Hivi TCRA wanaweza kutupa sababu za msingi kwa nini bei ya internet Tanzania ni zaidi ya mara kumi ya bei ya internet Rwanda?

Synthesizer

JF-Expert Member
Feb 15, 2010
11,143
18,774
Bei za internet ya wastani kwa Tanzania na baadhi ya nchi zinazotuzunguka ni kama ifuatavyo:

1575992086473.png


Source: Worldwide mobile data pricing: The cost of 1GB of mobile data in 230 countries
Reference: Worldwide Mobile Data Pricing League | Cost of 1GB in 230 countries - Cable.co.uk


Hivi TCRA wanaweza kutupa sababu za msingi kwanini Tanzania bei ya internet ni kubwa hivi ukilinganisha na jirani zetu kama Rwanda?

Rwanda wamefanya nini ambacho Tanzania hatuwezi? Bei ya internet ni kitu muhimu sana katika mambo ya uchumi, biashara na maendeleo ya taifa kwa ujumla. Sasa kwa nini serikali ya awamu ya tano isianzie hapa kabla hata ya kukimbilia kwenye miradi ya mabilioni?

NB: Zimbabwe inaongoza duniani kwa bei kubwa ya internet

Hii ni habari kulingana na utafiti na taarifa ifuatayo: Worldwide mobile data pricing: The cost of 1GB of mobile data in 230 countries

MICHANGO YA WADAU:
View attachment 1288779
safari com ya kenya 1 ksh=22.63 tsh
View attachment 1288782
Airtel uganda, 1 ush = 0.63 tsh
View attachment 1288780
airtel rwanda, 1rwanda franc = 2.5 tsh
View attachment 1288781
airtel tanzania.

Sasa naomba mniambie methodologies ambazo zimaetumika na hilo shirika kuonyesha Tanzania ina gharama kubwa za matumizi ya internet.

Nimechukua mitandao michache lakini hata tukienda kulinganisha kwa mitandao mingine bado price tz ipo chini.
=======
tatizo kubwa lililopo apa forum mnafarijiana uongo ili mradi uchangie tu mada:hakuna kitu utaniambia skijui katika hii field

infact usishangae tu kwamba wananunua internet bali kuna tozo pia kutumia kitu kinaitwa mkongo wa taifa: LTE cables built across the whole country, it works this way: ukipiga simu a wave is sent to a tower then from the tower its sent underground, it depends sasa hapa some use LTE ila ikishapita hapa kuna ofisi zinaitwa MSC (Mobile Switching center),

sasa hapa ndo mkongo wa taifa unaingilia kati, kwakua hakuna kampuni ya simu imejenga fibre optics kutoka mikoa yote kufika dar ambapo ni control centre ttcl walishafanya hivo kitambo sana na land lines zao za nyuma, wanaingia ubia na hapo wanalipa tozo ingine ya kupiga simu kutumia, we ulikua unadhan ni internet tu wananunua ujue kuanzia leo na access ya kupiga simu wananunua pia,(upuuzi ni watu wanafikiria kwamba things travel over air) ni shida ya kubisha hovyo bila kuelewa mambo


hapo ni upande wa kupiga simu: upande wa internet kuna kampuni ambazo zinahusika na internet kulingana na location uliopo: ukituma post yako ya jamii forum inapita kwenye mtandao wako wa simu alafu inapita kwa muuzaji wake wa internet then inapita under the ocean kukutana na cables zingine chini ya bahari zilizotengenezwa na makampuni mbalimbali mpaka message ifike inapotakiwa kufika na message itarudi tena in form of packets mpaka kwa simu ya mlengwa ama computer ama kifaa chochote kinachotakiwa kupokea hio packet: so mpaka hapa, mitandao ya simu inanunua alafu anaemuuzia mitandao ya simu nae ananunua, alafu tena nae ananunua and the trend goes that way: kelele nyingi mnapiga hapa ila mnaonekana mazuzu tu maaana hamjui mnachoongea

japokua ni mengi sana watanzania hatutaki kujua ila tunataka kukariri maisha na kubaki kuwaambia watoto mimi nlikua nakuaga wa kwanza darasani ilihali unashindwa kujua mitandao ya simu inanunua data
 
Nadhani ungeweka wazi hiyo 1GB kwa 11,500 ina maanisha nini hasa.
Mimi kwa matumizi yangu shilingi mia tano tu napata wastani wa MB 500 - 1GB kupitia Halotel.
Nikiwa na 10,000 napata GBs za kumwaga za kutumia zaidi ya siku 30.
 
Kwa hiyo wakuu, huyu jamaa kafungua sijui Excel yake na kaandika namba zisizo na kichwa wala miguu, then mmekaa serious kabisa mnakubaliana naye. Hamna link ya hii tafiti wala nini mtu kajiandikia tu vitu vyake.

Comparison ya kawaida Ya vifurushi vya Airtel Rwanda na Airtel Tanzania:



Hii kweli ni 10x ya utofauti wa bei per GB. Fanya conversion na unapata bei ni ile ile.
 
SIjawahi kununu 1GB kwa elfu kumi.

Hizi data umezitoa wapi????????
Utakuwa unanunua vifurushi ambavyo ni kama vina discount. Hii ni taarifa ya Worldwide mobile data pricing: The cost of 1GB of mobile data in 230 countries

 
Kwahiyo mkuu umeamini kabisa 1GB kwa Tanzania ni wastani wa Tsh. 11,500/-?
Mkuu, tunapoongelea bei ya data usikaze fikra kwenye vifurushi vya makampuni ya simu. Sana sana angalia labda subscription rates za data kwa mwezi
 
Hizi taarifa taarifa sidhani kama ni za kweli, tz kwa afrika mashariki ndo ina internet ya bei nafuu kuliko nchi yoyote tukizungumzia mobile internet. Tuekee chanzo cha taarifa yako.
Tayari Mkuu, nimerekebisha na kuweka chanzo. Ila sasa usiseme ni uongo wa mabeberu.
 
Nadhani ungeweka wazi hiyo 1GB kwa 11,500 ina maanisha nini hasa.
Mimi kwa matumizi yangu shilingi mia tano tu napata wastani wa MB 500 - 1GB kupitia Halotel.
Nikiwa na 10,000 napata GBs za kumwaga za kutumia zaidi ya siku 30.
Kuna mambo kadhaa lazima uzingatie. Unaweza ukaweka 1GB na kuwa unatumia kwa ajili ya WhatsApp message tu, inaweza kukaa zaidi ya siku 30. Sasa lazima uangalie bei kwa namna inayotoa ulinganifu, kwa mfani, IGB ita download data kiasi gani kwa nchi mbalimbali, sasa hiyo ndio itakupa ulinganifu wa bei. Utakuta kwa Rwanda labda, 1 GB uta download kitabu kizima chenye chapter 10, wakati Tanzania uta download chapta moja tu ya kitabu hicho.

Halafu, ukitaka kujua uhalisi wa bei, nunua airtime ya kama Tshs 20,000 bila kuingia kwenye kifurushi cha data halafu download mziki mmoja tu ndio utajua uhalisi wa bei ya 1GB hapa Tanzania
 
Ukitaka kujua kuwa bei ya data ni kubwa, weka salio bila kujiunga halafu endelea ndo utajua thamani halisi ya kifurusi. Hicho ndo kimefanyiwa tafiti. Haya mambo ya kujiunga ni uhuni tu
Ahsante sana kwa ufafanuzi mzuri sana Mkuu. Watu humu wanabisha kwa bei za vifurushi vya data ambazo ni discounted data prices! Umeeleza vizuri sana maana ya bei ya data. Thanks.
 
Kwani mkuu GB 1 wewe huwa unainunua kwa shilingi elfu 11500 au hujui tafiti zimefanyiwa ulaya
Ulaya ambako ndiko tunapeleka wataalamu wetu kujifunza research methods, sivyo? Baada ya kufundishwa na hao mabeberu sasa tunajifanya tunajua kufanya utafiti kuliko wao, au tuanataka kukandia utafiti wao kuwa hawajui kufanya utafiti?

Hebu soma taarifa ya Mkuu Rushanju hapa chini nione kama una neno zaidi;

Ukitaka kujua kuwa bei ya data ni kubwa, weka salio bila kujiunga halafu endelea ndo utajua thamani halisi ya kifurusi. Hicho ndo kimefanyiwa tafiti. Haya mambo ya kujiunga ni uhuni tu
 
Back
Top Bottom