Hivi Rais Magufuli anayafahamu haya?

Hivi Rais Magufuli anayafahamu haya?

K
Sikiliza ndugu yangu.
Rais Magufuri si chochote si lolote, uwezo wake wa kutatua kero za wananchi unaishia kwenye upeo wa mache wake.

Kitu chochote kilicho mbali na upeo huo, hana uwezo wa kukitatua.
Kweli ndio maana kuna mkuu wa wilaya katika kila wilaya anamuwakilisha rais
 
K

Kweli ndio maana kuna mkuu wa wilaya katika kila wilaya anamuwakilisha rais
Nachosema ni kwamba hana uwezo wa kufanya kazi na mfumo wa uongozi uliopo. Ni lazima awepo mahala yeye mwenyewe, wakati mwingine na mke wake, ndo unaona anatatua kero sasa.
 
Hujaeleza tatizo angalau cases kadhaa inayohusiana na unyanyasaji unaofanywa na hao watendaji wa kata; mfano tarehe.....mtendaji wa kata ya ....aliweka watu kadhaa ndani bila sababu ya msingi hadi wanatolewa kwa rushwa.....hali kadhalika mtendaji wa kata ya.....aliweka mtu/watu ndani ktk mazingira ya kubadilisha rushwa. Umeeleza jumlajumla sana.
Ila nimedokeza kuna Mama mume wake alipigwa ndani ya ofisi ya kata. Alikuwa mtuhumiwa na sasa ameambiwa na katibu wa mkuu wa mkoa amuone mkuu wa wilaya ili hatua stahiki zifuatwe.Sio vizuri kuitaja hiyo kata
 
Nachosema ni kwamba hana uwezo wa kufanya kazi na mfumo wa uongozi uliopo. Ni lazima awepo mahala yeye mwenyewe, wakati mwingine na mke wake, ndo unaona anatatua kero sasa.
Aliowateua je? Wanakula mishahara bure?
 
Ila nimedokeza kuna Mama mume wake alipigwa ndani ya ofisi ya kata. Alikuwa mtuhumiwa na sasa ameambiwa na katibu wa mkuu wa mkoa amuone mkuu wa wilaya ili hatua stahiki zifuatwe.Sio vizuri kuitaja hiyo kata
HII haitoshi kutip chochote....hapa ni JF, huhitaji kutoa taarifa ya kufumbafumba. Be straight ili wahusika waweze kutrace tatizo...
 
Hivi unadhani kwa ulivyojieleza mtu atakuelewa??? Kuna watendaji kata na vijiji wanapiga kazi na hawanyanyasi watu bila sababu.

Nikuombe tu just be specific kuwa mtendaji wa kata ya ......bwana/bibi fulani ambaye alifanya makosa 1,2,3 nk na bila kumtaja kwa jina napo haitakusaidia maana huenda kahama.

Sent using Jamii Forums mobile app
Kuwa muelewa .kuna mtendaji wa kata fulani aliruhusu watuhumiwa wakapigwa na mmoja alifariki.upelelezi unaendelea na mke wa marehemu anatakiwa amuone mkuu wa wilaya.siwezi kuitaja.maana upelelezi unaendelea. Ila fanya tafiti zako ujionee haya nilionandika kama kweli au si kweli
 
HII haitoshi kutip chochote....hapa ni JF, huhitaji kutoa taarifa ya kufumbafumba. Be straight ili wahusika waweze kutrace tatizo...
Kwa msaada wa umma tu. Tar 26/10/2019 mtendaji wa kata ya kahama wilaya ya ilemela mkoani Mwanza aliruhusu watuhimiwa kupigwa na kuteswa na Migambo na Mwanajeshi . Mmoja alifariki na baada ya kuwapiga ilitakiwa watoe pesa mil 9 ya vitu vilivyodaiwa kuibiwa. Inasemekana baada ya hali kuwa ngumu waliwapeleka polisi kirumba na wengi waliachiwa kwa mazingira tatanishi.Kibaya zaidi ofisi ya mtendaji wa kata iligeuka kuwa kama mahakama. Na Mtendaji wa kata haruhusiwi kujihusisha na kesi za jinai. Anatakiwa akamate alafu apeleke polisi
 
Rais Magufuli ni Rais asiyependa kuona watu wanafanyiwa dhuluma na kunyanyaswa.

Mfano mzuri ni alipokuwa kahama alimuonea huruma toka moyoni kabisa mama ambae mume wake aligongwa gari na polisi traffic.

Ila kiuhalisia huku ngazi za chini wananchi bado wanadhulumiwa na kunyanyaswa sana. Hasa maeneo ya vijijini.

Watendaji wa kata wamejipa madaraka makubwa mno, wanawakamata watu wanawafungia katika lock up zao kinyume na Sheria.

Maana Mtendaji wa Kata haruhusiwi kisheria kusikiliza kesi za jinai, ila kama mlinzi wa amani anatakiwa akamate watuhumiwa kisha awapeleke polisi.

Lakini mambo ni tofauti. Wanakamata watu wanawapiga na kutengeneza mazingira ya kupewa rushwa.

Katika kila wilaya kuna Mkuu wa Wilaya na kamati yake ya ulinzi na usalama ya wilaya Je hawayaoni haya na kumpa taarifa Rais?

Maana kila kukicha ni matukio yanayofanana tu hasa maeneo ya vijijini.
Kwahiyo watendaji wa kata nchi nzima wanafanya hayo?
 
Kuwa muelewa .kuna mtendaji wa kata fulani aliruhusu watuhumiwa wakapigwa na mmoja alifariki.upelelezi unaendelea na mke wa marehemu anatakiwa amuone mkuu wa wilaya.siwezi kuitaja.maana upelelezi unaendelea. Ila fanya tafiti zako ujionee haya nilionandika kama kweli au si kweli
Si umesha sema upelelezi unaendelea we unawashwa nini? Au unania ya kuharibu upelelezi?
 
Sikiliza ndugu yangu.
Rais Magufuri si chochote si lolote, uwezo wake wa kutatua kero za wananchi unaishia kwenye upeo wa mache wake.

Kitu chochote kilicho mbali na upeo huo, hana uwezo wa kukitatua.

Yap na sababu awamu yake haifanyi kazi kwa mifumo bali one man show.
 
Back
Top Bottom