Hivi Rais Magufuli anayafahamu haya?

Chagu wa Malunde

JF-Expert Member
Jul 11, 2015
8,708
5,711
Rais Magufuli ni Rais asiyependa kuona watu wanafanyiwa dhuluma na kunyanyaswa.

Mfano mzuri ni alipokuwa kahama alimuonea huruma toka moyoni kabisa mama ambae mume wake aligongwa gari na polisi traffic.

Ila kiuhalisia huku ngazi za chini wananchi bado wanadhulumiwa na kunyanyaswa sana. Hasa maeneo ya vijijini.

Watendaji wa kata wamejipa madaraka makubwa mno, wanawakamata watu wanawafungia katika lock up zao kinyume na Sheria.

Maana Mtendaji wa Kata haruhusiwi kisheria kusikiliza kesi za jinai, ila kama mlinzi wa amani anatakiwa akamate watuhumiwa kisha awapeleke polisi.

Lakini mambo ni tofauti. Wanakamata watu wanawapiga na kutengeneza mazingira ya kupewa rushwa.

Katika kila wilaya kuna Mkuu wa Wilaya na kamati yake ya ulinzi na usalama ya wilaya Je hawayaoni haya na kumpa taarifa Rais?

Maana kila kukicha ni matukio yanayofanana tu hasa maeneo ya vijijini.
 
Yakitokea matukio ya hivyo yakifika kwenye Kamati ya Ulinzi na Usalama yanashughulikiwa na haki inatendeka. Ila hawawezi kutoa taarifa kwa Bw Rais kama wameshatatua tatizo.

macson
 
Yakitokea matukio ya hivyo yakifika kwenye Kamati ya Ulinzi na Usalama yanashughulikiwa na haki inatendeka. Ila hawawezi kutoa taarifa kwa Bw Rais kama wameshatatua tatizo. Lakini kuna baraza la usalama la Taifa rais ni Mwenyekiti nafikiri masuala kama haya yanapaswa kuripotiwa kama walishughulikia au vipi?

macson
Ngoja tuone. Kuna mtendaji alikamata watuhumiwa mbaya zaidi waliwapiga mmoja akafariki.Mke wa marehemu ameambiwa amuone mkuu wa wilaya .Ngoja tuone kama haki itatendeka
 
Lock up ya mtendaji kata is unlawful custody hairuhusu kumlaza mtu kama inabidi wanatakiwa wampeleke Polisi.Siku akiwafia mtuhumiwa watajua cha kujibu.

Sent using Jamii Forums mobile app
Awamu hii Wala

Mbona Kuna Mama mwenye kichanga alikamatwa kwa kosa la mumewe na kupelekwa lockup ya polisi mtoto usiku baridi ndugu wamekuja kumchukua mtoto polisi wamegoma, basi wakaomba apewe blangeti nalo wakakataa mwishowe kichanga baridi kikakiingia kikafa polisi. Asbh Mama anawaonyesha mtoto keshajifia zamani

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ulisemalo kwa kweli kama limetokea basi awamu hii inaipanda sheria
Awamu hii Wala

Mbona Kuna Mama mwenye kichanga alikamatwa kwa kosa la mumewe na kupelekwa lockup ya polisi mtoto usiku baridi ndugu wamekuja kumchukua mtoto polisi wamegoma, basi wakaomba apewe blangeti nalo wakakataa mwishowe kichanga baridi kikakiingia kikafa polisi. Asbh Mama anawaonyesha mtoto keshajifia zamani

Sent using Jamii Forums mobile app

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sikiliza ndugu yangu.
Rais Magufuri si chochote si lolote, uwezo wake wa kutatua kero za wananchi unaishia kwenye upeo wa mache wake.

Kitu chochote kilicho mbali na upeo huo, hana uwezo wa kukitatua.
 
Nenda kwenye mamlaka husika kabla ya kukimbilia kwa Mkuu wa Wilaya
 
Awamu hii Wala

Mbona Kuna Mama mwenye kichanga alikamatwa kwa kosa la mumewe na kupelekwa lockup ya polisi mtoto usiku baridi ndugu wamekuja kumchukua mtoto polisi wamegoma, basi wakaomba apewe blangeti nalo wakakataa mwishowe kichanga baridi kikakiingia kikafa polisi. Asbh Mama anawaonyesha mtoto keshajifia zamani

Sent using Jamii Forums mobile app
Mbaya sana
 
How? Au niripoti kivipi?
Hujaeleza tatizo angalau cases kadhaa inayohusiana na unyanyasaji unaofanywa na hao watendaji wa kata; mfano tarehe.....mtendaji wa kata ya ....aliweka watu kadhaa ndani bila sababu ya msingi hadi wanatolewa kwa rushwa.....hali kadhalika mtendaji wa kata ya.....aliweka mtu/watu ndani ktk mazingira ya kubadilisha rushwa. Umeeleza jumlajumla sana.
 
Nahofia uhai wangu.ila ni mambo ambayo yapo wazi sana
 
Hivi unadhani kwa ulivyojieleza mtu atakuelewa??? Kuna watendaji kata na vijiji wanapiga kazi na hawanyanyasi watu bila sababu.

Nikuombe tu just be specific kuwa mtendaji wa kata ya ......bwana/bibi fulani ambaye alifanya makosa 1,2,3 nk na bila kumtaja kwa jina napo haitakusaidia maana huenda kahama.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom