Hivi TANESCO na Tanga Cement kunani lakini?

Tanesco clears Tanga Cement on 49m/- bills

2007-12-01 08:52:04
By Guardian Reporter


The Tanzania Electric Supply Company (Tanesco), which on Thursday gave Tanga Cement Company only a day to pay what it called overdue power bills amounting to some 49m/-, yesterday said it had discovered that payment had been long effected after all.

Tanesco Managing Director Idris Rashid told a hastily called news conference on Thursday afternoon that they had given the Tanga firm until yesterday to pay the bills or face an immediate power cut.

He said they had already sent the cement company a note reminding it on the need to clear its bills by the deadline.

But yesterday Tanesco explained in a letter addressed to the TCC managing director, a copy of which was faxed to this paper, that they had no problem with the cement company regarding the outstanding payment earlier referred to.

Part of the letter read: `We want to confirm to have received your outstanding payment amounting to 49,041,763.20, which you paid on November 21, 2007 well before elapsing of the set deadline of November 30, 2007.`

In the letter, signed by William Mhando on behalf of the MD, Tanesco states that it is all out to maintain smooth supplier-customer relations for mutual benefit.

TCC Managing Director Juerg Fluehmann meanwhile said in a letter to the Tanesco management - alongside a similar one addressed to this paper - that his company had paid the purported outstanding bills amounting to 49,041,763.20/- by cheque No. 002885 on November 21, 2007.

He added that they also paid re-connection and inspection fees amounting to 6,609,000/- by cheque No. 002886.

Fluehmann said his firm was listed with the Dar es Salaam Stock Exchange and that any negative reports on its financial reputation might cause shifts in market confidence and erode the market value of its shares.

A senior official with TCC speaking on authority stressed on Thursday that they had already settled the amount in question `through a cheque that was duly collected by the Tanga Regional Tanesco Manager on the 21st of this month`.

`If these people (Tanesco) continue to behave this strangely and really make good their power disconnection threat, we shall have no option but to seek legal redress,` said the official, adding that there was proof that the cheque in question had already been cleared with the respective bank.

Production at the Tanga firm stopped for 24 hours last week after Tanesco cut the power supply line that feeds it, charging that it (TCC) had tampered with electricity flow and consumption monitoring equipment and defaulted on the payment of the 49m/-.

The media quoted MD Fluehmann as swiftly denying the charges.

He said the measure taken by the power company violated the law on the supply of electricity, which he said stated that consumers must be served with a written notice of at least 48 hours before disconnection is effected.

An emphatic Fluehmann explained that their monthly electricity bill ranged between 450m/- and 500m/- and swore that they had always paid on time.

Power to the cement firm was restored the very next day without any condition, apparently on orders from the Tanesco Board of Directors.

SOURCE: Guardian

Sasa mtaelewa maana ya arbitration! Milioni 49 itatutokea puani. Nimesema ni ubabaishaji tuu! Huyu Dr. kabla ya kutoa vitisho hivyo hakuwauliza wachini yuake nini current situation? Halafu hawa ndio mnategemea watatukomboa.Twafa.
 
Sitashangaa nikisoma TCC wamepata source nyingine ya umeme wa kuendeshea kampuni yao. Kwa yeyote anayejua biashara anajua
the bargaining power of big customers (Porters five forces). Unaweza kuwanyanyasa customers wadogo wadogo lakini sio kampuni kubwa kama TCC.

Leo TCC wakipata umeme wao au wakiamua kutumia makaa ya mawe, Tanesco watapata hasara kubwa sana maana hizo 500M zilizopotea watazitoa kwa nani?

Sisemi Tanesco iwaonee huruma TCC, hapana , ninachosema ni kwamba TTC ni strategic partner wa Tanesco kwahiyo inabidi wawe wanaongea na kuwe na mawasiliano ya mara kwa mara ili hata kama kuna tatizo, wakae chini na kuangalia namna ya kulitatua. Kampuni inayolipa 500M kila mwezi, kweli utasema wameshindwa kulipa 49M, hivyo wakatiwe umeme?

Lakini kila nikisoma walivyofanya Tanesco, naanza ku question hata busara na pia management skills za huyo MD wao. Ndio maana Tanzania tumeua mashirika yote ya umma maana kama watu wenyewe ni hawa, unategemea wewe ungekuwa customer utafanya nini? Unahamia kwingine. Tanesco wanatamba shauri ya monopoly lakini wanasahau kwamba huku nje viwanda kama TCC hawatumii umeme wa namna hiyo kwasababu ni aghali. TCC nao wanaweza kupata njia nyingine ya kuendeshea viwanda vyao na itakuwa pigo kwa Tanesco.
 
Wayego TCC jengeni mtambo wenu wa umeme achaneni na TANESCO wasiojua kumjali mteja. Yaani mtu anakulipa Shs 500millioni kila mwezi na unashindwa ku-negotiate deni la shs 45million mpaka kumkatia umeme? Hii ni kutafuta cheap popularity na ni moja ya tabia ya ukiritimba!! Naamini VAT na kodi zingine kwenda serikalini kwa mwezi na zaidi hata mara kumi ya hilo deni. Huu ni mfano wa dysfunctional decisions zinazofanyika. Kwanza ni aibu mtu aliyetangaza kuacha kazi kwa uamuzi wake mwenyewe halafu unamrudisha. Huku ni kujenga hisia kuwa kuna watu ambao ni indispendable kwenye nyadhifa fulani na kumvimbisha kichwa mhusika.
 
Dr. Idris Rashid oyeeeeeee.

Hatutaki ubabaishaji, kila anayedaiwa lazima alipe bill yake, kama hicho kiwanda kinamtu kinamtegemea serikalini shauri yake, Dr. Idriss wewe fanya kazi ili Tanesco iweze kurudi kwenye hali yake... ukikubali siasa zikiendeshe kiwanda hapo kutakuwa hakuna kusonga mbele.

Mkuu,

Kama nilichosoma magazetini ni kweli, basi Rashid hastahili pongezi, anastahili kuwa sacked.

Kama director wa Tanesco anaweza kufanya hivyo, hapo tuna tatizo, tena tatizo kubwa sana. TCC sio wewe na mimi ni customer mkubwa ambaye anahitaji special attention. Ilitakiwa Tanesco wawe karibu sana TCC na kuongea nao mara kwa mara. Lakini kwenye hili yaani sio tatizo kabisa maana sio kama TCC wameshindwa kulipa bali kulikuwa na kutokuelewana kati ya hawa wakubwa wawili.

Monopoly ya Tanesco ikiondolewa, Tanesco watakufa baada ya muda mfupi maana shirika lingine haliwezi kufanya kama walivyofanya Tanesco.
 
Monopoly ya Tanesco ikiondolewa, Tanesco watakufa baada ya muda mfupi maana shirika lingine haliwezi kufanya kama walivyofanya Tanesco.

..simply bei ya umeme itapanda mara dufu!na serikali haitaweza kuingilia kati kama sasa,maana itakuwa ni biashara huria!

..ukweli ni kuwa kwa current situation umeme unatakiwa uwe bei maradufu ya hii!

..huwezi fanya biashara ya umeme kwa bei hizi,labda kama unatoa huduma!
 
Heshima kwa WanaJambo wenzangu. "Mbalamwezi" ameanzisha mjadala mzuri sana kwakweli.... Mimi nimechanganyikiwa pale ambapo katika siku moja, TANESCO wanakubali kuwa Tanga Cement hawadaiwi(Guardian 01 December 2007);Na wakati huo huo Tanga Cement wanasema wanawa "SUE" TANESCO kutokana na hasara waliyoipata (Daily News, 01 December 2007). Hapo kwa kweli mimi jasho linanitoka kuelewa niamini lipi?? Na mzee wetu Dk Idris Aliondoka (so they said) na kurudi within few hours (siwezi kusema ni siku, less than 72hrs ni hours)...

Tafadhali someni hii:

TITUS KAGUO
Daily News; Saturday,December 01, 2007 @00:05


TANGA Cement Company said yesterday that it intends to sue the Tanzania Electric Supply Company (Tanesco) demanding 2bn/- in damages for causing massive business loss to the firm and injuring its corporate image.
Professor Samuel Wangwe, a member of the firm's Board of Directors, told a news conference that Tanga Cement suffered heavy losses after Tanesco unilaterally disconnected power at its plant for about 30 hours on November 20 and November 21.
Prof. Wangwe, who was addressing the press on behalf of the Chairman of the firm's Board of Directors, Mr Dave King, said apart from lost business estimated at around 7m/- per hour when power went off at the plant, the reputation of the cement makers was also soiled during the crisis.
The disconnection was a result of 49m/- disputed power supply bill to the plant, when meter reading was interrupted after installation of a device to monitor the flow of power.
Prof. Wangwe said the disputed 49m/- bill was settled on November 21. "We also paid 6.6m/- reconnection charges," he added.
"We are the biggest consumers of power with monthly bills of around 450m/-, it is surprising Tanesco chose to mudsling us instead of resolving our disputes amicably," Prof. Wangwe said.
He said although Tanesco had many shortcomings in delivery of its services including erratic power supply and provision of low voltage, Tanga Cement had never claimed compensation nor attacked it in the press.
"We have always opted to talk and work closely with Tanesco," he said.
The Public Relations Manager of Tanesco, Mr Daniel Mshana, declined to comment yesterday saying the matter would be handled by the firm's lawyers.
He said the press conference convened by Tanesco on Thursday had nothing to do with the Tanga Cement Company.
He refuted reports by a local weekly that President Jakaya Kikwete and the Prime Minister, Mr Edward Lowassa, differed over resignation of Tanesco Managing Director, Dr Idris Rashid.

Copyright @TSN 2007 All Rights Reserved
 
Hii ndiyo management tuliyozoea! Populist na ubabe. Nilishasema awali ni kawaida ya Tanesco kukubambikia bill na kukwambia kuwa lipa kwanza ndiyo tujadiliane. Samahani lakini naona wengi wetu bado tunapigana vita tuliyoishinda miaka 46 iliyopita. Tunamtetea Idris kwa sababu tu ni mswahili mwenzetu dhidi ya hao waliowahi kututawala. Mteja mkubwa sehemu yeyote duniani anaheshimiwa. Si huku kupanda majukwaani na kutoa vitisho visivyo na msingi. Sasa akikata umeme, atakayefaidika nani? Mimi sitashangaa hawa mabwana watakapoiburuta Tanesco mahakamani kwa kutofuata mkataba( soma taarifa ya boss wa Tanga Cement) na Tanesco kuamriwa kulipa mabilioni. Tumeona yakifanyika Mwanza, IPTL n.k. Hamna jipya hapa, ni kutafuta umaarufu tuu. Na sasa bodi imenyamazishwa ndiyo tutakoma kabisa. Kwa vitendo hivi kweli tunategemea kuvutia wawekezaji wa maana? Disputes ni kawaida ya mikataba na zina njia ya kuzitatua lakini sio hivi. Bora angeenda.

NO,NO,BIG NO!
wawekezaji,No i mean WACHUMAJI hawawezi kupungua nchi hii,
Ikiwa kama MR.President Mwenyewe akikujua tu kwamba wewe ni mtu makini na umeishi nnje kwa kipindi kirefu atakuita akuambie "Thatha Lete basi Wadhungu wawekeze nchini"
Sasa jamani namna hii tuna wawekezaji au matapeli ambao wasio nauchungu na nchi yao wanakula nao.Na hii ndio maana tuna wawekezaji FAKE wanokula kona kila kukicha na mapesa yetu ss tumebaki kusema wawekeaji nani kakuambia?,wezi tu wote hao!
Umesikia kwamba yule Msouth wa MILLENIUM HOTEL kala kona!?
Sasa mtu(MUWEKEZAJI) serious anaweza kukimbia na pesa ya nchi kama hii?
 
Kuna mtu yoyote anayejua undania wa kilichotokea kwenye hiyo mita?
 
NO,NO,BIG NO!
wawekezaji,No i mean WACHUMAJI hawawezi kupungua nchi hii,
Ikiwa kama MR.President Mwenyewe akikujua tu kwamba wewe ni mtu makini na umeishi nnje kwa kipindi kirefu atakuita akuambie "Thatha Lete basi Wadhungu wawekeze nchini"
Sasa jamani namna hii tuna wawekezaji au matapeli ambao wasio nauchungu na nchi yao wanakula nao.Na hii ndio maana tuna wawekezaji FAKE wanokula kona kila kukicha na mapesa yetu ss tumebaki kusema wawekeaji nani kakuambia?,wezi tu wote hao!
Umesikia kwamba yule Msouth wa MILLENIUM HOTEL kala kona!?
Sasa mtu(MUWEKEZAJI) serious anaweza kukimbia na pesa ya nchi kama hii?

Unamlinganisha Msouth wa Millenium Hotel na TCC? Vitendo kama hivi ndiyo vinawafanya investors wa calibre ya TCC kusita kuwekeza nchini na kutubakizia hao wa Millenium Hotel!
 
NO,NO,BIG NO!
wawekezaji,No i mean WACHUMAJI hawawezi kupungua nchi hii...,
Ikiwa kama MR.President Mwenyewe akikujua tu kwamba wewe ni mtu makini na umeishi nnje kwa kipindi kirefu atakuita akuambie "Thatha Lete basi Wadhungu wawekeze nchini"
Sasa jamani namna hii tuna wawekezaji au matapeli ambao wasio nauchungu na nchi yao wanakula nao.Na hii ndio maana tuna wawekezaji FAKE wanokula kona kila kukicha na mapesa yetu ss tumebaki kusema wawekeaji nani kakuambia?,wezi tu wote hao!
Umesikia kwamba yule Msouth wa MILLENIUM HOTEL kala kona!?
Sasa mtu(MUWEKEZAJI) serious anaweza kukimbia na pesa ya nchi kama hii?

Mkuu, weka hoja zako zieleweke na tujadili. Unapinga uwekezaji au unatetea?

Kumbuka tulikotoka, ambapo bia ilikuwa uwe na kibali maalum ili uweze kunua kwa sharehe yako ya ubatizo...na sigara za ulanguzi...na hata mafuta ya kupaka tu ya Rays yalitoka Kenya. Tulishindwa kuendeleza mashirika na makampuni yetu wenyewe, japo tuna malighafi kibao hapa, tumlaumu nani, wageni?

Hata kama kuna matapeli kati yao, si wote...yule aliyekimbia na hela za LAPF ndo anatoa picha ya wote kweli?

Unajua kodi kubwa kabisa zinalipwa serikalini na Sigara, TBL, Tanga Cement, Twiga Cement, Mbeya Cement? Na ambazo zinatumika kukujengea bara bara wewe mwananchi? Kabla ya mageuzi haya ya kiuchumi, tulijenga bara bara zipi hasa kwa pesa ya walipa kodi (makini hapa, usichanhanye pesa za misaada?)

Tanesco wamechemsha, na Dr Idris kapigiwa simu na Finance manager wa Tanga Cement over 50 times hajawahi kupokea hata moja, ni biashara ya namna gani wanafanya hawa? wanauza sura?

Wakati Idris anaamrisha Tanesco wakate umeme Tanga Cement 20.10.2007, kulikuwa na kikao cha majadiliano kinaendelea btwn the two, na huku wanakata umeme ebo!

Na Tanga Cement wakalipa siku iliyofuata...kumbuka, hii 49 haikuwa kwenye bill ya kawaida, ilikuwa kwenye mgogoro, maana yalikuwa makadirio ya nyongeza tu...hata tunapotetea haya ma uzalendo, tuwe makini tusipendelee tu ali mradi.

Pamoja na blanda yote hii, wanasema "Tanesco i me clear TCC..."yaani hawaombi hata radhi? Napata shaka sasa .Dr Idris
 
Unamlinganisha Msouth wa Millenium Hotel na TCC? Vitendo kama hivi ndiyo vinawafanya investors wa calibre ya TCC kusita kuwekeza nchini na kutubakizia hao wa Millenium Hotel!

Fundi, yule alikuwa mpangaji tu wa Millennium building...kwa ajili ya biashara ya nyumba ya kulala na sehemu ya ugali..kuwa investor tunamkweza hasa. Na unaweza kuona udhaifu ktkt mkataba ndo umempa upenyo wa kuanza na pango, si unajua competence yetu kwenye mikataba?
 
JK amtoe Dr. Idrisa kwenye uongozi wa TANESCO. HAFAI. Period. Kama MD hawezi hata kujua nani ni mteja mashuhuri kwake, basi ni kipofu kuliko hata jongoo.
 
Sitashangaa nikisoma TCC wamepata source nyingine ya umeme wa kuendeshea kampuni yao.

Haswaaa Mkuu,

TCC wako mbioni kufunga mtambo wa nishati, pengine within next month watatangaza tenda. Millioni 500 bili ya mwezi hiyooooo Dr Idris anaikosa...

TCC wanasema japo wanahitaji 33,000 KV kuendeshea mitambo yao, supply ya Tanesco imekuwa around 20,0000 na kiduchu..."Tunavumilia hata quality ya umeme tunaopata toka Tanesco," Prof Wangwe.
 
Hivi hatujiulizi kwa nini tunapotangaza kuuza mashirika yetu kama ya Simu, Maji,Reli n.k hakuna invetor wa maana anayejitokeza isipokuwa fake kama Richmonds, City Water n.k? Hakuna serious investor atawekezeza kwenye mazingira kama haya tunayoyaona!M.D wa utility company anakataa kupokea simu kutoka kwa strategic investor wake? Mangapi yangeokolewa kama angepokea hiyo simu!
 
Haswaaa Mkuu,

TCC wako mbioni kufunga mtambo wa nishati, pengine within next month watatangaza tenda. Millioni 500 bili ya mwezi hiyooooo Dr Idris anaikosa...

TCC wanasema japo wanahitaji 33,000 KV kuendeshea mitambo yao, supply ya Tanesco imekuwa around 20,0000 na kiduchu..."Tunavumilia hata quality ya umeme tunaopata toka Tanesco," Prof Wangwe.

Na bado! Kwa bei hizo wanazotaka kutoza, wengi tutakimbilia solar, kupikia bio-gesi n.k!
 
NO,NO,BIG NO!
wawekezaji,No i mean WACHUMAJI hawawezi kupungua nchi hii,

Unataka kujua kwa nini unawaona hawa wachumaji? Soma hapa:

Akizungumza jana jijini Dar es Salaam, Waziri Mkuu wa Canada, Stephen Harper, alisema kuwa uwekezaji katika sekta ya madini nchini unafanywa kwa kutumia sheria za ndani za nchi, hivyo kasoro zinazojitokeza kwenye madini ni matokeo ya ubovu wa sheria hizo.

Umeelewa?
 
..simply bei ya umeme itapanda mara dufu!na serikali haitaweza kuingilia kati kama sasa,maana itakuwa ni biashara huria!

..ukweli ni kuwa kwa current situation umeme unatakiwa uwe bei maradufu ya hii!

..huwezi fanya biashara ya umeme kwa bei hizi,labda kama unatoa huduma!
Dar si Lamu,

Una uhakika na hili? Mimi umeme Dar kwenye nyumba yangu nalipia pesa nyingi zaidi kwa mwezi kuliko ninazolipa hapa UK, why? Wakati gharama za uendeshaji kwa vyovyote UK ziko juu mno hasa kwenye mishahara na pia matumizi yangu ya umeme hapa ni makubwa zaidi ya nikiwa Dar.

Wakiondoa monopoly ya Tanesco huenda bei zikashuka. Wasiwasi wangu tu ni kwamba wakiondoa monopoly basi hao wawekezaji wapya wata concentrate mijini na kuacha sehemu kubwa ya nchi bila umeme. Lakini Tanesco inabidi wabadilike na waache ujinga huu wanaofanya wa kujifanya wao ndio miamba.

Kwasasa tungeweka nguvu kubwa kutumia makaa ya mawe kwenye kuzalisha umeme, hii litaleta ajira kwa watu wetu na pia linaweza kupunguza gharama za kuzalisha umeme, japo kutakuwa na madhara kwenye mazingira. Lakini makaa yenyewe, kama wenye nayo ni akina Big Mkapa, unategemea nini? Watazalisha makaa yamejaa matope, wanataka wakamue ng'ombe wao mpaka anaanza kutoa damu.

Pia solar power bado ni aghali sana Tanzania. Jua tunalo la kutosha, tunge encourage matumizi ya solar na pia kuwapa incentives watengenezaji ambao wangetengeneza hizo panel kwa wingi hapo TZ hapo TZ, matokeo yake bei yake ingeshuka sana, mahitaji ya umeme wa Tanesco yangepungua, mambo yaliyotokea 2006 tusingeyaona tena.
 
Hivi hatujiulizi kwa nini tunapotangaza kuuza mashirika yetu kama ya Simu, Maji,Reli n.k hakuna invetor wa maana anayejitokeza isipokuwa fake kama Richmonds, City Water n.k? Hakuna serious investor atawekezeza kwenye mazingira kama haya tunayoyaona!

Malizia, hayo ni :

1. mazingira duni ya nishati, yanayosababisha daily investment operational costs ziwe juu, na hivyo kufanya hata bidhaa ziwe bei ghali zisizoweza kushindana na na bidhaa za nje,

2. Hata baada ya kubadilisha sera za uchumi wetu, Watu wetu wengi wanakumbatia mawazo mgando, yasiyobadilika na mwenendo mpaya wa uchumi wa dunia...unafanya biashara "without being business minded," hutaweza.

3. Wengi hatutaki kuelewa kuwa "market economy is an economic model based on competition."

4. Ukikubali mfumo huu, ujue ni kama soka: unacheza ili ushinde, na si kucheza ukijifanya mpinzani wako anawajibika akuonee huruma ili ushinde!
 
Ndugu Mtz na Dar,

so far Tanesco hawana ukiritimba tena wa kuzalisha umeme. Kuna players ktk power generation wengine kama IPTL, ambao umfumo huu unaitwa Public Private Partnership. Tatizo bado ku liberalize power supply.

Tusisahau pia kuwa u ghali wa kuendesha Tanesco unatokana na kulipa wazalishaji binafsi pesa nyingi sana, na hii ni matokeo ya mikataba mibovu.

Mfano, 2004 Tanesco walikusanya sh 188.5 bn, wakawalipa wachovu IPTL na wengine sh 124.6 bn (usishangae, unashangaa nini? sijakosea, maji yamezidi unga), 2005,walikusanya sh 221.5 bn, wakawalipa hao washkaji wengine sh 176 bn. 2006, wamekusanya 232 bn, wakawapa hao wazalishaji wengine 242 bn. Mwaka huu, miezi 9 ya mwanzo, wamekula hasara ya zaidi ya 58 bn.

Kuna tatizo la ki ufundi pia, kwamba umeme mwingi unaibiwa kuliko ule unaolipiwa na wateja.

Taasisi nyingi za serikali ni wanaiwa wakubwa. Siasa zinatumika ku neutralize hii.
 
Back
Top Bottom