Ndumbayeye
JF-Expert Member
- Jan 31, 2009
- 7,420
- 4,034
but kwanini una mashaka na ufanisi wa Tiss ? operations zao ni za siri wakati mwingine inakuwa shida hata kuupima. Huenda Tiss ndio namba 1, kwanini sio? wameshindwa wapi?
Need, desire, determination of the political establishment and the people, persistence and continued challenges are the best ingredients required to have a strong national intelligence body(ies) in a country. So, that mix must be available for Tz to measure up to the mentioned countries' intelligence.Habari ndugu zangu,
Maswali yangu nitayafikisha kwa kuandikwa kwa kirefu kidogo.
Hivi ni nini huwa kinafanya nchi fulani kuwa na vyombo imara sana vya kijasusi?
Wanafanya kazi vema sana kuanzia kueneza ushawishi wa nchi yao nje ya mipaka,
Wanakusanya taarifa nyeti sana za kibiashara, kiteknolojia , kijeshi na hata kutunga sera bora kabisa za mambo ya nje na yale ya ndani. Mfano hai katika hili ni mashirika ya kijasusi ya nchi kama Marekani, China, Urusi, India, Ujerumani na Israeli.
Mfumo wa kiintelijensia ambao nchi nyingi hutumia ni ule ambao uko katika sehemu tatu:
Lakini mpaka leo hii mataifa yanazidiana sana katika hii tasnia ya Ujasusi,
- Shirika la Ujasusi wa nje,
- Shirika la Ujasusi wa ndani na,
- Shirika la ujasusi wa kijeshi.
Hatuwezi kulinganisha uwezo wa mashirika ya Kijasusi ya nchi ya India na yale ya Marekani au Uingereza. Mara ya kwanza niliamini sababu kubwa ni uchumi lakini kuna mataifa kama Israel, Iran, Cuba na Ethiopia (Hapa Afrika) wana vyombo imara sana vya kijasusi na mara nyingine hata kunyukana na mataifa yenye uchumi mkubwa hapa duniani. Mfano hai katika hili ni jinsi shirika la kijasusi la Israeli MOSSAD walivyoweza kuwashughulikia majasusi wa Kirusi na nchi za Kiarabu kipindi cha vita baridi. Au jinsi shirika la kijasusi la nchi ya CUBA (D.I, G-2 au DGI) lilivyoweza kushangaza dunia baada ya kushindana na mashirika ya kijasusi ya nchi kubwa na tajiri hapa duniani kama C.I.A la Marekani na M.I 6 la Uingereza.
Na kama ni mafunzo basi M.I 6 la Uingereza lingekuwa la kwanza,
Maana hakuna shirika lenye historia ndefu duniani kama hili katika nyanja nzima ya Ujasusi. Kwanza kabisa limeundwa mwaka 1909 ambayo ni miaka mingi kabla ya C.I.A, K.G.B wala MOSSAD. Na katika historia ya kuundwa kwa C.I.A majasusi wake wengi walipata mafunzo kutoka Uingereza na kwa Wajerumani walioenda Marekani mwaka 1945 baada ya vita ya pili ya dunia katika mpango maalumu uitwao OPERATION PAPERCLIP. Lakini baada ya vita baridi kuanza mashirika ya kijasusi ya Uingereza kuanzia M.I.5 na M.I.6 yalijikuta yapo uchi dhidi ya mashirika ya kijasusi ya Urusi ya Kisovyeti kama K.G.B na G.R.U. Je, ni nini kilifanya nchi yenye nguvu duniani kama Uingereza kuyaogopa sana Mashirika ya kijasusi ya nchi zinazohusiana na Urusi?
Mpaka kipindi hiki nashawishika kusema katika mashirika ya kijasusi yenye nguvu hapa duniani ni haya yafuatayo:
O.S.S, C.I.A, F.B.I, D.IA na mengineyo ya Marekani- Hapa sitazungumzia sana lakini ukweli upo wazi kabisa. Mashirika haya yamesaidia nchi ile kuwa na Uchumi mkubwa sana duniani, Ushawishi mkubwa kwenye utamaduni (HipHop, I phone, Basketball, Fasheni,Filamu na hata lugha), jeshi lenye nguvu sana na linaweza kufanya kazi popote duniani, Ushawishi wa mkubwa kiuchumi kuanzia kwenye taaisisi nyeti hapa duniani kama Umoja wa Mataifa, Umoja wa Ulaya na Benki ya Dunia. Pia raia wa Marekani katika utafiti wa kawaida ni watu wanaojihisi kuwepo salama ndani ya nchi yao kwasababau ya uwepo wa vyombo hivyo. Kubwa zaidi ni jinsi wanavyowashughulikia maadui zao nje na ndani ya mipaka ya Marekani.
F.S.B, S.V.R na G.R.U ya Urusi- Haya yameweza kuijenga Urusi ambayo ilikuwa imepengaranyika na isiyokuwa na matumaini kurudi kuwa taifa lenye nguvu sana kijeshi, kidiplomasia, kisayansi na mpaka sasa Urusi imeanza kupanua maslahi ya kiuchumi na kitamaduni.
MOSSAD, SHINBET na AMAN ya Israeli- Israeli ni jamii iliyozungukwa na maadui wengi ndani na nje ya mipaka yake tangu taifa hilo linaundwa mwaka 1948. Wamefanya makubwa sana japo wanasaidiwa sana na nchi kama Marekani na Uingereza kwa kiasi kikubwa. Lakini kama wasingekuwa na nguvu binafsi msaada wa Marekani ungeishia kuwa kama msaada wa Urusi kwa nchi za Kiarabu ambazo nyingi zimepangaranyika kama SYRIA, IRAQ na LIBYA. Kubwa ambalo wanafanya tofauti na nchi nyingine ni kucheza na saikolojia za viongozi wa kidini wa nchi nyingi hapa duniani. Mfano mpaka leo hii Wakristo wengi duniani hasa wale wenye ushawishi Marekani kama John Hagee wanahubiri kwamba kuivamia Israeli ni kupigana na mkono wa Mungu na kuleta laana. Unaweza kuwa hujui lakini hii yote ni kazi ya Intelijensia.
WIZARA YA ULINZI YA IRAN- Marekani na NATO wamewawinda hawa jamaa tokea mwaka 1979 na wakawawekea vikwazo vikali sana lakini mpaka leo hii majama wanadunda. Kila siku wanasayansi wakubwa wanaongezeka na wanauzima ushawishi wa Marekani na Israeli usiendelee kutanuka katika Ukanda wa Mashariki ya kati. Wanayatumia makundi kama Hezbollah na Hamas kuwashughulikia Israeli na mpaka sasa wamefanya kazi kubwa sana Urusi nchini Syria ili kulinda serikali ya Bashar Al Assad. Hata kama wanasaidiwa na Urusi na Uchina wao wenyewe wameweza kusimama kiasi cha kuwafanya mahasimu wao wakubwa Wamarekani wakae Mezani ili kusaini mikataba ya Kinyuklia ambayo mataifa mengi ya Magharibi yalipinga. Iraq, Libya, Syria na Afghanistani zimepangaranyuka lakini hawa majamaa bado ni wabishi sana. Adui yao mwingine ni Ufalme wa Saudi Arabia ambao una jeshi kubwa na utajiri mkubwa lakini bado wanawaogopa sana Iran. Vyombo vyao vya Usalama vina nguvu sana.
B.N.D la Ujerumani- Baada ya vita ya pili ya dunia nchi ilipangaranyuka na watu hawakuwapenda kabisa Wajerumani. Ikafika kipindi kwamba hata silaha za nzito wakawa wanaogopa kumiliki kwasababu dunia nzima ingesema Ujerumani anataka kuleta matatizo kama ya miaka ya nyuma. Uwezo wa B.N.D ulijikita kwenye kujenga nguvu za kiuchumi na kisiasa. Ujerumani ilifanya makubwa sana kwenye uchumi miaka ya 60, 70 na 80 ambapo hakuna aliyeweza kuamini. Wanauchumi wakubwa kama Helmut Schmidt na Willy Brandt ambao waliwahi kuwa mawaziri wakuu wa nchi hiyo wanahistoria kubwa ndani ya B.N.D Walisadia kuijengea Ujerumani ushawishi mkubwa barani Ulaya na ana sauti kubwa sana ndani ya muungano wa Ulaya mpaka hii leo. Miaka ya 70 Ufaransa alikuwa anafanya majaribio mengi sana ya silaha za Kiatomiki na Waziri moja aliwahi kusema "Sisi Wafaransa tunatengeneza mabomu ya Nyuklia lakini Ujerumani yeye ana "Deutsche Mark" ambayo ni hela ya Ujerumani na ina nguvu kuliko mabomu yetu kwasababu inatumika na sisi mabomu tunayaweka kwenya ghala" Minong'ono inasema mpaka sasa Wajerumani na B.N.D wanaamini kwamba Tanzania ni yao na wanaushawishi mkubwa sana kwenye siasa za nchi yetu (Hili bado halijathibitika)
Baada ya haya yote, maswali yangu ni haya yafuatayo:
Je, kuna siku ambapo na sisi nchi yetu ya Tanzania inaweza ikafika hapo wenzetu walipofika (Kuwa na ushawishi mkubwa kisiasa, kidiplomasi, kiutamaduni na kiuchumi) ?
Je, ni kitu gani haswa ambacho nchi hizi walifanya hadi kuweza kuyafanya mataifa yao yawe na vyombo imara vya kijasusi ;sisi tunaweza kuiga kwao hizo mbinu kuviendeleza vyombo vyetu na taifa kwa ujumla?
Je, tufanye nini ili T.I.S.S ,M.I ya JWTZ , Intelijensia ya Jeshi la Polisi na Kitengo cha Ujasusi wa Kiuchumi: Ziweze kurudi kwenye sifa yake iliyotukuka ambayo waliijengea nchi yetu kuanzia miaka ya 60 hadi 80 mwishoni, kuanzia kwenye Ulinzi wa raia, Mipaka ya nchi, rasili mali zetu na kuendeleza sayansi na teknolojia?
NB: NAOMBA TUJIBU KIZALENDO BILA KULETA MIHEMKO YA KIVYAMA, NA TUSITUMIE MATUSI WALA KEJELI.
CC: MSEZA MKULU , Red Giant , mngony , Bukyanagandi , Infantry Soldier , de'levis , Yericko Nyerere , nankumene , Chief , kui , mshana jr , Kabaunyeri , The Emperor
but kwanini una mashaka na ufanisi wa Tiss ? operations zao ni za siri wakati mwingine inakuwa shida hata kuupima. Huenda Tiss ndio namba 1, kwanini sio? wameshindwa wapi?
Kwanza tuwe na uchumi imara ndio tutaweza kuboresha hayoHabari ndugu zangu,

Huo uchumi imara huwezi kuupata kama huna intelligence imara. Yani kazi muhimu za intelligence ni tatu ikiwemo ya hiyo kuhakikisha taifa tuvuka viunzi na kudukua mambo mbali mbali yahusuyo uchumi.Kwanza tuwe na uchumi imara ndio tutaweza kuboresha hayo
[emoji106] [emoji106] Yaap naona umesikia kilio changu kwa kubadilisha cover..
TISS wanafanya kazi za siri lakini matokeo ya kazi zao hayawezi kua siri hata siku moja,
Wahenga walisema penye moshi ndipo panapo moto, na mimi binafsi naamini hivyo.
Mambo mazuri hata yafanyikie gizani yataonekana tu kwa nje, na mabaye vile vile yatajulikana (La kuvunda halina Ubani). Haiihitaji kuwa na akili ya ISAAC NEWTON kujua kwamba taifa limefika pabaya leo hii.
Unapoona nchi ambayo ilikuwa TUMAINI LA WANYONGE inegeuzwa kuwa SHAMBA LA BIBI,
Hapo mtu yeyote mwenye uelewa mdogo kama mimi ni lazima ujiulize maswali kama yangu:
Kwa kweli mimi nimeangalia kwa mtazamo wa kiraia kabisa naona kwamba kuna Sehemu tumejikwaa,
- Kwanini huko nyuma RASILIMALI zetu zilikuwa haziporwi kiasi ambacho tunaona hii leo?
- Kwanini Tanzania yetu ambayo zaidi ya asilimi 70% ya wananchi wake ni wakulima (Nguvu kazi tosha kabisa), ina ardhi kubwa na yenye rutuba na soko zuri tu. Hakuna chochote cha maana kinachoendelea, Hivi hao wanajua hatari ya uhaba wa chakula inayotukabili huko mbeleni ?(COLLAPSE IN FOOD SECURITY). Lakini hatuoni
- Kwanini Elimu ambayo ni moja ya silaha ya kukomboa nchi yetu imeharibiwa kiasi hiki na wanasiasa huku chombo kama TISS kipo: Hivi unataka kuniambia hao TISS hawajui kwamba Taifa la watu wajinga ni rahisi sana kuingiliwa na Adui?
- Ushawishi wa Tanzania Kimataifa umenyauka kwa kiasi kikubwa na kibaya zaidi kipindi hiki tumevaa sera ya kujitenga (ISOLATION POLICY) na ile sera yatu ya mwanzo tumeitupia kapuni bila hata kuangalia madhara yake kwa kina. Kizazi cha akina Mzee Mahiga, Membe, Kikwete, Ahmed Salim, na Wengine hakina muda mrefu sana. Hivi hao TISS wanatuachia Tanzania gani sisi? Hii hii ya BAVICHA na UVCCM kweli? Hawatutendei haki hata kidogo.
Haiwezekani nchi yetu kila siku iwe ni ya kulalamika na hakuna kinachofanyika halafu useme kwamba vyombo vya Usalama vnafanya kazi kwa asilimia 100%
unachojibu ni tofauti na ulichoulizwa au mchango unaitajika yani ndugu wew unachanganya dagaa na maharagweee kwa pamojaKwa jinsi navyoona mashirika ya kijasusi yote uliyoyataja ndio yanayoongoza na kuamua siasa za nchi husika, kwa maana nyingine ndio wanawaongoza wanasiasa..
lakini hapa kwetu ni kinyume chake, siasa ndio zinazowaongoza, wanasiasa ndio wanaowaongoza.
Polisi anaambiwa na mwanasiasa kamata yule, bila hata kujiuliza anamkamata kwa ajili ya nini, anatekeleza.
Waache kutumiwa na wanasiasa (kutumika kisiasa) wafanye mambo kwa weledi.
ndugu nazani upo sahihi ila hii bajeti sio kubwa kivile mkuu,,, na hata tukiitaji bajeti iwe kubwa tuanze na mitambo ya kisasa kutokana na dunia imebadilika intelligencia inaitaji vyombo vya kisasa tena kwa wingi ili kubaini matukio mapema na kuona namna ya kuzuia, na pili kupeleka watumishi wake kusoma njee kwa wingi katika nyanja tofauti ususani katika mambo ya IT, Mambo ya economic hapo mkuu tutaweza sogea kwa hatua kubwaaMkuu wangu nimekuelewa sana,
Wazalendo hata Tanzania wapo, wewe mwenyewe ukiwa mojawapo.
Muhimu ni kwamba hakuna vyombo vinavyokuwa na bajeti kubwa sana katika nchi kama Ulinzi na Usalama,
Hili nimeliona kwa nchi tajiri na maskini. Ukisoma Brandt Report ya mwaka 1980 inasema Afrika haiendelei kwasababu sehemu kubwa ya bajeti zao inaenda kwenye Ulinzi na Usalama tofuati na shughuli za Kijamii kama afya na elimu.
Ile ripoti ni kithibiti tosha kwamba tunawekeza sana kwenye Usalama,
Tanzania ile ya Ujamaa yenye wasomi wachache na uchumi wa kuvuta kama mnati ilikuwa ina vyombo Imara sana,
Apson Mwang'onda aliyewahi kuwa mkurugenzi wa TISS alikiri kwamba uwezo wa TISS ya kuanzia 1997 hadi leo,
Ina utofauti mkubwa na ile ya akina Mzee Mzena, Kitine na Kombe hasa kwenye Weredi.
Swali langu kubwa ni kwamba kwa hali ilivyo sasa na kipindi kile,
Tanzania yetu ingekuwa imara sana kwenye mambo ya Ulinzi na Usalama,
Ukiangalia uchumi umekuwa mkubwa na wasomi wameongezeka sana,
Lakini bado kasi yetu hairidhishi, Je, tumekosea wapi ili tuige wenzetu wa nje?
mkuu umejibu vizur ila umekosea kusema ofisi zao zisiwe vificho ni bora ziwe vificho tuTISS inatakiwa iwe taasisi inayojitegemea kwa Kila kitu. Tofauti na sasa ambapo rais ndo boss wao na hutakiwa kutii matamko ya Boss wao bila kuzingatia yana athari zipi katika jamii.
Pili,sijajua kwa hapa kwetu Intelijensia ya Uchumi upo katika level gani. Intellijensia hii inakuja kuwa muhimu sana na yenye manufaa makubwa kwa miaka mingi ijayo. Kama tunataka kuwa taifa lenye ushawishi katika nyanja zingine za Kijamii lazima kwanza tuwe na Uchumi imara na hilo hutegemea na intelligensia yetu imefanya kazi kwa namna ipi.
TISS naamini wapo humu,mfikishieni Taarifa boss wenu afanye kazi kubwa sana katika kuinua na kuendeleza intelijensia ya mambo ya Uchumi. Ina manufaa mengi kipindi kijacho.
Pili,taasisi hii ya Ujasusi isiwe kitu cha kificho kama ilivyo sasa. Ofisi zao ziwe wazi na taratibu zao zijulikane.
Wasiwe wazuri tu kwenye kutoboa watu macho na kung'oa meno pamoja na kucha.