Ndugu Mtz na Dar,
so far Tanesco hawana ukiritimba tena wa kuzalisha umeme. Kuna players ktk power generation wengine kama IPTL, ambao umfumo huu unaitwa Public Private Partnership. Tatizo bado ku liberalize power supply.
Tusisahau pia kuwa u ghali wa kuendesha Tanesco unatokana na kulipa wazalishaji binafsi pesa nyingi sana, na hii ni matokeo ya mikataba mibovu.
Mfano, 2004 Tanesco walikusanya sh 188.5 bn, wakawalipa wachovu IPTL na wengine sh 124.6 bn (usishangae, unashangaa nini? sijakosea, maji yamezidi unga), 2005,walikusanya sh 221.5 bn, wakawalipa hao washkaji wengine sh 176 bn. 2006, wamekusanya 232 bn, wakawapa hao wazalishaji wengine 242 bn. Mwaka huu, miezi 9 ya mwanzo, wamekula hasara ya zaidi ya 58 bn.
Kuna tatizo la ki ufundi pia, kwamba umeme mwingi unaibiwa kuliko ule unaolipiwa na wateja.
Taasisi nyingi za serikali ni wanaiwa wakubwa. Siasa zinatumika ku neutralize hii.
Mbalamwezi,
Lengo la PPP ni kwamba iko proved kwamba private companies are more efficient when it comes to delivering services compared to public organisations, hence a need to use private companies in delivering these services. Lakini kinachotumika hapo ni kinyume maana umeme wa IPTL ni aghali zaidi na mara nyingi hata hawazalishi lakini wanalipwa. Kwa maoni yangu hiyo si PPP tena bali ni ufisadi.
Serikali inatakiwa ifungue soko la solar energy ili wasindane na Tanesco hasa kwenye maeneo ya mikoani.
Tanesco hawatakiwi kusaini mkataba na mtu au shirika lolote, wanachotakiwa sana sana ni MOU kuonyeshakwamba kama bei itakuwa reasonable watanunua umeme huo. Hivyo mtu yeyeote mwenye uwezo anaweza kuanza kutengeneza umeme na kuwauzia Tanesco. Kitakachoamua ni bei. Hii ni kinyume kabisa na ilivyo sasa.
Nakubaliana na wewe kwamba serikali yenyewe ni wadaiwa. Hapa Tanesco inabidi wawe wakali, ukiondoa idara nyeti kama hospitali, naona idara zingine wakatiwe tu kama hawalipi.