka tu kama yai la bata mzinga wakati haki za wananchi zinaporwa na serikali, huyu Jaji Vipi anajua kweli maana ya kuwa Chief Justice!?
Hajui kabisa majukumu yake..

Kila nikikumbuka zile danadana za uteuzi wake na haya yanayotokea hivi sasa, naconclude kabisa kwamba he was first compromised before being confirmed..

Huyu ni CJ wa ovyo haijapata kutokea..

CJ kila shuguli ya Ikulu hata ambazo hazimuhusu yupo pale na anapewa nafasi ya kuongea..

CJ sio mtu wa kuwa hadharani-hadharani kila siku..ndio nature ya kazi yake.
Naam, hata akitokea hadharani wananchi mnasema hapa kuna jambo na kweli linakuwepo..

Kumbuka enzi zile za Retired CJ Samatta,humuoni ovyo ovyo na akitokea hadharani ni kwa jambo mahsusi linalomuhusu kiukweli..

Lakini huyu kwenye kuapishwa Ma DC yumo, kupokea report za ajabu ajabu sijui za Makinikia yumo..na anapewa nafasi ya kuongea..

Huku Mhimili anaoungoza ambao unapaswa kuwa HURU kwelikweli unaingiliwa na watawala na yupo tuu..

He is the WORST CJ Tanzania has ever had in its history.
 
Suluhisho la kudumu na litakaloirejesha nchi kwenye mstari mnyoofu na wa heshima ni PEOPLES REVOLUTION. MAPINDUZI YA UMA.

Haya mapinduzi yanapaswa yaanzishwe na raia kwa dhati kabisa bila kujali gharama zake.

Kwa mfumo huu, hakuna mabadiliko yatakayoshuka kutoka kwa wanasiasa wanaopigania matumbo yao.

Ila naamini, IPO SIKU watu wataamua na watawala watasikiliza.
Mkuu, umeongea UKWELI MTUPU bila ya kupepesa macho.
 
72 Reactions
Reply
Back
Top Bottom