Mbona umeuliza na kutoa jibu hapo hapo? Katika hii awamu hao ndio wanaotakiwa...waliofyatuka! Hivyo ndivyo alivyowahi kutamka "BWANA YULE" kwamba ni kichaa na sifa kubwa anayoitaka anapoteua ni hiyo, wawe vichaa kama yeye. Sasa ikitokea kwamba alifanya makosa alipokuteuwa kwani hukuwa kichaa lazima sasa uoneshe kuwa na wewe umo.
Ukilegealegea na kuanza kutumia busara badala ya ukichaa, lazima utumbuliwe. Watu kama Nape walishindwa kutambua hili mapema hivyo walijaribu kutenda majukumu yao wakitanguliza hekima na kilichowapata hawatakisahau. Alionesha ukichaa ulivyo hadharinj kwa kutolewa bastola na toka siku hiyo anajua hatari ya kichaa kupewa rungu.
RC Agrey Mwanri huenda akawa kipenzi cha bosi wake labda hata zaidi ya waliomtangulia kwani ni katika wale wanaojua namna ya kuji-adapt katika mazingira chini ya huu utawala. Asiachie hapo, aongeze juhudi hadi hata familia yake ione tofauti na kwamba baba kabadilika. Hongera Mwanri! Milango karibu itafunguka kwani katika awamu hii ukichaa unalipa.