OLS
JF-Expert Member
- Oct 12, 2019
- 419
- 670
TCRA katika taarifa yao kuhusu ufafanuzi wa bei za data iliyotolewa Mei 9, 2022 ilionesha kuwa zaidi ya 95% ya watanzania hutumia data kwa kujiunga vifurushi vinavyotolewa na mitandao. Yaani watanzania hawatumii internet kabla ya kujiunga na kifurushi.
Suala hili limenifanya niangalia kwa mwezi Juni watanzania walitumia Tsh ngapi kwa kuangalia taarifa zinazotolewa na TCRA kila robo ya mwaka. Kwa mwezi Juni 2023, watanzania walitumia terabyte 83 ambazo ni sawa na Megabytes(MBS) 88,627,220,736. Kwa kuangali kwa wastani katika vifurushi bei ya mb moja ni Tsh 2.25 ambapo ukizidisha utapata Tsh. 199,411,000,000 yaani bilioni 199.41.
Fedha zinazotumika kununua data ni kubwa kwa 64% ya fedha zinazotumika kwa kupiga simu na kutuma sms. Hii inaonesha kuwa watanzania wanatumia zaidi data kwa mawasiliano kuliko kupiga simu au kutuma sms.
Ukiangalia matumizi ya serikali kwa mwezi June 2023 ilikuwa ni Tsh Trilioni 2.35. Yaani hapa nasema, matumizi ya raia kwenye kununua data ni sawa na 8% ya matumizi ya serikali(Total expenditure and net learning).
Kaa humo. Mimi naenda kula mabungo.
Signed OLS