Hivi sisi watanzania ni binadamu original?

Hivi sisi watanzania ni binadamu original?

Wajerumani wa leo bado wanashangaa ilikuwakuwaje hadi babu na bibi zao kumtukuza na kumshangilia Hitler wakimuona kama mkombozi. Wengine wao wamebaki wakijiuliza kinachoweza kuwapata watu wenye akili timamu hadi kumhusudu binadamu mwenzao na kumuona kama mungu-mtu na kauli yake kuwa sheria.

Ingawa Historia inafundisha mengi na kutuonya juu ya hali kama hizo, wengi tumeshindwa kujifunza na kwa Watanzania wenzangu sishangai hata kidogo. Kwa miaka sitini tumeruhusu mambo yale yale, watu wale wale, mfumo ule ule...hakika hali hii inatisha, inaudhi na inakasirisha na mwisho wake hauwezi kuwa mzuri.

Leo hii polisi anayetakiwa kulinda usalama wa raia na mali yake, anaamka asubuhi, anavaa magwanda yake, anaingia mtaani na si kutimiza wajibu wake kikatiba ...la hasha, kumsaka au kumvizia raia, kumnyanyasa kwa kumbambikizia kosa na hatimaye kumpora kidogo alicho nacho ili asifiwe kwa kuiingizia serikali mapato, huku tukipiga makofi.

Kwamba Katiba inaweza kuwekwa kando kwa kisingizio cha kunyosha nchi na sisi tukapiga vigelegele ni dalili mbaya sana. Tunaumwa na bila kutambua kwamba tunahitaji matibabu ya haraka tunaelekea kubaya. Kwamba mwenzetu anaweza kukamatwa kwa kutoa maoni na sisi tukashangilia ni kwamba tumekufa kiakili ingawa tunatembea.
 
Sanaaaaa huu uzuzu na uoga wetu ndo umetufanya tusiendelee
Mbona kuna maendeleo makubwa tu ya kinyumenyume?. Tizama afya, elimu, jamii...labda Serikali hii itatusaidia. Sijui?. Labda Mh. Magufuli atasaidia?
 
Kwa yanayoendelea hapa nchini na jinsi umma wa watanzania unavyochukulia mambo haya, ,nina swali moja tu linalouliza kama ifuatavyo.

Hivi sisi watanzania ni binadamu "original" kama walivyo watu wa mataifa mengine au sisi ni binadamu "fake"?

Kabla hujasema nafanya utani,think twice first.
Kwa kweli wapo feki na orijino.. Mfano mashabiki wengi wa Chadema ni binadamu feki.. Haiwezekani na haitawezekana yaani Lowasa huyu alietukanwa sana na Chadema Leo awe mgombea wenu kupitia Chadema na Slaa akawe msaliti
 
Lowassa alikuwa ni mtaji mzuri wa kisiasa kwetu na angalia kura alizopata na jinsi tulivyokamata majiji.

Nyinyi mmekariri tu wala hampimi tulichovuna.Kweli mna akili fupi!
 
Si kwasababu wao wanafana na sisi, mkafikiri kuwa wao ni sawa sisi.Hapana.

Wao ni mfano wa sisi, ila sisi ndio halisi.

Sisi tuliwatawala. Tunawatawala. Tutawatala.

Tukienda kwao hutushangilia na kututhamini sana. Wao wakija kwetu, si kitu.
 
Lowassa alikuwa ni mtaji mzuri wa kisiasa kwetu na angalia kura alizopata na jinsi tulivyokamata majiji.

Nyinyi mmekariri tu wala hampimi tulichovuna.Kweli mna akili fupi!
Mmevuna majiji? Kwahiyo bila Lowasa msingeshinda majiji.. Umesahu Slaa alishinda majiji mangapi? SABABU Slaa alishafungua njia, mtu yoyote angesimama Chadema majiji lazima yangeongezeka tu kwa hesabu rahisi
 
Kwa yanayoendelea hapa nchini na jinsi umma wa watanzania unavyochukulia mambo haya, ,nina swali moja tu linalouliza kama ifuatavyo.

Hivi sisi watanzania ni binadamu "original" kama walivyo watu wa mataifa mengine au sisi ni binadamu "fake"?

Kabla hujasema nafanya utani,think twice first.

salary slip.....swali lako la msingi sana, kuamini au kutoamini ni mtazamo wa mtu mwenyewe, binafsi inanipa wakati mgumu kuamini.
 
Kwa nlvotazama malumbano ya hoja itv na mambo yanavokwenda hapa nchini nina hakika watz wengi waliumbwa cku ya 5 mpaka ya 6 wakati Mungu akiwa amechoka na anaelekea cku ya 7 kupumzika. Bdo wtz akili hazipo sawa. Kuna watu mpaka leo wanaamini utawala huu ni chaguo la Mungu.
 
Mimi nimefatilia kile kifo cha yule dada anaesemena amebakwa hadi kufa ni kwamba diamond platnumz ndie msanii bora kwa sasa tz hayo aliyasema ozil wakat anafunga goli dhidi ya hardware za kusambaza mchanga kwenye uchaguzi wa kumpata miss wa korosho husaidia kumfanya mtu aoge kwenye gari ambalo halina laptop zenye ukubwa wa chai ya maziwa yenye barabara za kwenda calculator maji makubwa ya kilimanjaro ndio huletja matairi ya kifaru cha mwinuko wa bahari kwenye ukuta wa maji*
 
Nilishawahi kuwaza hili sana nikapata jibu endapo tutauza Aridhi yote kwa wageni! 70% tukaishi kwenye nyumba za kupanga tutapata akili maana kuna watu wa kanda nyingine wakishapata ugali na maharage tu huwa wanasahau matatizo yao yote!!
 
Back
Top Bottom