Hivi ni nini hufanya nchi kuwa na Intelijensia imara?


Malcom Lumumba

Malcom Lumumba

JF-Expert Member
Joined
Jul 26, 2012
Messages
13,296
Likes
36,347
Points
280
Malcom Lumumba

Malcom Lumumba

JF-Expert Member
Joined Jul 26, 2012
13,296 36,347 280
Habari ndugu zangu,
Maswali yangu nitayafikisha kwa kuandikwa kwa kirefu kidogo.
Hivi ni nini huwa kinafanya nchi fulani kuwa na vyombo imara sana vya kijasusi?
Wanafanya kazi vema sana kuanzia kueneza ushawishi wa nchi yao nje ya mipaka,
Wanakusanya taarifa nyeti sana za kibiashara, kiteknolojia , kijeshi na hata kutunga sera bora kabisa za mambo ya nje na yale ya ndani. Mfano hai katika hili ni mashirika ya kijasusi ya nchi kama Marekani, China, Urusi, India, Ujerumani na Israeli.


Mfumo wa kiintelijensia ambao nchi nyingi hutumia ni ule ambao uko katika sehemu tatu:
  1. Shirika la Ujasusi wa nje,
  2. Shirika la Ujasusi wa ndani na,
  3. Shirika la ujasusi wa kijeshi.
Lakini mpaka leo hii mataifa yanazidiana sana katika hii tasnia ya Ujasusi,
Hatuwezi kulinganisha uwezo wa mashirika ya Kijasusi ya nchi ya India na yale ya Marekani au Uingereza. Mara ya kwanza niliamini sababu kubwa ni uchumi lakini kuna mataifa kama Israel, Iran, Cuba na Ethiopia (Hapa Afrika) wana vyombo imara sana vya kijasusi na mara nyingine hata kunyukana na mataifa yenye uchumi mkubwa hapa duniani. Mfano hai katika hili ni jinsi shirika la kijasusi la Israeli MOSSAD walivyoweza kuwashughulikia majasusi wa Kirusi na nchi za Kiarabu kipindi cha vita baridi. Au jinsi shirika la kijasusi la nchi ya CUBA (D.I, G-2 au DGI) lilivyoweza kushangaza dunia baada ya kushindana na mashirika ya kijasusi ya nchi kubwa na tajiri hapa duniani kama C.I.A la Marekani na M.I 6 la Uingereza.

Na kama ni mafunzo basi M.I 6 la Uingereza lingekuwa la kwanza,
Maana hakuna shirika lenye historia ndefu duniani kama hili katika nyanja nzima ya Ujasusi. Kwanza kabisa limeundwa mwaka 1909 ambayo ni miaka mingi kabla ya C.I.A, K.G.B wala MOSSAD. Na katika historia ya kuundwa kwa C.I.A majasusi wake wengi walipata mafunzo kutoka Uingereza na kwa Wajerumani walioenda Marekani mwaka 1945 baada ya vita ya pili ya dunia katika mpango maalumu uitwao OPERATION PAPERCLIP. Lakini baada ya vita baridi kuanza mashirika ya kijasusi ya Uingereza kuanzia M.I.5 na M.I.6 yalijikuta yapo uchi dhidi ya mashirika ya kijasusi ya Urusi ya Kisovyeti kama K.G.B na G.R.U. Je, ni nini kilifanya nchi yenye nguvu duniani kama Uingereza kuyaogopa sana Mashirika ya kijasusi ya nchi zinazohusiana na Urusi?

Mpaka kipindi hiki nashawishika kusema katika mashirika ya kijasusi yenye nguvu hapa duniani ni haya yafuatayo:

O.S.S, C.I.A, F.B.I, D.IA na mengineyo ya Marekani- Hapa sitazungumzia sana lakini ukweli upo wazi kabisa. Mashirika haya yamesaidia nchi ile kuwa na Uchumi mkubwa sana duniani, Ushawishi mkubwa kwenye utamaduni (HipHop, I phone, Basketball, Fasheni,Filamu na hata lugha), jeshi lenye nguvu sana na linaweza kufanya kazi popote duniani, Ushawishi wa mkubwa kiuchumi kuanzia kwenye taaisisi nyeti hapa duniani kama Umoja wa Mataifa, Umoja wa Ulaya na Benki ya Dunia. Pia raia wa Marekani katika utafiti wa kawaida ni watu wanaojihisi kuwepo salama ndani ya nchi yao kwasababau ya uwepo wa vyombo hivyo. Kubwa zaidi ni jinsi wanavyowashughulikia maadui zao nje na ndani ya mipaka ya Marekani.

F.S.B, S.V.R na G.R.U ya Urusi- Haya yameweza kuijenga Urusi ambayo ilikuwa imepengaranyika na isiyokuwa na matumaini kurudi kuwa taifa lenye nguvu sana kijeshi, kidiplomasia, kisayansi na mpaka sasa Urusi imeanza kupanua maslahi ya kiuchumi na kitamaduni.

MOSSAD, SHINBET na AMAN ya Israeli- Israeli ni jamii iliyozungukwa na maadui wengi ndani na nje ya mipaka yake tangu taifa hilo linaundwa mwaka 1948. Wamefanya makubwa sana japo wanasaidiwa sana na nchi kama Marekani na Uingereza kwa kiasi kikubwa. Lakini kama wasingekuwa na nguvu binafsi msaada wa Marekani ungeishia kuwa kama msaada wa Urusi kwa nchi za Kiarabu ambazo nyingi zimepangaranyika kama SYRIA, IRAQ na LIBYA. Kubwa ambalo wanafanya tofauti na nchi nyingine ni kucheza na saikolojia za viongozi wa kidini wa nchi nyingi hapa duniani. Mfano mpaka leo hii Wakristo wengi duniani hasa wale wenye ushawishi Marekani kama John Hagee wanahubiri kwamba kuivamia Israeli ni kupigana na mkono wa Mungu na kuleta laana. Unaweza kuwa hujui lakini hii yote ni kazi ya Intelijensia.

WIZARA YA ULINZI YA IRAN- Marekani na NATO wamewawinda hawa jamaa tokea mwaka 1979 na wakawawekea vikwazo vikali sana lakini mpaka leo hii majama wanadunda. Kila siku wanasayansi wakubwa wanaongezeka na wanauzima ushawishi wa Marekani na Israeli usiendelee kutanuka katika Ukanda wa Mashariki ya kati. Wanayatumia makundi kama Hezbollah na Hamas kuwashughulikia Israeli na mpaka sasa wamefanya kazi kubwa sana Urusi nchini Syria ili kulinda serikali ya Bashar Al Assad. Hata kama wanasaidiwa na Urusi na Uchina wao wenyewe wameweza kusimama kiasi cha kuwafanya mahasimu wao wakubwa Wamarekani wakae Mezani ili kusaini mikataba ya Kinyuklia ambayo mataifa mengi ya Magharibi yalipinga. Iraq, Libya, Syria na Afghanistani zimepangaranyuka lakini hawa majamaa bado ni wabishi sana. Adui yao mwingine ni Ufalme wa Saudi Arabia ambao una jeshi kubwa na utajiri mkubwa lakini bado wanawaogopa sana Iran. Vyombo vyao vya Usalama vina nguvu sana.

B.N.D la Ujerumani- Baada ya vita ya pili ya dunia nchi ilipangaranyuka na watu hawakuwapenda kabisa Wajerumani. Ikafika kipindi kwamba hata silaha za nzito wakawa wanaogopa kumiliki kwasababu dunia nzima ingesema Ujerumani anataka kuleta matatizo kama ya miaka ya nyuma. Uwezo wa B.N.D ulijikita kwenye kujenga nguvu za kiuchumi na kisiasa. Ujerumani ilifanya makubwa sana kwenye uchumi miaka ya 60, 70 na 80 ambapo hakuna aliyeweza kuamini. Wanauchumi wakubwa kama Helmut Schmidt na Willy Brandt ambao waliwahi kuwa mawaziri wakuu wa nchi hiyo wanahistoria kubwa ndani ya B.N.D Walisadia kuijengea Ujerumani ushawishi mkubwa barani Ulaya na ana sauti kubwa sana ndani ya muungano wa Ulaya mpaka hii leo. Miaka ya 70 Ufaransa alikuwa anafanya majaribio mengi sana ya silaha za Kiatomiki na Waziri moja aliwahi kusema "Sisi Wafaransa tunatengeneza mabomu ya Nyuklia lakini Ujerumani yeye ana "Deutsche Mark" ambayo ni hela ya Ujerumani na ina nguvu kuliko mabomu yetu kwasababu inatumika na sisi mabomu tunayaweka kwenya ghala" Minong'ono inasema mpaka sasa Wajerumani na B.N.D wanaamini kwamba Tanzania ni yao na wanaushawishi mkubwa sana kwenye siasa za nchi yetu (Hili bado halijathibitika)

Baada ya haya yote, maswali yangu ni haya yafuatayo:

Je, kuna siku ambapo na sisi nchi yetu ya Tanzania inaweza ikafika hapo wenzetu walipofika (Kuwa na ushawishi mkubwa kisiasa, kidiplomasi, kiutamaduni na kiuchumi) ?


Je, ni kitu gani haswa ambacho nchi hizi walifanya hadi kuweza kuyafanya mataifa yao yawe na vyombo imara vya kijasusi ;sisi tunaweza kuiga kwao hizo mbinu kuviendeleza vyombo vyetu na taifa kwa ujumla?

Je, tufanye nini ili T.I.S.S ,M.I ya JWTZ , Intelijensia ya Jeshi la Polisi na Kitengo cha Ujasusi wa Kiuchumi: Ziweze kurudi kwenye sifa yake iliyotukuka ambayo waliijengea nchi yetu kuanzia miaka ya 60 hadi 80 mwishoni, kuanzia kwenye Ulinzi wa raia, Mipaka ya nchi, rasili mali zetu na kuendeleza sayansi na teknolojia?

NB: NAOMBA TUJIBU KIZALENDO BILA KULETA MIHEMKO YA KIVYAMA, NA TUSITUMIE MATUSI WALA KEJELI.

CC: MSEZA MKULU , Red Giant , mngony , Bukyanagandi , Infantry Soldier , de'levis , Yericko Nyerere , nankumene , Chief , kui , mshana jr , Kabaunyeri , The Emperor
 
olele

olele

JF-Expert Member
Joined
Dec 2, 2010
Messages
951
Likes
489
Points
80
olele

olele

JF-Expert Member
Joined Dec 2, 2010
951 489 80
Kwa jinsi navyoona mashirika ya kijasusi yote uliyoyataja ndio yanayoongoza na kuamua siasa za nchi husika, kwa maana nyingine ndio wanawaongoza wanasiasa..

lakini hapa kwetu ni kinyume chake, siasa ndio zinazowaongoza, wanasiasa ndio wanaowaongoza.

Polisi anaambiwa na mwanasiasa kamata yule, bila hata kujiuliza anamkamata kwa ajili ya nini, anatekeleza.

Waache kutumiwa na wanasiasa (kutumika kisiasa) wafanye mambo kwa weledi.
 
Lil G

Lil G

Member
Joined
Dec 15, 2014
Messages
83
Likes
73
Points
25
Lil G

Lil G

Member
Joined Dec 15, 2014
83 73 25
Uimara wa intelijensia katika nchi inategemea mambo mengi ila kwangu naona mambo makubwa mawili.

1. Uzalendo wa hali ya juu.
2. Nguvu ya kiuchumi.

Ukiangalia hizo nchi ulizoainisha kua zipo juu kiintelijensia, angalia uzalendo wa watu wake na vyombo vyake vya ulizi na usalama upo juu sana.

Intelijensia bila kua na nguvu ya uchumi ni ngumu. Baadhi ya nchi wana invest sana kwenye ulinzi na maisha ya watu yanadolola kiuchumi angalia CUBA na ETHIOPIA

Huo mtazamo wangu mdau
 
Malcom Lumumba

Malcom Lumumba

JF-Expert Member
Joined
Jul 26, 2012
Messages
13,296
Likes
36,347
Points
280
Malcom Lumumba

Malcom Lumumba

JF-Expert Member
Joined Jul 26, 2012
13,296 36,347 280
Uimara wa intelijensia katika nchi inategemea mambo mengi ila kwangu naona mambo makubwa mawili.

1. Uzalendo wa hali ya juu.
2. Nguvu ya kiuchumi.

Ukiangalia hizo nchi ulizoainisha kua zipo juu kiintelijensia, angalia uzalendo wa watu wake na vyombo vyake vya ulizi na usalama upo juu sana.

Intelijensia bila kua na nguvu ya uchumi ni ngumu. Baadhi ya nchi wana invest sana kwenye ulinzi na maisha ya watu yanadolola kiuchumi angalia CUBA na ETHIOPIA

Huo mtazamo wangu mdau
Mkuu wangu nimekuelewa sana,
Wazalendo hata Tanzania wapo, wewe mwenyewe ukiwa mojawapo.
Muhimu ni kwamba hakuna vyombo vinavyokuwa na bajeti kubwa sana katika nchi kama Ulinzi na Usalama,
Hili nimeliona kwa nchi tajiri na maskini. Ukisoma Brandt Report ya mwaka 1980 inasema Afrika haiendelei kwasababu sehemu kubwa ya bajeti zao inaenda kwenye Ulinzi na Usalama tofuati na shughuli za Kijamii kama afya na elimu.

Ile ripoti ni kithibiti tosha kwamba tunawekeza sana kwenye Usalama,
Tanzania ile ya Ujamaa yenye wasomi wachache na uchumi wa kuvuta kama mnati ilikuwa ina vyombo Imara sana,
Apson Mwang'onda aliyewahi kuwa mkurugenzi wa TISS alikiri kwamba uwezo wa TISS ya kuanzia 1997 hadi leo,
Ina utofauti mkubwa na ile ya akina Mzee Mzena, Kitine na Kombe hasa kwenye Weredi.

Swali langu kubwa ni kwamba kwa hali ilivyo sasa na kipindi kile,
Tanzania yetu ingekuwa imara sana kwenye mambo ya Ulinzi na Usalama,
Ukiangalia uchumi umekuwa mkubwa na wasomi wameongezeka sana,
Lakini bado kasi yetu hairidhishi, Je, tumekosea wapi ili tuige wenzetu wa nje?
 
Malcom Lumumba

Malcom Lumumba

JF-Expert Member
Joined
Jul 26, 2012
Messages
13,296
Likes
36,347
Points
280
Malcom Lumumba

Malcom Lumumba

JF-Expert Member
Joined Jul 26, 2012
13,296 36,347 280
Kwa jinsi navyoona mashirika ya kijasusi yote uliyoyataja ndio yanayoongoza na kuamua siasa za nchi husika, kwa maana nyingine ndio wanawaongoza wanasiasa..

lakini hapa kwetu ni kinyume chake, siasa ndio zinazowaongoza, wanasiasa ndio wanaowaongoza.

Polisi anaambiwa na mwanasiasa kamata yule, bila hata kujiuliza anamkamata kwa ajili ya nini, anatekeleza.

Waache kutumiwa na wanasiasa (kutumika kisiasa) wafanye mambo kwa weledi.
Mkuu hii inaweza kuwa sababu,
Lakini vyombo vya Usalama vinatakiwa kufanya kazi na wanasiasa kwa ukaribu wa hali ya juu,
Hili lipo kote duniani kuanzia Marekani, Uingereza hata Urusi; na hii ni protokali ya kiutawala.

Ukakasi unakuja pale ambapo ukaribu wa hivi vyombo na wanasiasa unakuwa siyo wenye Afya,
Hasahasa pale vinapoanza kuhusishwa na kazi za kisiasa nje kabisa ya mipaka ya majukumu yake,
Ninachojiuliza ni kwamba hivi vyombo vyetu havina protokali za kiutendaji zinazozuia majasusi wake kufanya kazi za kisiasa?
Au kuwaminya wanasiasa, wafanya biashara wakubwa au maafisa wa nje ya nchi wanapotaka kuingiza pua zao kwenye utendaji wa hizi idara? Wanakuwa wapi wakati haya yanatokea ?
 
amygdala

amygdala

JF-Expert Member
Joined
Jul 11, 2016
Messages
1,081
Likes
973
Points
280
amygdala

amygdala

JF-Expert Member
Joined Jul 11, 2016
1,081 973 280
ni mipango tu..naona nchi kama rwanda yenyew ni nchi ndogo ana lakin unaweza ukaona wana ambition ya kudominate pengine eneo lote hili la maziwa makuu kama mtu unaweza kusoma movements zao...................mi naona hawa jamaa wana ambitions za hatari kwe eneo hili na kwa jinsi walivyo serious lazima wataleta.......kngne pia nchi zetu znaweza kuwa na uwezo mzuri tu wa kijasusi lakin issue inaweza kuwa tunatumiaje uwezo huo kwa mfano C.I.A na K.G.B wote walikua wazuri lakin C.I.A pampja na mambo mengne lakn walifanikiwa sana kueneza ushawish wa marekan kwe nchi nyng pamoja na kufanya sana ujasus wa kiuchumi hata marafiki zake wa ulaya na hii ilsaidia kuboost uchumi wa nchi lakn K.G.B walijikita sana kwe ujasu wa mambo ya kijeshi pamoja na kueneza ucommunist na hii ilisaidia nchi kuwa taifa kubwa lenye ushawish na uwezo wa kujilinda lakin haikusaidia nchi kiuchumi...........kwa nchi yetu sisi hapa ukiangalia tulipotoka na mambo meng tulioyafanya kusaidia nchi zngne enz za kupigania uhuru basi ni wazi inatakiwa tuwe very active kwe foreign intelligence ili tuwe na ushawish na nchi ambazo tulizisaidia na tusibaki tu kuwa na sifa za tulisidia cjui ukomboz but hao tuliowasaidia leo hii hatuna ushawsh kwe hzo nchi.................km kanchi km rwanda kanajiongeza kwann cc tunanchi kubwa na rasilimali kibao tusiweze? ni mipango tu hasa jesh letu na intelligency maana wao wapo kila cku but ila hizi sirikali zetu hubadilika kisiasa.........
 
bhachu

bhachu

JF-Expert Member
Joined
Jul 29, 2015
Messages
5,049
Likes
4,317
Points
280
Age
31
bhachu

bhachu

JF-Expert Member
Joined Jul 29, 2015
5,049 4,317 280
Nadhani tuwafuate Israel watueleze wamefanikiwaje na MOSSAD
 
mngony

mngony

JF-Expert Member
Joined
Jul 27, 2012
Messages
3,275
Likes
2,053
Points
280
mngony

mngony

JF-Expert Member
Joined Jul 27, 2012
3,275 2,053 280
Umezungungumza mengi Mkuu

Mashirika haya pia yanatofautiana uwezo katika aina mbalimbali za ukusanyaji taarifa. Mimi sio mjuzi ila niliwahi kusikia kwa Human Intelligency Tanzania tuko vizuri sana. Pia Uingereza kupitia GCHQ ndio wanaongoza kwa SIGNT.

Lakini overall kwangu mimi uimara ya mashirika haya ya kijasusi unategemea sana na mambo mawili
1.Uimara wa Uchumi
2.Uzalendo

1.Uchumi ndio inawezesha vitu vingi Mkuu, kuanzia teknolojia, vifaa, mafunzo, mazingira bora ya kufanya kazi n.k. nitoe mfano tu kidogo, nchi hizo zenye uchumi mkubwa serikali zina data base ya kila mwananchi, karibu taarifa zake nyingi zimeunganishwa na kurahisisha mtu kupatikana pale anapohitajika. Sasa fananisha na nchi zinazoendelea, mfano kuwapata wanadaiwa wa bodi ya mikopo ni ngumu kiasi, angalau sasa tunaenda huko

Ulimwengu umebadilika sana, teknolojia imekuwa kwa kiasi kikubwa sana, hivyo matumizi ya teknolojia yana msaada mkubwa sana katika uimarishaji wa taasisi katika ukuusanyaji wa taarifa, maana cha muhimu ni taarifa. Uwezo wa kukusanya taatifa nyingi ndio unakufanya uwe bora. Pamoja na teknlojia sikatia kuwa bado Human Intelligency ina umuhimu wake.

Lakini pia uchumi mkubwa ndio umewawezesha wenzetu kuwa na taasisi zaidi ya moja na kugawana majukumu. Japo sisi tuna Idara ya mambo ndani, nje na hiyo ya jeshi lakini wenzetu wanafull taasisi inasaidia kidogo kurahisisha majukumu. Sisemi kama sisi hatuwezi hapana, ila ni bora zaidi kwangu mimi nionavyo. Ukiangalia UK wana hiyo MI6, MI5, na GCHQ. US wana zaidi ya 15, Isreal nao. Angalau wanazaidi ya moja. Russia waliwahi kugundua MI6 wa waingereza kuwa wanatumia dead drop ya tofali la kutengeneza ambalo waliliweka sehemu katika ukuta wa mtaa mmoja ambapo majasusi wa kiingereza walikuwa wakiweka na kuchukua taarifa kwa wireless. Yote ni teknolojia hiyo

Ndio maana kama sio China kuiba teknolojia wasingeweza leo kutunishiana msuli na mmarekani.

Pia ubora wa teknolojia wa CIA na Mossad imewaathiri sana wa Iran kuelekea umiliki wa silaha za nyuklia. Japo umewataja na kuwasifia kuwa wameweza kupambana na wababe kiukweli wameshindwa hasa kutokana na unyuma teknolojia( soma kitabu Spies against armageddon)

2. Uzalendo ndio nguzo kubwa sana, hiki kimewasaidia sana watu kama Mossad na kuwaumiza sana Waarabu. Muisrael hata akiwa wapi ana uzalendo wa hali juu sana. Jonathan Pollard alikuwa CIA, unaweza sema kulikuwa na maslahi zaidi na bora maana nchi ilikuwa imeshaendelea lakini asili yake na uzalendo wake kwa Israel na shauku ya kutaka kuona linasimama, aliiba sira za intelligency ya jeshi na kupeleka kwao. Waisrael wengi ndio wako hivyo mashirika karibu yote nchi mbalimbali. Uzalendo ni nguzo muhimu,kama mtu yuko kwa watu kakualia nakusomea huko ndio yuko hivyo je akiwa kwake kabisa atakuwaje? Isreal iliwatumia waisrael wengi sana walio nchi za kiarabu, hao ndio waliwapa ushindi, walipeleka taarifa Isreal. Hii kutapakaa naona wanyarwanda ndio wanaiga sana. Operesheni wahamiani haramu ilikuwa nzuri kwa mtizamo wangu na itakiwa kuwa endelvu

Kuna mtu kataja wanyarwanda kuwa wanaonekana kuwa na ambitions za kutawala Afrika mashariki, hilo ni kweli na mimi naliona, hawa jamaa wanafanya juu chini kuitawala afrika mashariki/maziwa makuu. Hata wakenya wameweka juhudi sana kwenye ujasusi wa kiuchumi pia. Wanyarwanda wamejitapakaza sana ukanda huu na wakijatahidi kujiingiza kwenye mamlaka za ushawishi na sehemu nyeti, hapa najua wengi tunafahamu haihitaji maelezo. Niliwahi kukutana na mwanafunzi wa kinyarwanda wakati nasoma, yeye alikuwa Rais wa chuo, pia akagombea alichukua kadi ya Chama na akatokea kuwa kiongozi wa Chama, na akatokea kuwa mmoja ya viongozi wa chama tuliokutana na Mh Rais. Hakuwa mtanzania na kwao ni Kigali na ana ndugu zake bado wapo Kigali lakini kujua hayo ilihitaji ujanja na akili ya kujiongeza. Sasa hata kwa kumuangalia tu unajua huyu sio. Sasa imagine huyu anatoka hapo, anakuwa endorsed na Chama mwisho anapata nafasi kuingia mamlaka za uongozi wa nchi kuanzia chini mpaka anafika juu. Mwisho ndio hao tunaskia wamepotelea Rwanda. Mtu huyo anapata nafasi ya kushikana mikono na Rais tena kipindi tuna uhusiano wa kulegalega Rwanda hadi kuwepo kwa tishio la usalama. Dodoma kule kuna wanyarwanda wamejaa sana utafikiri walijua tutahamia Dodoma. Wame target bunge na wabunge. Wengine wanapitia kigoma kisha wanatoka kule kuja kusoma Vyuoni, alafu anasema anatoka Kigoma. Cha ajabu akimaliza chuo, haondoki Dodoma anabaki hapo mjini anatafuta shughuli ya kizushi, wengi ni wa kike. Wanyarwanda wanatumia sana majasusi wa kike kutokana na uzuri wao kama honey trap, na pia uwezo wa kuvaa uhusika.Ndio tunasikia Waziri kaibiwa na mwanamke aliyelala naye

Sijui sisi tulikuaje huko kabla wala sasa hivi kwa sababu sipo wala sina habari yeyote lakini naona kuna juhudi zaidi zinahitajika. Leo hii chukulia mfano Burundi, Congo kote Rwanda anataka kuweka ushawishi wake. Rwanda kamleta Sudan Kusini jumuiya ya EA alafu tumeachiwa mzigo wa kusuluhisha migogoro yake. Leo Museveni anamsikiliza Rwanda. Wanafanya juhudi kuongeza ushawishi. Leo sisi kweli wa kuomba Rwanda kutuwekea mfumo wa computer kwenye taasisi zetu nyeti!

Kwenye uchumi angalia jambo dogo tu, siku tunapitisha bajeti yetu, Kenya wao wakapitisha kesho yake. Kuna vitu tulivichukua Waziri akitoa mfano wa Kenya kesho yake Kenya wakavitoa hivyo vitu, ni katiika ushindani wa kiuchumi. Haikutokea bahati mbaya

Samahani niko njiani kwenye daladala kama nimeandika haraka bila mtiririko mzuri.

MALCOM LUMUMBA
 
Malcom Lumumba

Malcom Lumumba

JF-Expert Member
Joined
Jul 26, 2012
Messages
13,296
Likes
36,347
Points
280
Malcom Lumumba

Malcom Lumumba

JF-Expert Member
Joined Jul 26, 2012
13,296 36,347 280
Umezungungumza mengi Mkuu

Mashirika haya pia yanatofautiana uwezo katila aina mbalimbali za ukusanyaji taarifa. Mimi sio mjuzi ila niliwahi kusikia kwa Human Intelligency Tanzania tuko vizuri sana. Pia Uingereza kupitia GCHQ ndio wanaongoza kwa SIGNT, Signal intelligency.

Lakini overall mwangu mimi uimara ya mashirika haya ya kijasusi unategemea sana na mambo mawili
1.Uimara wa Uchumi
2.Uzalendo

1.Uchumi ndio inawezesha vitu vingi Mkuu, kuanzia teknolojia, vifaa, mafunzo, mazingira bora ya kufanya kazi n.k. nitoe mfano tu kidogo, nchi hizo zenye uchumi mdogo serikali ina data base ya kila mwananchi, karibu taarifa zake nyingi zimeunganishwa na kurahisisha mtu kupatikana pale anapohitajika. Sasa fananisha na nchi zinazoendelea, kuwapata wanadaiwa wa bodi ya mikopo ni shida

Ulimwengu umebadilika sana, teknolojia imekuwa kwa kiasi kikubwa sana, hivyo matumizi ya teknolojia yana msaada mkubwa sana katika uimarishaji wa taasisi katika kukusanya taarifa, maana cha muhimu ni taarifa. Uwezo wa kukusanya taatifa nyingi ndio unakufanya uwe bora. Pamoja na teknlojia sikatia kuwa bado Human Intelligency ina umuhimu wake.

Lakini pia uchumi mkubwa ndio umewawezesha wenzetu kuwa na taasisi zaidi ya moja na kugawana majukumu. Japo sisi tuna Idara ya mambo ndani, nje na hiyo ya jeshi lakini wenzetu wanafull taasisi inasaidia kidogo kurahisisha majukumu. Sisemi kama sisi hatuwezi hapana, ila ni bora zaidi kwangu mimi. Ukiangalia UK wana hiyo MI6, MI5, na GCHQ. US wana zaidi ya 15, Isreal nao. Angalau wanazaidi ya moja. Russia waliwahi kugundua MI6 wa waingereza kuwa wanatumia dead drop ya tofali la kutengeneza ambalo waliliweka sehemu katika ukuta wa mtaa mmoja ambapo majasusi wa kiingereza walikuwa wakiweka na kuchukua taarifa kwa wireless. Yote ni teknolojia hiyo

Ndio maana kama sio China kuiba teknlojia wasingeweza leo kutunishiana msuli na mmarekani.

Pia ubora wa teknolojia wa CIA na Mossad imewaathiri sana wa Iran kuelekea umiliki wa silaha za nyuklia. Japo umewataja na kuwasifia kuwa wameweza kupambana na wababe kiukweli wameshindwa hasa kutokana na unyuma teknolojia( soma kitabu Spies against armageddon)

2. Uzalendo ndio nguzo kubwa sana, hiki kimewasaidia sana watu kama Mossad na kuwaumiza sana Waarabu. Muisrael hata akiwa wapi ana uzalendo wa hali juu sana. Jonathan Pollard alikuwa CIA, unaweza sema kulikuwa na maslahi zaidi na bora maana nchi ilikuwa imeshaendelea lakini asili yake na uzalendo wake kwa Israel na shauku ya kutaka kuona linasimama, aliiba sira za intelligency ya jeshi na kupeleka kwao. Waisrael wengi ndio wako hivyo mashirika karibu yote nchi mbalimbali. Uzalendo ni nguzo muhimu,kama mtu yuko kwa watu kakualia nakusomea huko ndio yuko hivyo je akiwa kwake kabisa atakuwaje? Isreal iliwatumia waisrael wengi sana walio nchi za kiarabu, hao ndio waliwapa ushindi, walipeleka taarifa Isreal. Hii kutapakaa naona wanyarwanda ndio wanaiga sana. Operesheni wahamiani haramu ilikuwa nzuri kwangu

Kuna mtu kataja wanyarwanda kuwa wanaonekana kuwa na ambitions za kutawala Afrika mashariki, hilo ni kweli na mimi naliona, hawa jamaa wanafanya juu chini kuitawala afrika mashariki/maziwa makuu. Hata wakenya wameweka juhudi sana kwenye ujasusi wa kiuchumi pia. Wanyarwanda wamejitapakaza sana ukanda huu na wakijatahidi kujiingiza kwenye mamlaka za ushawishi na sehemu nyeti, hapa najua wenfi tunafahamu haihitaji maelezo. Niliwahi kukutana na mwanafunzi wa kinyarwanda wakati nasoma, yeye alikuwa Rais wa chuo, pia akagombea alichukua kadi ya Chama na akatokea kuwa kiongozi wa Chama, na akatokea kuwa mmoja ya viongozi wa chama waliokutana na Mh Rais. Hakuwa mtanzania na kwao ni Kigali na ana ndugu zake bado wapo Kigali lakini kujia hayo ilihitaji ujanja na akili ya kujiongeza. Sasa hata kwa kumuangalia tu unajua huyu sio. Sasa imagine huyu anatoka hapo, anakuwa endorsed na Chama mwisho anapata nafasi kuingia mamlaka za uongozi wa nch kuanzia chini mpaka anafika juu. Mwisho ndio hao tunaskia wamepotelea Rwanda. Dodoma kule kuna wanyarwanda wamejaa sana utafikiri walijua tutahamia Dodoma. Wame target bunge na wabunge. Wengine wanapitia kigoma kisha wanatoka kule kuja kusoma Vyuoni, alafu anasema anatoka Kigoma. Cha ajabu akimaliza chuo, haondoki Dodoma anabaki hapo mjini anatafuta shughuli ya kizushi, wengi ni wa kike. Wanyarwanda wanatumia sana majasusi wa kike kutokana na uzuri wao kama honey trap, na pia uwezo wa kuvaa uhusika.Ndio tunasikia Waziri kaibiwa na mwanamke aliyelala naye

Sijui sisi tulikuaje huko kabla wala sasa hivi kwa sababu sipo wala sina habari yeyote lakini naona kuna juhudi zaidi zinahitajika. Leo hii chukulia mfano Burundi, Congo kote Rwanda anataka kuweka ushawishi wake. Rwanda kamleta Sudan Kusini jumuiya ya EA alafu tumeachiwa mzigo wa kusuluhisha. Leo Museveni anamsikiliza Rwanda. ushawishi wanajitahidi watushinde. Leo sisi kweli wa kuomba Rwanda kutuwekea mfumo wa computer kwenye taasisi zetu nyeti!

Kwenye uchumi angalia jambo dogo tu, siku tunapitisha bajeti yetu, Kenya wao wakapitisha kesho yake. Kuna vitu tulivichukua Waziri akitoa mfano wa Kenya kesho yake Kenya wakakitoa hiko kitu, ni katiika ushindani wa kiuchumi. Haikutokea bahati mbaya

Samahani niko njiani kwenye daladala kama nimeandika haraka bila mtiririko mzuri.

MALCOM LUMUMBA

Mkuu Shukrani sana.
Umetufungua kwa kiasi kikubwa.
Kwa maelezo yako haya ni dhahiri kwamba Tanzania kuna sehemu tumejikwaa,
Wanasiasa hasahasa CCM ndiyo wameharibu nchi, yote haya yametokea mikononi mwao. (Halina Ubishi)

Japo ukiwasikiliza wanausalama wetu wanakwambia kwamba tupo upo salama,
Hata hapo ulipowasifia kwamba wako vizuri kwenye Ulinzi wa ndani na Human Intelligency,
Hili sina uhakika sana kwasababu matukio na hali ya nchi vinazungumza kinyume kabisa na hizo sifa zao.

Wewe mkuu unahisi nini kifanyike ili kulikomboa hili taifa?
Maana hatupo mahali pazuri kama ambavyo wengi wanajiaminisha.

 
Malcom Lumumba

Malcom Lumumba

JF-Expert Member
Joined
Jul 26, 2012
Messages
13,296
Likes
36,347
Points
280
Malcom Lumumba

Malcom Lumumba

JF-Expert Member
Joined Jul 26, 2012
13,296 36,347 280
ni mipango tu..naona nchi kama rwanda yenyew ni nchi ndogo ana lakin unaweza ukaona wana ambition ya kudominate pengine eneo lote hili la maziwa makuu kama mtu unaweza kusoma movements zao...................mi naona hawa jamaa wana ambitions za hatari kwe eneo hili na kwa jinsi walivyo serious lazima wataleta.......kngne pia nchi zetu znaweza kuwa na uwezo mzuri tu wa kijasusi lakin issue inaweza kuwa tunatumiaje uwezo huo kwa mfano C.I.A na K.G.B wote walikua wazuri lakin C.I.A pampja na mambo mengne lakn walifanikiwa sana kueneza ushawish wa marekan kwe nchi nyng pamoja na kufanya sana ujasus wa kiuchumi hata marafiki zake wa ulaya na hii ilsaidia kuboost uchumi wa nchi lakn K.G.B walijikita sana kwe ujasu wa mambo ya kijeshi pamoja na kueneza ucommunist na hii ilisaidia nchi kuwa taifa kubwa lenye ushawish na uwezo wa kujilinda lakin haikusaidia nchi kiuchumi...........kwa nchi yetu sisi hapa ukiangalia tulipotoka na mambo meng tulioyafanya kusaidia nchi zngne enz za kupigania uhuru basi ni wazi inatakiwa tuwe very active kwe foreihn intelligence ili tuwe na ushawish na nchi ambazo tulizisaidia na tusibaki tu kuwa na sifa za tulisidia cjui ukomboz but hao tuliowasaidia leo hii hatuna ushawsh kwe hzo nchi.................km kanchi km rwanda kanajiongeza kwann cc tunanchi kubwa na rasilimali kibao tusiweze? ni mipango tu hasa jesh letu na intelligency maana wao wapo kila cku but ila hizi sirikali zetu hubadilika kisiasa.........
Mkuu hilo ndiyo swali ninalojiuliza mpaka leo hii,
Tangu nimebalehe nimekuwa nikisikia na kuzisoma habari za Tanzania yetu,
Mambo mazuri na ya kishujaa iliyoyafanya ndani na nje ya mipaka yake kipindi cha Mzee Nyerere.
Leo haya yote yamebaki kuwa ni historia na ukiangalia vizuri hata huo ushawishi wa Tanzania unanyauka kwa kasi sana.
Upande wa pili siasa yetu ya ndani ilishatushinda miaka miaka thelethini iliyopita,
Ni dhahiri tumejikwaa vibaya na inabidi tujitathimini upya kama Taifa tena kwa uwazi tu,
Mkuu mngony kaelezea vizuri sana hapo juu.
 
amygdala

amygdala

JF-Expert Member
Joined
Jul 11, 2016
Messages
1,081
Likes
973
Points
280
amygdala

amygdala

JF-Expert Member
Joined Jul 11, 2016
1,081 973 280
mi kwa mtazamo wangu ningependa tuwe na determination flan tuwaze hata kuja kuwa regional power katika eneo hili sasa huko hatuwez fika kwa kuishia kusema tuko salama(defensive) bali inabidi tuwe na uwezo wa kijasusi kwe offensive pia..nchi ndogo kama rwanda inajidai kumanipulate mambo km tunavyoona kwann sisi tushndwe? we need to project our influence hvyo idara zetu za ujasusi ziwekeze huko pia..kama kina saudia,iran na turkey wanafanya basi na sisi tunaweza fanya pia ilacha kwanza inabidi tuwe na hio ambition
 
Alphaking2023

Alphaking2023

JF-Expert Member
Joined
May 20, 2015
Messages
2,081
Likes
1,885
Points
280
Alphaking2023

Alphaking2023

JF-Expert Member
Joined May 20, 2015
2,081 1,885 280
Nimeupenda huu uzi binafsi napenda sana kufanya kazi kama intelligence kwa maslahi ya taifa Ila naamini intelligence itakuwa bora kama watu wake watakuwa wazalendo halisi
 
Bujibuji

Bujibuji

JF-Expert Member
Joined
Feb 4, 2009
Messages
43,160
Likes
40,580
Points
280
Bujibuji

Bujibuji

JF-Expert Member
Joined Feb 4, 2009
43,160 40,580 280
Is a good spy born or made?
Tukiweza kujibu hapa tutajua nini cha kufanya ili kuwa na vitengo vya kiintelijensia vyenye mashiko
 
Compact

Compact

JF-Expert Member
Joined
Oct 22, 2015
Messages
3,807
Likes
8,678
Points
280
Compact

Compact

JF-Expert Member
Joined Oct 22, 2015
3,807 8,678 280
TISS inatakiwa iwe taasisi inayojitegemea kwa Kila kitu. Tofauti na sasa ambapo rais ndo boss wao na hutakiwa kutii matamko ya Boss wao bila kuzingatia yana athari zipi katika jamii.

Pili,sijajua kwa hapa kwetu Intelijensia ya Uchumi upo katika level gani. Intellijensia hii inakuja kuwa muhimu sana na yenye manufaa makubwa kwa miaka mingi ijayo. Kama tunataka kuwa taifa lenye ushawishi katika nyanja zingine za Kijamii lazima kwanza tuwe na Uchumi imara na hilo hutegemea na intelligensia yetu imefanya kazi kwa namna ipi.

TISS naamini wapo humu,mfikishieni Taarifa boss wenu afanye kazi kubwa sana katika kuinua na kuendeleza intelijensia ya mambo ya Uchumi. Ina manufaa mengi kipindi kijacho.

Pili,taasisi hii ya Ujasusi isiwe kitu cha kificho kama ilivyo sasa. Ofisi zao ziwe wazi na taratibu zao zijulikane.

Wasiwe wazuri tu kwenye kutoboa watu macho na kung'oa meno pamoja na kucha.
 
jamiink

jamiink

Senior Member
Joined
Dec 24, 2014
Messages
157
Likes
149
Points
60
jamiink

jamiink

Senior Member
Joined Dec 24, 2014
157 149 60
Ahsante kwa mleta uzi kuna vitu vikuu viwili wachangiaji wengi wamevitaja navyo ni uzalendo na uchumi. Mimi naomba niongeze kimoja katika hivyo ambavyo kuna baadhi wamekigusia nacho ni kuwa na malengo mamoja kama nchi.
Tunaweza tukajifunza kuwa na uzalendo, tukaweka mbinu na ushawishi wa kiuchumi lakini kama hatuna lengo moja kama Taifa tutakuwa tunazurura kwenye vichaka tu bila sababu.
Mfano toka tupate uhuru nchi hii imesema ina maadui watatu ujinga,maradhi na rushwa lakini kwa mienendo yetu haionekani kama kweli kuna nia ya dhati ya kupambana na maadui zetu bali tumekuwa na porojo tu katika hili.

Katika kuunganisha haya yote matatu ningependa kusema turudi pale kwenye kuwa na lengo moja kama Taifa, tujenge uzalendo wa kweli kama Taifa kwa maana ya kila mtanzania kuwa na sauti na mchango wa mawazo yake kuthaminiwa katika ustawi na maslahi mapana ya Taifa (hii unaweza ona kwenye mataifa kama US na UK) ambapo demokrasia ya kweli ndo kitu muhimu zaidi kwao. Vitengo vya ulinzi na usalama kufanya kazi kwa weledi na kuwafanya wananchi kuwapenda na kuwathamini pia. Tukiweza kufanikisha haya tunaweza kuirudisha nchi pamoja na kuweza kujenga uchumi wetu kwa pamoja.

Kama tutashindwa kuwa na lengo moja kama Taifa na kukubali kuwa wazalendo wa kweli basi tusahau kuwa na uchumi mkubwa. Wenzetu wameendelea kwa sababu siku zote wamekuwa wamoja na wanaheshimu fikra za mwananchi katika nchi yao.

Muhimu: Intelejensia bila kuaminika na wananchi wake ni ngumu sana kuwa imara maana itapata shida katika kukusanya taarifa. Mfano hapa kwetu mtu akijulikana kama TISS au Polisi urafiki wa yeye na mwananchi wa kawaida unapotea, watu wanamuona kama snitch tu lakini kwa wenzetu watu hao wanaheshimika kwa sababu wanaheshimu wengine na wanatunza siri za watoa taarifa.
Kwetu hapa ni ngumu sana kupata whistle blower kwa sababu hakuna uhakika wa kumlinda mtoa taarifa ndio maana mpaka vitu virushwe kwenye mitandao ya kijamii ndio watu wanafanyia kazi baada ya kuona aibu.

Pia wananchi wanatakiwa wajue haki zao kikatiba na waweze kuzidai na kuzitekeleza kwa wengine hii itasaidia sana kuweka mazingira rafiki kati ya viongozi na wanaowaongoza.
 

Forum statistics

Threads 1,273,319
Members 490,351
Posts 30,477,938