Hivi R, L na H, ni Ugonjwa wa Taifa?

Opuk Jater

Senior Member
Joined
Dec 25, 2018
Messages
101
Points
225

Opuk Jater

Senior Member
Joined Dec 25, 2018
101 225
Habari Wanandugu,

Katika kitu ambacho huwa kinanishangaza katika nyakati hizi ni maandishi na matamshi ya baadhi ya herufi na silabi. Huwa najiuliza kuwa Watanzania tunakwama wapi kwenye herufi "R" na "L" kuanzia kuyaandika mpaka kutamka?

Miaka ya nyuma kulikuwa na kichaka cha kujificha kuwa kuna Makabila ambayo hayana herufi "R" kwenye lugha zao za nyumbani, hasa mikoa ya kusini (Lindi & Mtwara).

Lakini siku hizi siyo kushindwa kutamka bali yanabadilishwa kabisa. Utakuta mtu na elimu yake anakuandikia "RAKINI" badala ya "LAKINI", Eti " KALILI" badala "KARIRI", kuna muda unamsikiliza mtu mpaka unashindwa kumwelewa kama anaongea kiswahili au anatumia lugha nyingine.

Tena kuna hawa Wachungaji na Manabii ukiwaskia wakiongea ndiyo wanazikazia " L" badala ya "R". Halafu hapo bado haujahamia kwenye vyombo vya habari.

Sasa cha ajabu siwani wakiwa wanabadili matumizi ya R na L wakiwa wanazungumza Kiingereza. Kwa hiyo huu ugonjwa ni ulimbukeni uliotujaa au ni wa makusudi?


MAONI KUTOKA KWA WADAU

Hizo ni athari za lugha ya nyumbani na sio rahisi kubadilisha kama unavyofikiri.Lugha yoyote inayokuja kwako kama lugha ya pili lazima itaathiriwa na lugha ya kwanza.Nailo ni swala la ulimi sio akili.Hata wazungu kwenye nchi wanazozungumza kingereza wanatofautiana lafudhi kati ya nchi na nchi wakati lugha ni ile ile.kwaiyo hiyo ni kawaida sana kwenye jamii yetu na kamwe hatuwezi kufanana ulimi.
 

jaji mfawidhi

JF-Expert Member
Joined
Feb 20, 2016
Messages
6,536
Points
2,000

jaji mfawidhi

JF-Expert Member
Joined Feb 20, 2016
6,536 2,000
Kiongozi fulani wa nchi ya SADC huwa anachapia hayo maneno yani mpaka unajiskia kutapika, alafu wasanii nao wanachapia balaa, TATIZO KUBEBWA SHULE kunachangia sana
 

Mr Q

JF-Expert Member
Joined
Aug 16, 2012
Messages
8,442
Points
2,000

Mr Q

JF-Expert Member
Joined Aug 16, 2012
8,442 2,000
Naomba usinijumuishe kwenye huo upumnavu wa watu wachache ambao lugha mama zimeathiri matamshi yao kwenye lugha hii ya kiswahili.
 

jiwe angavu

JF-Expert Member
Joined
Aug 28, 2015
Messages
1,939
Points
2,000

jiwe angavu

JF-Expert Member
Joined Aug 28, 2015
1,939 2,000
Ndio matokeo ya kupuuza maslahi ya walimu na kulegeza vigezo vya watu kujiunga na ualimu. Maana wengi walikua ni mafelia.

Unategemea nini sasa?
 

gigabyte

JF-Expert Member
Joined
May 27, 2015
Messages
1,098
Points
2,000

gigabyte

JF-Expert Member
Joined May 27, 2015
1,098 2,000
Hizo ni athari za lugha ya nyumbani na sio rahisi kubadilisha kama unavyofikiri.Lugha yoyote inayokuja kwako kama lugha ya pili lazima itaathiriwa na lugha ya kwanza.Nailo ni swala la ulimi sio akili.Hata wazungu kwenye nchi wanazozungumza kingereza wanatofautiana lafudhi kati ya nchi na nchi wakati lugha ni ile ile.kwaiyo hiyo ni kawaida sana kwenye jamii yetu na kamwe hatuwezi kufanana ulimi.
 

racso kaunda

Member
Joined
Aug 16, 2019
Messages
52
Points
125

racso kaunda

Member
Joined Aug 16, 2019
52 125
Naamini wana JF wote mpo sawa. JF imepata bahati kuwa na waandishi au wadadavuaji wazuri sana.

Lakini wapo ambao wanasumbuliwa na Maneno 'R' na 'L'. Baadhi hawajui R watumie wapi na L waweke wapi. Kuna mwana JF kaandika Lais Magufuli badala ya Rais Magufuli

Mwingine kaandika jambo lahisi badala ya jambo rahisi. Mwingine kaandika mahali 'namshukulu Mungu,' badala ya 'namshukuru Mungu'. Wapo pia wanaotatizwa na neno 'hawezi kufika' wakiandika 'awezi kufika'.

Nia yangu ya kuandika uzi huu ni kwamba, tusome vizuri uzi za wadadavuaji wa JF ambao tunawajua wako vizuri kwenye kiswahili maana Elimu haina mwisho.
 

Forum statistics

Threads 1,354,202
Members 518,466
Posts 33,086,702
Top