Hivi R, L na H, ni Ugonjwa wa Taifa?

Brain-app

JF-Expert Member
Joined
Jul 22, 2018
Messages
1,773
Points
2,000

Brain-app

JF-Expert Member
Joined Jul 22, 2018
1,773 2,000
Mjerumani kushindwa kutamka vizuri maneno ya kiswahili ni jambo linaloeleweka lakini Mswahili kushindwa kutamka vizuri maneno ya lugha yake ya kiswahili ni kihoja.
Lazima tufike sehemu sasa tukubaliane na hali, kanda ya ziwa, mbeya kote, kanda ya kati na sehemu mbalimbali hizi herufi zimeshaashindikana. Tukubali tu kama vile mjerumani hawezi kusema roho anasema hoho au mtu wa india kusema wewe hawezi hata umshikie bunduki atasema veve. Au kama kiingereza cha kimarekani kilivyo tofauti kimatamshi na kiingereza cha uingereza. Kuna sehemu mpaka bbadhi ya majina yameathirika KAROLI...KALOLI,nk
 

JokaKuu

Platinum Member
Joined
Jul 31, 2006
Messages
17,014
Points
2,000

JokaKuu

Platinum Member
Joined Jul 31, 2006
17,014 2,000
Kwa kawaida, ningeweza kusema kwamba kiwango cha elimu aliyopata mtu kama huyu inawezekana kuwa elimu ya msingi.
Lakini kama mtu wa aina hiyo ni mtu aliyemaliza kidato cha nne au sita, hicho kitakuwa ni kielelezo tosha cha ubovu wa elimu yetu.
..matatizo hayo yalitakiwa yashughulikiwe wakati watoto wako shule za msingi wanapoanza kujifunza kusoma na kuandika.

..wakati mwingine tuna tatizo la kutoku-aim for perfection. Mtoto akijua kuandika hata kama kwenye "r" anaandika "l" waalimu hawachukui muda kumrekebisha.

..matokeo ya utamaduni wa kulipua-lipua kazi ndiyo haya tunayoyashuhudia sasa kwamba tuna taifa la watu wasiojua kuzungumza na kuandika kwa ufasaha lugha yao ya taifa.
 

Kalamu1

JF-Expert Member
Joined
Jul 7, 2018
Messages
4,057
Points
2,000

Kalamu1

JF-Expert Member
Joined Jul 7, 2018
4,057 2,000
..matatizo hayo yalitakiwa yashughulikiwe wakati watoto wako shule za msingi wanapoanza kujifunza kusoma na kuandika.

..wakati mwingine tuna tatizo la kutoku-aim for perfection. Mtoto akijua kuandika hata kama kwenye "r" anaandika "l" waalimu hawachukui muda kumrekebisha.

..matokeo ya utamaduni wa kulipua-lipua kazi ndiyo haya tunayoyashuhudia sasa kwamba tuna taifa la watu wasiojua kuzungumza na kuandika kwa ufasaha lugha yao ya taifa.
Ninakubaliana nawe moja kwa moja.
Haya uliyosema hapa ndiyo wanayofanya wenzetu ambao mifumo yao ya elimu ilishafanyiwa marekebisho.
 

Executor

JF-Expert Member
Joined
Sep 29, 2014
Messages
726
Points
1,000

Executor

JF-Expert Member
Joined Sep 29, 2014
726 1,000
Kikubwa tunaelewana tu.....
Mfano: unamnyatia binti fulani, katika mchakato wako wa kumshawishi kwa njia ya meseji akawa anakosea kosea katika uandishi namna hiyo utamrekebisha...?
 

JokaKuu

Platinum Member
Joined
Jul 31, 2006
Messages
17,014
Points
2,000

JokaKuu

Platinum Member
Joined Jul 31, 2006
17,014 2,000
Mkuu tafadhali, mimi sio mshabiki wa Magufuli, lakini haimaanishi nitamponda kwenye tatizo la kibinadamu. Magufuli anakijua kiswahili vizuri hata kama sio kwa kiwango cha kupata A+, lakini anakijua. Isipokuwa anapata tatizo ya kutamka herufi fulani fulani, kutokana na herufi hizo kutokuwepo kwenye lugha aliyozungumza hasa wakati wa utotoni. Hilo ni tatizo ambalo hata awe rais wa dunia hakuna atakayemshangaa kutokuweza kuzitamka. Ingekuwa wakati wa kuandika pia anafanya kosa hilo ungekuwa na hoja lakini sio kwenye kutamka boss.
..kwa maoni yangu Jpm amebeba ajenda ambayo hakupaswa kuibeba.

..ajenda ya kukisambaza Kiswahili ilitakiwa ibebwe na Raisi ambaye anazungumza Kiswahili kilichonyooka.

..Na kwa attitude zetu hapa Tz, za kuendekeza uzembe-uzembe, tunaweza kufika mahali wenzetu huko nje wakawa wanatubeza kuwa tunazungumza Kiswahili kibovu.
 

Kiranga

JF-Expert Member
Joined
Jan 29, 2009
Messages
48,078
Points
2,000

Kiranga

JF-Expert Member
Joined Jan 29, 2009
48,078 2,000
Kiranga kimsingi naona hapa ni kama unasaka kuibuka mshindi kwenye hili jambo. Nina maeneo mengi naweza kusaka ushindi ila sio kwenye hili. Naomba nikubali unalosema kwani sioni mtu anajifunza vipi kutamka herufi inayokataa kwenye ulimi wake. Sio kwake tu bali ni kwa walio wengi sioni wakitoboa kwenye hilo.
Mbona watu tunajifunza Kifaransa na Kihispania lugha ambazo si tu si za mama zetu, bali pia hata hazizungumzwi kwetu tulikozaliwa, na tunajitahidi kupata matamshi yanayokubalika.

Inakuwaje rais wa nchi kakaa bungeni miaka 20 kabla ya urais, kafika chuo kikuu, kapata uwaziri, mpaka leo matamshi ya lugha ya taifa yanamtatiza?

Huo ni ujinga au uvivu?

Nyerere mbona naye kazaliwa bara huko lakini hakuwahi kuchanganya L na R katika Kiswahili wala kufanya makosa ya kusikika sana katika kusema Kiswahili?

Mbona John Shibuda kazaliwa huko huko kwa kina Magufuli lakini Kiswahili anaongea vizuri tu?

Msisingizie lugha ya Mama kwa uzembe wa mtu bunafsi.
 

tindo

JF-Expert Member
Joined
Sep 28, 2011
Messages
24,940
Points
2,000

tindo

JF-Expert Member
Joined Sep 28, 2011
24,940 2,000
..kwa maoni yangu Jpm amebeba ajenda ambayo hakupaswa kuibeba.

..ajenda ya kukisambaza Kiswahili ilitakiwa ibebwe na Raisi ambaye anazungumza Kiswahili kilichonyooka.

..Na kwa attitude zetu hapa Tz, za kuendekeza uzembe-uzembe, tunaweza kufika mahali wenzetu huko nje wakawa wanatubeza kuwa tunazungumza Kiswahili kibovu.
Mkuu jokakuu hebu tuwe wakweli, hivi tatizo la Magufuli ni kukijua kiswahili au kupata tatizo la kutamka baadhi ya herufi kwa usahihi kutokana na lugha yake mama? Sina sababu ya kukataa jambo ambalo najua fika anafahamu kiswahili japo sio kwa kiwango cha rais mstaafu A.H.Mwinyi.

Hii ajenda ya kukibeba kiswahili kimataifa nadhani sababu hasa ni ajenda yenye kubeba udhaifu wake binafsi kwenye lugha ya kiingereza. Sioni kama ni ajenda inayoweza kubebwa na rais ajaye iwapo atakuwa anakimudu vyema kiingereza. Na hili inachangiwa kwamba vipao mbele vyetu vingi vinafuata utashi wa rais aliye madarakani, kuliko vipaombele vilivyo kwenye mipango ya Taifa.
 

Forum statistics

Threads 1,365,419
Members 521,216
Posts 33,345,781
Top