Umesema point ya maana sana, haijalishi uko wapi, ushabiki ni mdudu mbaya, unakufanya sense za uzalendo zipotee.
Mimi namlaani Balozi Mula Mula, kwa kukosa direction na vision ya maana ya ubalozi wetu huko USA. Siku zote yuko kwenye blog za "kidaku" kama vijimambo, DMV DMV,DMV. Watanzania wametawanyika kila kona ya US, kufanya DMV kama ndio wawakilishi wa Wtz wanaoishi US ni uharamia. Kazi ya Balozi wa nchi ni kuiwakilisha nchi yake kwenye nchi za nje, lakini inaelekea Mula mula anawakilisha watz wa DMV kwa nchi yao ya Tanzania, lol.
Halafu JK hana kazi hadi akapoteza muda kuongea na Wtz wa DMV? Kila mwanasiasa akienda US anawatafuta hao washabiki wa CCM DMV, wanamuingiza na balozi huko, wanaanza kupiga siasa. Mwigulu alienda mwaka jana, JK Membe, the list is long. Kuna tija gani? Mkutano wa juzi, umeleta tija gani, nilidhani JK angetoa direction nini wabongo wa us wafanye ili issue ya uraia pacha iingizwe kwenye katiba ya sasa au inayotungwa, kawaacha njia panda, kuwa wajenge hoja? Is this thing bado ipo kwenye stage ya kujengewa hoja bado?, si hoja zilishajengwa na uongozi wake ukabariki, au nilikuwa simuelewi Membe alivyokuwa analiongelea hilo swala sometimes back akiwa London? Sasa kama bado lipo kwenye kujengewa hoja, si angetoa forum ya kujengea hiyo hoja? au anataka kutumia tawi la ccm dmv?
Swala lingine hili la uraia pacha, JK kawananga kiaina wana DMV, kuwa waache kupoteza muda kujadili nani kavaa nguo fupi kwenye mitandao ya kijamii bali,watumie muda wao wajenge hoja ya uraia pacha. Sasa mimi najiuliza, wajenge hojahoja gani? Labda kama alikuwa anamaanisha kulobby,kutoa rushwa etc. Mimi nilidhani nchi na uongozi wake una interest na uraia pacha, na ndio maana wanazungumzia sana DIASPORA, NHC, PPF, NSSF kutwa kucha wanapishana US kutafuta watanzania waje kuwekeza hapa nyumbani, sasa itakuwaje nchi ina interest na huo uwekezaji, lakini haina interest na uraia wa hao wawekezaji wenyewe?
JK kusema uraia pacha sio interest ya watanzania, including him anD Membe, ni kuwatosa wabongo wanaoishi nje na kukosa umakini kuhusu msimamo wake na watanzania waishio nje. Kwa maneno mengine, Diaspora/DICOTA haina maana kama uraia pacha hauna maana kwenye uongozi wa Muungwana. Yule desk officer pale foreign affairs anayeshughulika na Diaspora aondolewe tu.
Watanzania wanaoshi nje wanaleta fedha nyingi sana nyumbani hapa. Mimi namfahamu mama mmoja watoto wake wako nje, wanatuma fedha mara kwa mara na kujenga majumba. Hizo foreign currency inflows zinaboost uchumi wa JK, it is time JK kuwa na interest na hiyo issue in his heart, yeye na Membe, na waache kuwananga wabongo waishio nje kuwa wanapoteza muda mrefu kujadili mapaja badala ya kujadili uraia pacha-- wajadili nini zaidi, kila kitu kinajulikana, utashi tu wa JK na viongozi wenzake kulifanya jambo hilo lipite kwenye katiba!!! Kwa sababu, ukweli nchi inahitaji hawa watanzania wenzetu warudi kuja kumiliki ardhi na miradi ya kuzalisha uchumi. Wasiwaze sana na kuwa na woga kuwa hawa wenzetu watarudi hapa kuja kuchukua uongozi wa kisiasa, waondoe hilo ombwe na waangalie maslahi mapana ya taifa letu.