Hivi sisi watanzania ni waoga, wajinga au tumelogwa? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hivi sisi watanzania ni waoga, wajinga au tumelogwa?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Ta Muganyizi, Jan 21, 2011.

 1. Ta Muganyizi

  Ta Muganyizi JF Gold Member

  #1
  Jan 21, 2011
  Joined: Oct 19, 2010
  Messages: 5,134
  Likes Received: 413
  Trophy Points: 180
  Nimesoma muda mrefu na kusikiliza makundi mbalimbali humu nchini pamoja na wananchi kwa ujumla dalili zote zinaonesha watanzania wamechoka.

  Kama kuna mtu aliangalia TBC jana muda wa saa 4:30 utaona wazee na vikongwe walivyokata tamaa ya kuishi. Wengine walidiriki kusema wanasubiri kufa tu maana wanaona hata aibu kusema wao ni watanzania ambao wanaishi katika nchi ambayo inaamini maisha bora kwa kila mtanzania. Serikali iliwatoza kodi walipokuwa vijana na kilichoko sasa ni matunda ya juhudi zao wakiwa na nguvu za kuzalisha, lakini sasa wao wanaoneka ni takataka.

  Pili ndani ya ccm watu wanaona jinsi nchi ilivyoenda mrama kila anayetaka kuiba anaiba tu raslimali hakuna wakusema chochote. Madini yanazidi kuibiwa, miundo mbinu kama reli vimeharibika, umaskini unaongezeka, ufisadi ndo usiseme yaanin kila kitu tabu lakini mkuu wa kaya kimyaaaaaaaa.

  Wananchi woote wanashangaa wanajua kabisa kuwa nchi iko pabaya. Sasa njia muafaka ni ipi?

  Mapinduzi........mapinduzi.........mapinduzi inabidi yafanyike tena ya umma kama huko Tunisia lakini nani aanzishe? Watu waoga kama nini. Wamechoka na uonevu lakini maneno ya kulaumu ndo mengi. Sasa inabidi tutoe maneno ya kufikia muafaka tufanyeje? Nikitoa ushauri hapa si ajabu thread hii ikaondolewa kuwa nitasababisha matatizo nchini hivyo tubaki hivi hivi tu jamaa waendelee kuila nchi yetu. Siku moja nilishauri kuwa Jwtz waangalie mwenendo wa nchi lo!. Naomba tukubalianae katika jukwaa hili tufanyeje ili tubadilishe hali hii. Lile la kusubiri uchaguzi hadi 2015 naona limezoeleka na bado kura zitaibiwa tu. Waadhiri vyuo vikuu wamechoka, wanafunzi wamechoka, wafanyakazi wamechoka, polisi hoi wanaona ni bora walale kwenye lindo kule benki kuliko home kwao walikopanga, kila sekta wamechoka sasa tunasubiri nini?

  Naomba wadau mtaje hapa chini nani aanzishe ili wengine tufuate.... nikieleza mie kama hapo awali thread inapotea. Jamani ni hivi "Bora kuwa maskini lakini huru, kuliko kuwa tajiri lakini mtumwa" Mapinduzi muhimu jama na muda ndo huuu, tuandamane nchi nzima auuuu????? na nani aanzishe kutoa tamkoooo????? aghhh. Jeshi la JWTZ si kweli kuwa la wananchi, linalinda wachache aaaahh. Nikiendelea nitaambiwa mie mhaini, jamani kulaumu kumeisha tutoe suluhishoooo. Tajeni basi hapa chini nani aanzishe??? Mie nampendekeza Mwakyembe wewe je?
   
 2. Ng'wanangwa

  Ng'wanangwa JF-Expert Member

  #2
  Jan 21, 2011
  Joined: Aug 28, 2010
  Messages: 10,179
  Likes Received: 895
  Trophy Points: 280
  waoga kweli.

  Si unaona hata hawachangii thread yako!?
   
 3. Crashwise

  Crashwise JF-Expert Member

  #3
  Jan 21, 2011
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 22,172
  Likes Received: 862
  Trophy Points: 280
  Ikifika muda wake hutakuwa na haja ya kutafuta wa kuanzisha na hutoelewa nani kaanzisha.....kwani polisi waliamini ujasili wa vijana uliotokea Arusha na Mbeya

  ...acha tuchukue mafunzo taratibu, sasa hivi tumesha jifunza jinsi ya kukabiliana na mabomu ya mashozi na risasi kwambali na jinsi ya kuandamana kwenda sehemu husika hili mimi nilikuwa silijui kabisa kumbe ni hakiri ndogo tu, kinachofata sasa hivi ikitokea soo kama la Arusha kitaeleweka tu....na ninaomba siku hiyo kiwake nchi nzima ili polisi kama ni wa moshi basi wabaki moshi na kama ni Arusha wabaki Arusha hapo mbona patakuwa patamu
   
 4. Ta Muganyizi

  Ta Muganyizi JF Gold Member

  #4
  Jan 21, 2011
  Joined: Oct 19, 2010
  Messages: 5,134
  Likes Received: 413
  Trophy Points: 180
  Sana mkuu mie nakwambia watanzania tuna wadudu vichwani. Sioni wa kuanzisha moto ni nani
   
 5. Azimio Jipya

  Azimio Jipya JF-Expert Member

  #5
  Jan 22, 2011
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 3,370
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135

  Mkuu mbona mambo yanakwenda vizuri tu!
  ... maandalizi yako stage muhimu...!
  ... Vikao huhudhurii nini?
  ... Hakuna shida kabisa ... Hakuna linaloharibika ingawa inaonekana hivyo..
   
 6. B

  Bull JF-Expert Member

  #6
  Jan 22, 2011
  Joined: Nov 4, 2008
  Messages: 984
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kwanini mnafikiria mabadiliko ya fujo badala ya kuwaelimisha watanzania waliochoka kukikchagua chama ambacho unaona kitakuletea maendeleo ??? Nadhani ni kwasababu chama unachokiamini, hakikubaliki kwa watanzani,
   
 7. Najijua

  Najijua JF-Expert Member

  #7
  Feb 23, 2011
  Joined: Nov 5, 2010
  Messages: 1,029
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Ndugu zangu watanzania naumia sna na mambo yanavyokwenda katika hii nchi yetu kipenzi iitwayo Tanzania Ambayo kwa wachache wananiita Shamba la bibi kwa kuwa mjanja masikini anaweza amka tajiri.
  1. Tumeona na kiusikia mmiliki wa DOWANS ametua nchi tena na kafanya Press Conference lakini hakuna reaction zozote toka kwetu wakati huyu ndiye anayesababisha matatizo na umasikini wote unaokuwa kwa kasi kila kukicha.

  2. TANESCO wamepandisha gharama za umeme hakuna reaction zozote toka kwetu na mbaya zaidi gharama zimepanda na umeme ndio hakuna kabisa upo wa machale tuu unatusaidia kunyoosha nguo na kuonekana smart mtaani.

  3. Nauli za mabsi yaendayo mikoani nazo zinapanda, tutashindwa hata kwenda salimia wazee wetu mikoani. nao watashindwa kuja kutusalimu au hata kuja kwa ajili ya matibabu zaidi kwa magonjwa yaliyoshindikana huko. Fanya reference Tanzania Daima ya jana tarehe 23/02/2011.

  4. Gharama za maisha nazo zinapanda kwa kasi hebu chukulia bei ya sukari ilivyopanda mara dufu mwezi januari ilikuwa 1600/=Tshs leo huku ni 2500/= kwa kilo.

  5. Maji na bado historia kwa watanzania tuliowengi, maji tunayaona kwa masaa yasiozidi matau na ndg zetun kule vijijin maji yenye rangi nyeupe (Water is Colorless) hawajawahi kuyaona wengine mpaka wanakufa.

  Haya yote hakunja kiongozi wa serikalini au hata vyama vya siasa wanashutuka kwa mambo yanavyokwenda, watanzania tumenyamaza kana kwamba hakuna linalo tutafuna na kutuumiza ndio maana najiuliza tumelogwa?waoga?wajinga?au .....................?
   
 8. Sizinga

  Sizinga JF-Expert Member

  #8
  Feb 23, 2011
  Joined: Oct 30, 2007
  Messages: 7,922
  Likes Received: 454
  Trophy Points: 180
  be open,si kila mtuyupo bongo anaweza refer hiyo Tanzania Daima....hembu tuambie lina nini,then tuje kwenye mada
   
 9. Duduwasha

  Duduwasha JF-Expert Member

  #9
  Feb 23, 2011
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 5,139
  Likes Received: 2,175
  Trophy Points: 280
  Ngoja waarabu wamalize yao na sie tuanze kwetu ndio suruhisho la viongozi wasio na machungu kwa wananchi wao. ,afao matamu wanayopata ndio yanayotupa shida wananchi kwani zinawafanya waone nchi ipo safi
   
 10. Katavi

  Katavi Platinum Member

  #10
  Feb 23, 2011
  Joined: Aug 31, 2009
  Messages: 39,474
  Likes Received: 4,131
  Trophy Points: 280
  Huenda ni waoga na wajinga, lakini hilo la kurogwa sina uhakika nalo...
  Hata hivyo ipo siku tu watu uvumilivu utawashinda na uoga utatoweka na watafanya kile kinachotakiwa...
   
 11. FuturePresident

  FuturePresident JF-Expert Member

  #11
  Feb 23, 2011
  Joined: Nov 9, 2010
  Messages: 322
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Is just the matter of time....Time will tell......lets wait and see....if we are coward,stupid, silly, ignorance or......all will come out, not far away from here.... where we are now!!!!!!!!!!
   
 12. Najijua

  Najijua JF-Expert Member

  #12
  Feb 23, 2011
  Joined: Nov 5, 2010
  Messages: 1,029
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  When is that time?au tunasubiri mambo yafike hali mbaya ndio tuanze tia maji tia maji??yako wapi matumaini ya Mtanzania wa kipato cha chini?yako wapi maisha bora?yako wapi matumaini ya mhitimu wa shahada ya chuo kikuu?

  Hali inazidi kuwa ngumu wakati mkulima hana matumaini kila siku bei za mazao zinashuka, fedha ya nchi inashuka dhamni kila kukicha, bei za vyakula zinapanda kila siku na bado wafanyakazi mishahara ipo pale pale na watanzania wamenyamaza kana kwamba hakuna liwaumizalo.

  Kule zambia mkate uliwahi panda bei raia wakaingia mtaani serikali ikasikia kilio chao, sisi hatujawahi waeleza vilio vyetu viongozi nao wamekuwa viziwi na vipofu
  Aliyetuloga watanzania yu hai au amekufa??????????
   
 13. DOUGLAS SALLU

  DOUGLAS SALLU JF-Expert Member

  #13
  Feb 23, 2011
  Joined: Nov 13, 2009
  Messages: 11,603
  Likes Received: 4,709
  Trophy Points: 280
  Limbwata la CCM, wanapigika lakini bado wanishabikia CCM
   
 14. Anko Sam

  Anko Sam JF-Expert Member

  #14
  Feb 23, 2011
  Joined: Jun 30, 2010
  Messages: 3,216
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  TUNALOGWA KILA MWAKA NA MWENGE WA CCM. Mwenge wa Nyerere ulikuwa unachoma mabeberu, wahujumu uchumi, wanyonyaji, walanguzi nk nk, pia ulikuwa una hamasisha watu wawe wamoja kwa kujiletea maendeleo.

  Huu wa CCM ya sasa unalimwata la Bagamoyo, una walaza wananchi na kuuchoma moyo wa kizalendo na kila mtu anajiona kama mhamiaji vile, anaona hawajibiki kwa lolote zaidi ya kulipa kodi serikalini ya asilimia 50% kwa walio kwa wenye ajira rasmi.

  Kwa vile tumelogwa zigi zigi, utaona tuna toa maneno ya kukata tamaa;
  Mfano; 1: "...we waache tu, iko siku wananachi wata amka....! Yeye siyo mwananchi?
  2: Mwingine anaweka na ka kiingereza kidogo "..Is just the matter of time... Time will tell..lets wait and see..! Are you still waiting to see not to do?
  3:..ipo siku tu watu uvumilivu utawashinda na uoga utatoweka na watafanya kile kinachotakiwa...! Aaah!
  4: ...Waache tunawasubiri 2015...!

  Jamani, tujitambue kila mtu awajibike ipasavyo katika ukombozi wa nchi, sentensi za kichovu hivi tuachane nazo tubadirike.
   
 15. apolycaripto

  apolycaripto JF-Expert Member

  #15
  Feb 23, 2011
  Joined: Feb 11, 2011
  Messages: 637
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 45
  Watanzania watatuelewa iwapo tutajiweka wazi badala ya kuficha sura zetu huku tukiwaamasisha kunyanyuka na ku-fight.Hawawezi kutekeleza wito wetu sisi "invisible" wanadai tu waoga wa kwanza!
   
 16. Kasheshe

  Kasheshe JF-Expert Member

  #16
  Feb 23, 2011
  Joined: Jun 29, 2007
  Messages: 4,690
  Likes Received: 91
  Trophy Points: 145
  Anza na wewe:

  Weka jina lako na contact zako wazi alafu pigani watu wafanye yale unayotaka. Haiwezekani umejificha hivyo alafu unalaamu wengine.
   
 17. THINKINGBEING

  THINKINGBEING JF-Expert Member

  #17
  Feb 23, 2011
  Joined: Aug 9, 2010
  Messages: 2,726
  Likes Received: 854
  Trophy Points: 280
  Sisi ni waoga na wajinga tena tumelogwa.
   
 18. lm317

  lm317 JF-Expert Member

  #18
  Feb 23, 2011
  Joined: Nov 2, 2009
  Messages: 452
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Aa! Wapi labda muoga wewe
  Mimi nitaenda kujilipua subiri utaona!
   
 19. sijuikitu

  sijuikitu JF-Expert Member

  #19
  Feb 23, 2011
  Joined: Feb 8, 2011
  Messages: 286
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  sio wajinga, wala sio waoga na wala hawajalogwa.....ni WATANZANIA...full stop
   
 20. Indume Yene

  Indume Yene JF-Expert Member

  #20
  Feb 23, 2011
  Joined: Mar 17, 2008
  Messages: 2,932
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 145
  Hakuna mtu ambaye amezoea Umaskini bali tunaendekeza umaskini. Sidhani kama ni ujinga kuendekeza umaskini. Kujibu swali lako, watanzania si wajinga bali ni waoga katika kudai haki zao za msingi.
  Wakati sasa umefika watanzania tuachane na uoga tudai nchi yetu. Libya wanatandikwa na mabomu from the sky lakini bado wameshikamana kudai nchi yao. Naamini ndani ya masaa 48 hadi 72 ile nchi itakuwa imekombolewa, na Gaddafi atakuwa historia.
   
Loading...