Hivi sisi watanzania ni waoga, wajinga au tumelogwa?

Hodi wanajamvi, Hii ni post yangu ya kwanza na naomba niulize hivi,

Kwa nini watanzania tunapenda kutumia majina ya bandia?

Maana nimechunguza hata humu wengi wetu tunatumia majina ya bandia, Hivi tunamuogopa nani?
Yaani ume join December 2012 post yako ya kwanza March 2013 duh kazi ipo.........
 
hodi wanajamvi, hii ni post yangu ya kwanza na naomba niulize hivi,

kwa nini watanzania tunapenda kutumia majina ya bandia?

Maana nimechunguza hata humu wengi wetu tunatumia majina ya bandia, hivi tunamuogopa nani?
toa kwanza kibanzi wenye jicho lako ndipo ulitazame jicho la mwenzako!!!!!
Jiweke wewe verified sasa hivi .within 30 minitues na mimi nitasomeka verified user.
 
Hakuna anayeogopa bali ni namna tu ya kuwasiliana ambayo watu wengi humu wanaipendelea maana kuna baadhi wameweka majina yao.
Kwani ukijua jina la mtu inakusaidia nini?
 
Mi nadhani hii ni sahihi kabisa, JF mawazo/mchango wa mtu ndo una matter, na si jina, jinsia, dini, rangi wala...........
Ni fundisho pia kwa wale wanaoangaliaga nani kaseme halafu ndo kaseme kitu gani?
 
Hodi wanajamvi, Hii ni post yangu ya kwanza na naomba niulize hivi,

Kwa nini watanzania tunapenda kutumia majina ya bandia?

Maana nimechunguza hata humu wengi wetu tunatumia majina ya bandia, Hivi tunamuogopa nani?

Wenyewe na vile tunavyoweza fanya.
 
Tofautisha uoga na uhuru wa kutoa maoni. Hii iko dunia nzima sio Tanzania tu, kwenye forum kama hii ndo fursa ya kupingana kwa hoja hata na Baba yako bila nyie kujuana. Majadiliano huwa hayawi exciting kama watu mnajuana. Ndio maana hata hao wenye majina yao halisi wana ID hata kumi humu. Huwezi kujua labda mimi ndio baba yako mzazi...
 
wasiwasi nayo akili japo sio kila dakika
jina sahihi sio hoja sahihi
kificho cha jina eleza madhara yake
jina sahihi sio ishu, hoja kabambe twataka
 
Kwenye mitandao mingine wenaweka majina yao halisi ila hapa JF panachekesha hata ile dhana ya 'THE HOME OF GREAT THINKERS' haina maana, ni kama kijiwe fulani tuu. Wapo wengine wana account mbili humu humu moja jina halisi na nyingine 'AKA'.
 
wana jf 2po kama wapelekez ama usalama sasa tukijitambulisha tunaweza kosa jibu sahihi la kile kitu tunachohitaji,ki2 kingine ni uhuru wa kujieleza.!
 
sasa wewe ndugu unataka hata JK ashindwe kuchangia hoja? Kwa maana nae yumo humu kwa id bandia. Kwa mfano hoja za mapenzi angechangia vipi si ingekuwa kichekesho?
 
Jina halisi sio muhimu wengi tungeshindwa kuchangia baadhi ya post, huo wala sio woga.
 
ila ni kweli watanzania sisi ni waoga sana.
waliosoma wanajifanya maneno mengi vitendo vinavyohitaji ujasiri wanajifungia majumbani mwao na kuendelea kujadiliana mada ya waliyotakiwa kufanya kwa vitendo.
waofa kuanzia watoto wazazi viongozi wetu na wanajamii kwa ujumla.
kutokuwa mwoga ni utamaduni.sisi hatuna huo utamaduni labda ndio tuanze leo kuutengeneza.
 
Yaani ume join December 2012 post yako ya kwanza March 2013 duh kazi ipo.........

hapo nilipo-bold napo panaonyesha sifa yake ya uoga kama sie watanzania wenzake...atafakari kisha aje na majibu ya kwanini ajiunge kisha akae 3 months then atume post ya kwanza ya kinafiki...huu nao ni uoga in its true colors
 
Hujakatazwa kutumia jina lako halisi ukitaka uweke na picha.. Kwa raha zako.

Chagua unachoona kinakufaa!

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
 
Back
Top Bottom