MALCOM LUMUMBA
JF-Expert Member
- Jul 26, 2012
- 20,897
- 63,784
Habari ndugu zangu,
Maswali yangu nitayafikisha kwa kuandikwa kwa kirefu kidogo.
Hivi ni nini huwa kinafanya nchi fulani kuwa na vyombo imara sana vya kijasusi?
Wanafanya kazi vema sana kuanzia kueneza ushawishi wa nchi yao nje ya mipaka,
Wanakusanya taarifa nyeti sana za kibiashara, kiteknolojia , kijeshi na hata kutunga sera bora kabisa za mambo ya nje na yale ya ndani. Mfano hai katika hili ni mashirika ya kijasusi ya nchi kama Marekani, China, Urusi, India, Ujerumani na Israeli.
Mfumo wa kiintelijensia ambao nchi nyingi hutumia ni ule ambao uko katika sehemu tatu:
Hatuwezi kulinganisha uwezo wa mashirika ya Kijasusi ya nchi ya India na yale ya Marekani au Uingereza. Mara ya kwanza niliamini sababu kubwa ni uchumi lakini kuna mataifa kama Israel, Iran, Cuba na Ethiopia (Hapa Afrika) wana vyombo imara sana vya kijasusi na mara nyingine hata kunyukana na mataifa yenye uchumi mkubwa hapa duniani. Mfano hai katika hili ni jinsi shirika la kijasusi la Israeli MOSSAD walivyoweza kuwashughulikia majasusi wa Kirusi na nchi za Kiarabu kipindi cha vita baridi. Au jinsi shirika la kijasusi la nchi ya CUBA (D.I, G-2 au DGI) lilivyoweza kushangaza dunia baada ya kushindana na mashirika ya kijasusi ya nchi kubwa na tajiri hapa duniani kama C.I.A la Marekani na M.I 6 la Uingereza.
Na kama ni mafunzo basi M.I 6 la Uingereza lingekuwa la kwanza,
Maana hakuna shirika lenye historia ndefu duniani kama hili katika nyanja nzima ya Ujasusi. Kwanza kabisa limeundwa mwaka 1909 ambayo ni miaka mingi kabla ya C.I.A, K.G.B wala MOSSAD. Na katika historia ya kuundwa kwa C.I.A majasusi wake wengi walipata mafunzo kutoka Uingereza na kwa Wajerumani walioenda Marekani mwaka 1945 baada ya vita ya pili ya dunia katika mpango maalumu uitwao OPERATION PAPERCLIP. Lakini baada ya vita baridi kuanza mashirika ya kijasusi ya Uingereza kuanzia M.I.5 na M.I.6 yalijikuta yapo uchi dhidi ya mashirika ya kijasusi ya Urusi ya Kisovyeti kama K.G.B na G.R.U. Je, ni nini kilifanya nchi yenye nguvu duniani kama Uingereza kuyaogopa sana Mashirika ya kijasusi ya nchi zinazohusiana na Urusi?
Mpaka kipindi hiki nashawishika kusema katika mashirika ya kijasusi yenye nguvu hapa duniani ni haya yafuatayo:
O.S.S, C.I.A, F.B.I, D.IA na mengineyo ya Marekani- Hapa sitazungumzia sana lakini ukweli upo wazi kabisa. Mashirika haya yamesaidia nchi ile kuwa na Uchumi mkubwa sana duniani, Ushawishi mkubwa kwenye utamaduni (HipHop, I phone, Basketball, Fasheni,Filamu na hata lugha), jeshi lenye nguvu sana na linaweza kufanya kazi popote duniani, Ushawishi wa mkubwa kiuchumi kuanzia kwenye taaisisi nyeti hapa duniani kama Umoja wa Mataifa, Umoja wa Ulaya na Benki ya Dunia. Pia raia wa Marekani katika utafiti wa kawaida ni watu wanaojihisi kuwepo salama ndani ya nchi yao kwasababau ya uwepo wa vyombo hivyo. Kubwa zaidi ni jinsi wanavyowashughulikia maadui zao nje na ndani ya mipaka ya Marekani.
F.S.B, S.V.R na G.R.U ya Urusi- Haya yameweza kuijenga Urusi ambayo ilikuwa imepengaranyika na isiyokuwa na matumaini kurudi kuwa taifa lenye nguvu sana kijeshi, kidiplomasia, kisayansi na mpaka sasa Urusi imeanza kupanua maslahi ya kiuchumi na kitamaduni.
MOSSAD, SHINBET na AMAN ya Israeli- Israeli ni jamii iliyozungukwa na maadui wengi ndani na nje ya mipaka yake tangu taifa hilo linaundwa mwaka 1948. Wamefanya makubwa sana japo wanasaidiwa sana na nchi kama Marekani na Uingereza kwa kiasi kikubwa. Lakini kama wasingekuwa na nguvu binafsi msaada wa Marekani ungeishia kuwa kama msaada wa Urusi kwa nchi za Kiarabu ambazo nyingi zimepangaranyika kama SYRIA, IRAQ na LIBYA. Kubwa ambalo wanafanya tofauti na nchi nyingine ni kucheza na saikolojia za viongozi wa kidini wa nchi nyingi hapa duniani. Mfano mpaka leo hii Wakristo wengi duniani hasa wale wenye ushawishi Marekani kama John Hagee wanahubiri kwamba kuivamia Israeli ni kupigana na mkono wa Mungu na kuleta laana. Unaweza kuwa hujui lakini hii yote ni kazi ya Intelijensia.
WIZARA YA ULINZI YA IRAN- Marekani na NATO wamewawinda hawa jamaa tokea mwaka 1979 na wakawawekea vikwazo vikali sana lakini mpaka leo hii majama wanadunda. Kila siku wanasayansi wakubwa wanaongezeka na wanauzima ushawishi wa Marekani na Israeli usiendelee kutanuka katika Ukanda wa Mashariki ya kati. Wanayatumia makundi kama Hezbollah na Hamas kuwashughulikia Israeli na mpaka sasa wamefanya kazi kubwa sana Urusi nchini Syria ili kulinda serikali ya Bashar Al Assad. Hata kama wanasaidiwa na Urusi na Uchina wao wenyewe wameweza kusimama kiasi cha kuwafanya mahasimu wao wakubwa Wamarekani wakae Mezani ili kusaini mikataba ya Kinyuklia ambayo mataifa mengi ya Magharibi yalipinga. Iraq, Libya, Syria na Afghanistani zimepangaranyuka lakini hawa majamaa bado ni wabishi sana. Adui yao mwingine ni Ufalme wa Saudi Arabia ambao una jeshi kubwa na utajiri mkubwa lakini bado wanawaogopa sana Iran. Vyombo vyao vya Usalama vina nguvu sana.
B.N.D la Ujerumani- Baada ya vita ya pili ya dunia nchi ilipangaranyuka na watu hawakuwapenda kabisa Wajerumani. Ikafika kipindi kwamba hata silaha za nzito wakawa wanaogopa kumiliki kwasababu dunia nzima ingesema Ujerumani anataka kuleta matatizo kama ya miaka ya nyuma. Uwezo wa B.N.D ulijikita kwenye kujenga nguvu za kiuchumi na kisiasa. Ujerumani ilifanya makubwa sana kwenye uchumi miaka ya 60, 70 na 80 ambapo hakuna aliyeweza kuamini. Wanauchumi wakubwa kama Helmut Schmidt na Willy Brandt ambao waliwahi kuwa mawaziri wakuu wa nchi hiyo wanahistoria kubwa ndani ya B.N.D Walisadia kuijengea Ujerumani ushawishi mkubwa barani Ulaya na ana sauti kubwa sana ndani ya muungano wa Ulaya mpaka hii leo. Miaka ya 70 Ufaransa alikuwa anafanya majaribio mengi sana ya silaha za Kiatomiki na Waziri moja aliwahi kusema "Sisi Wafaransa tunatengeneza mabomu ya Nyuklia lakini Ujerumani yeye ana "Deutsche Mark" ambayo ni hela ya Ujerumani na ina nguvu kuliko mabomu yetu kwasababu inatumika na sisi mabomu tunayaweka kwenya ghala" Minong'ono inasema mpaka sasa Wajerumani na B.N.D wanaamini kwamba Tanzania ni yao na wanaushawishi mkubwa sana kwenye siasa za nchi yetu (Hili bado halijathibitika)
Baada ya haya yote, maswali yangu ni haya yafuatayo:
Je, kuna siku ambapo na sisi nchi yetu ya Tanzania inaweza ikafika hapo wenzetu walipofika (Kuwa na ushawishi mkubwa kisiasa, kidiplomasi, kiutamaduni na kiuchumi) ?
Je, ni kitu gani haswa ambacho nchi hizi walifanya hadi kuweza kuyafanya mataifa yao yawe na vyombo imara vya kijasusi ;sisi tunaweza kuiga kwao hizo mbinu kuviendeleza vyombo vyetu na taifa kwa ujumla?
Je, tufanye nini ili T.I.S.S ,M.I ya JWTZ , Intelijensia ya Jeshi la Polisi na Kitengo cha Ujasusi wa Kiuchumi: Ziweze kurudi kwenye sifa yake iliyotukuka ambayo waliijengea nchi yetu kuanzia miaka ya 60 hadi 80 mwishoni, kuanzia kwenye Ulinzi wa raia, Mipaka ya nchi, rasili mali zetu na kuendeleza sayansi na teknolojia?
NB: NAOMBA TUJIBU KIZALENDO BILA KULETA MIHEMKO YA KIVYAMA, NA TUSITUMIE MATUSI WALA KEJELI.

- Shirika la Ujasusi wa nje,
- Shirika la Ujasusi wa ndani na,
- Shirika la ujasusi wa kijeshi.