Hivi Suma G uko wapi?

Balozi yuko kwa Trump,ila Saigon sijui kapotelea wapi
Saigon kaacha mziki na sasa yupo kidini zaidi kama mzee yusufu. Angekuwa mkristo ungesema ameokoka. Balozi anaendelea na mziki na katoa ngoma nyingine.
Hizi ni kama nilivyosikia ila sina hakika.
 
Ukimpata nitafutie pia

Jose mtambo wa kigambonino
Mnyalu
Caz T
Wale wanyama wa BDP (big dog pond)
Dula soul
Na wanyamakwinqwi wengine wa jamii ya hao niliowataja
Jose Mtambo hivi sasa ni mlevi wa gongo tena aliyepitiliza sidhani kama kaacha.
Muziki aliacha kuimba baada ya kutapeliwa na promota wake aliyeuza albamu nzima kwa Mhindi. Tena bila kupata hata senti, Mhindi naye akamtosa hata alipojua mwimbaji ni yeye na kwenye kasha ka albamu kuna picha yake.

"Ya nini niimbe halafu faida wanapata wengine, mimi sipati chochote", maneno yake aliyoyasema baada ya kukata tamaa kabisa ulevi ukawa ni suluhu yake.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom