Uchaguzi 2020 Hivi pamoja na "promo" yote ya mabango yaliyotapakaa nchi nzima, ni kwanini CCM inapelekwa mchamchaka na Tundu Lissu?

Mystery

JF-Expert Member
Mar 8, 2012
15,484
30,159
Kuna msemo wa wahenga usemao kuwa kizuri chajiuza na kibaya chajitembeza......................

Kwa namna CCM ilivyosambaza mabango nchi nzima, wakati wapinzani wao wa kisiasa, vyama vya upinzani, wakiwa hoi bin taabani, naweza ulinganisha usemi huo na hali halisi ya hivi sasa.

Hivi unawezaje kulinganisha mapokezi makubwa mno anayoyapata Tundu Lissu, ukimlinganisha na John Magufuli, wakati akiwa hana bango hata moja nchi nzima?

Ni wazi kuwa watu wao wa "marketing" wanafanya kazi ya ziada katika kufanya hiyo "promo" kwa kumtangaza kwa nguvu zote huyo mgombea wao wa kiti cha Urais, John Pombe Magufuli na ya wagombea wengine wa CCM.

Nimekuwa pia nikijiuliza hivi nguvu yote wanayotumia CCM ni ya nini wakati walishautangazia ulimwengu, kuwa vyama vya upinzani vimeshajifia "natural death" kutokana na utendaji wa kutukuka wa Magufuli!

Nimejiuliza pia hivi ni serikali ya CCM hii hii ambayo imekuwa ikisema kwa miaka 5 mfululizo, ikiwagomea kabisa kabisa kuwaongezea mishahara ya wafanyakazi wa Umma kwa madai kuwa serikali haina fedha hizo za kuwaongezea mishahara watumishi hao, lakini wakati huo huo wananchi tukishuhudia chama tawala cha CCM kikitapanya mali ya Umma kwa kusambaza mabango kila mahali hadi kubandika mabango hayo kwenye miti na kwenye sehemu za "kujisaidia" watu uchochoroni?

Hivi wananchi wanajisikiaje kuhusu matumizi haya mabaya kabisa ya pesa, wakati hospitali zetu nyingi, wananchi wengi wanakufa, kwa kukosa dawa muhimu za panadol?

Hivi nyinyi maccm mnawezaje kufanya "promo" kwenye mikutano yenu ya CCM, kwa kuwalipa mamilioni ya pesa wasanii maarufu akina Diamond, wakati watoto wetu wanakalia matofali, kwa kukosa madawati mashuleni?

Imenenwa na wahenga kuwa kupanga ni kuchagua..............

Kwa hiyo kwa CCM kwao wamepanga, kipaumbele chao ni kufanya "promo ya kufa mtu" kwa mgombea wao Magufuli nchi nzima hadi yanakinaisha na kuleta kichefu chefu!
 
Ndugu yangu, madikteta duniani kote ndivyo walivyo. Hupenda kujiaminisha na kuuaminisha ulimwengu kuwa wanapendwa sana. Sasa hilo litimie, wateule (kv. ma RC, ma DC, maRPC, maOCD, ma NEC, nk) wao huwekwa roho juu kusimamia projekti hiyo ya 'kupendwa kwa dik'.

Kila RC, DC, OCD wanahangaika na kushindana kila mmoja kuonesha amesambaza mabango kila pembe ya wilaya au mkoa wake, na vivyo hivyo amejaza nyomi mikutano ya kampeni ya dik. Ni mashindano ya kutetea tumbo ili dik aridhike.

Ni kweli hizo pesa zingeweza kuelekezwa kuboresha huduma za kijamii. Sijui kama wanaelewa TAL akiwaambia maendeleo ya watu!
 
Ndugu yangu, madikteta duniani kote ndivyo walivyo. Hupenda kujiaminisha na kuuaminisha ulimwengu kuwa wanapendwa sana. Sasa hilo litimie, wateule (kv. ma RC, ma DC, maRPC, maOCD, ma NEC, nk) wao huwekwa roho juu kusimamia projekti hiyo ya 'kupendwa kwa dik'. Kila RC, DC, OCD wanahangaika na kushindana kila mmoja kuonesha amesambaza mabango kila pembe ya wilaya au mkoa wake, na vivyo hivyo amejaza nyomi mikutano ya kampeni ya dik. Ni mashindano ya kutetea tumbo ili dik aridhike. Ni kweli hizo pesa zingeweza kuelekezwa kuboresha huduma za kijamii. Sijui kama wanaelewa TAL akiwaambia maendeleo ya watu!
Mabango ni mengi kuliko wapiga kura😅😅
 
Hii imekaa hivi: unamkuta mwanafunzi wa kiwango cha A+ ambaye average score yake ni 98% anasoma saana, kila wakati yupo library na kulala masaa machache - wakati huohuo unamkuta yule boya wa kiwango cha 2% maneno mengi tu, porojo, kutwa kumsema yule wa 98%. Kunsingizia vitu vibaya mpaka hata uchawi!

Hili ndio jibu la swali lako.
CCM kuleta maendeleo na uongozi uliotukuka wanafanya kwa kiwango cha 98%, kupiga kampeni 98%, kutumia wasanii kusherekea utekelezaji wa ilani yao ya miaka 5 iliyopita ni 98% na kutangaza ilani ya CCM 20-25 pia kuombea washiriki kura wanaifanya 98%!

Sasa Lissu ni gredi ya 2% - hivyo hakuna mabango, hakuna kutangaza sera zozote, kuporomosha uongo na matusi, na hasa hasa hakuna cha kupoteza! Ni 2%.

Kuhusu umati wa watu anao ukusanya, hiyo ni sawasawa na tanker la petrol likianguka umati linaokusanya na madhara yake - waulize Morogoro mwaka juzi.
 
CCM akili hawana yaani iwapo wangeamua badala ya kuchapisha mabango ya Magufuli wangenunua madawati sina shaka tatizo la watoto kukaa chini lingeisha Kwa Nchi mzima....

Walidhani MTU anashinda kiti cha Urais Kwa wingi wa mabango?

Slogan yetu watanzania ni hii:
" .......kufuli tunavunja, pombe tuna mwaga na Ikulu tunaingia, tumeamua Kwa ridhaa yetu wenyewe kumkataa shetani na kazi zake zote "
 
Hii imekaa hivi: unamkuta mwanafunzi wa kiwango cha A+ ambaye average score yake ni 98% anasoma saana, kila wakati yupo library na kulala masaa machache - wakati huohuo unamkuta yule boya wa kiwango cha 2% maneno mengi tu, porojo, kutwa kumsema yule wa 98%. Kunsingizia vitu vibaya mpaka hata uchawi!
Hili ndio jibu la swali lako.
CCM kuleta maendeleo na uongozi uliotukuka wanafanya kwa kiwango cha 98%, kupiga kampeni 98%, kutumia wasanii kusherekea utekelezaji wa ilani yao ya miaka 5 iliyopita ni 98% na kutangaza ilani ya CCM 20-25 pia kuombea washiriki kura wanaifanya 98%!
Sasa Lissu ni gredi ya 2% - hivyo hakuna mabango, hakuna kutangaza sera zozote, kuporomosha uongo na matusi, na hasa hasa hakuna cha kupoteza! Ni 2%.
Kuhusu umati wa watu anao ukusanya, hiyo ni sawasawa na tanker la petrol likianguka umati linaokusanya na madhara yake - waulize Morogoro mwaka juzi.
Nimeamini kuwa Tundu Lissu ni sawasawa na Daudi wa kwenye Biblia.......

Wakati Daudi anamwendea Goliath, kupigana naye aliamini kuwa Mungu ndiye anampa nguvu, lakini watu wote walikuwa wakimcheka na hata Goliath mwenyewe akasema kileteni hicho "kitoto" nikile nyama...........

Lakini wote tunajua matokeo ya mpambano huo, ni kwa mbabe aliyeshindikana na ulimwengu mzima, Goliath kupigwa na manati na kufa na katoto kadogo Daudi!

Hakika October 28 itakwenda kuandika historia mpya ya nchi hii kwa Tundu Lissu kuweza kushinda uchaguzi mkuu, pamoja na chama cha CCM "kubebwa" na vyombo vyote vya dola nchini, vya Polisi, NEC na TISS!
 
Hii imekaa hivi: unamkuta mwanafunzi wa kiwango cha A+ ambaye average score yake ni 98% anasoma saana, kila wakati yupo library na kulala masaa machache - wakati huohuo unamkuta yule boya wa kiwango cha 2% maneno mengi tu, porojo, kutwa kumsema yule wa 98%. Kunsingizia vitu vibaya mpaka hata uchawi!
Hili ndio jibu la swali lako.
CCM kuleta maendeleo na uongozi uliotukuka wanafanya kwa kiwango cha 98%, kupiga kampeni 98%, kutumia wasanii kusherekea utekelezaji wa ilani yao ya miaka 5 iliyopita ni 98% na kutangaza ilani ya CCM 20-25 pia kuombea washiriki kura wanaifanya 98%!
Sasa Lissu ni gredi ya 2% - hivyo hakuna mabango, hakuna kutangaza sera zozote, kuporomosha uongo na matusi, na hasa hasa hakuna cha kupoteza! Ni 2%.
Kuhusu umati wa watu anao ukusanya, hiyo ni sawasawa na tanker la petrol likianguka umati linaokusanya na madhara yake - waulize Morogoro mwaka juzi.
Na wewe great thinker?
 
Ishu ipo hapa:Unajeruhi mioyo ya watu kwa takribani miaka mitano,kila mtu kwa namna yake halafu badala ya kujificha angalu upunguze makali, maajabu ni kwamba unaanika sura yako kwenye kila kichochoro hapo unategemea nini kama sio kutonesha vidonda kwenye mioyo ya watu?.Na hii ni siri mojawapo ya Lissu kuzidi 'kushine'

Sent from my VF-795 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom