Hivi ni nani mshauri wa Mbowe na Dr Slaa..?

Juliana Shonza

JF-Expert Member
Dec 19, 2012
2,009
1,607
Katika vigezo muhimu na utaratibu unaofaa wa uongozi ulio bora ni pamoja na kuwa na ushauri. Kiongozi bora ni yule mwenye washauri bora, kupwaya kwa kiongozi yeyote ni matokeo ya kupwaya kwa washauri wake.

Nimeanza kwa utangulizi huo nikienda sambamba na anuani ya thread yangu juu ya washauri wa viongozi wawili wa juu wa chama cha demokrasia na maendeleo Chadema). Nimefikia hatua ya kujiuliza hayo kutokana na mwelekeo mbovu na kile kinachodhihirika kuwa kufa kwa Chadema kama chama kikuu cha upinzani hapa nchini.

chadema inakufa na inakufa kwa kasi ambayo haijatarajiwa, inakufa haraka sana. Kwani sasa ni kawaida kila uchao kusikia kuna mmoja wa kiongozi anaachia ngazi achilia mbali wanachama ambao wanarudisha kadi kwenye mikutano na wale ambao wamwamua kutupa kadi zao kimya kimya.

Hali ni mbaya kwani hata wale ambao hawakuwa wanachama bali walivutiwa na chama hiko huku mitaani nao wamepoteza mwelekeo na kukosa matumaini na Chama iko.

Miongoni mwa sehemu muhimu na ambazo zilikuwa zinatoa mwelekeo kwa Chadema ni kujiimarisha kwake katika eneo la vyuo vikuu, kwani katika jamii yetu wanazuoni ni watu ambao wanatoa mwelekeo kwa jamii nyingine ambayo inawasikiliza na kuwaamini. Lakini ni ukweli ulio bayana kuwa hakuna taasisi yeyote ya chuo ambayo inaielewa chadema tena, matamshi ya wanazuoni wakati wa bunge la katiba ambayo yamekuwa yakiiunga mkono CCM, serikali za wanafunzi kuwa chini ya CCM na hata wanafunzi kujiunga kwa wingi na CCM ni ushuhuda kuwa CCM inaimarika vyuoni na Chadema imekufa vyuoni. Mkutano wa Nape juzi na wanavyuo wa SAUT mwanza, sehemu ambayo ilikuwa ni Ngome ya CDM ni uthibitisho tosha, achilia mbali mkutano wa Riz Kikwetena wanavyuo wa Morogoro.

Lakini turudi kwenye vyombo vya habari ambako ndiko kuliibeba sana CDM katika kipindi chote cha uhai wake.Nako hali ni tofauti kabisa, leo ni kana kwamba chadema ama chama chochote cha upinzani hakipo kwani wanaoripotiwa ni CCM tu. Na ukweli kuhusu Chama Cha Siasai ni huu If u don't exist in media u don't exist kabisa. P. A ni sehemu muhimu katika Siasa na Chadema wameshachemka kabisa katika hili.

BAVICHA nako ni majanga matupu wamebaki watu wasiojielewa hawana harakati, hawana muamko wala hawajitumi. Wanasubiri maelekezo ya kushughulikia watu badala ya kufanya kazi za jumuiya ili kusaidia Chama.

LAKINI nikiwa ni mwanasiasa ambaye naiona na nimefanya siasa za upinzani na sasa chama tawala nautazama huu kuwa ni udhaifu wa viongozi wa juu wa Chama, udhaifu unaotokana na ushauri mbovu. Na ndipo ninapojiuliza nani hasa mshauri wa wakuu hao.

Kauli za Dr zinaonyesha kupoteza kabisa mwelekeo na kushindwa. Kujitoa kwa CDM kushiriki siasa za Zanzibar ni hatua moja kubwa ya kukifuta chama hiko katika vichwa vya wazanzibar kabisa ambao ni sehemu muhimu ya jamhuri.

Matendo ya Mbowe kukacha misiba ya viongozi wenzake wa juu na mengineyo inadhihirisha kukosa ushauri bora. Maamuzi yanayofanywa na viongozi kutokana na hulka binafsi mara nyingi huwa sio maamuzi sahihi lakini maamuzi yatokanayo na Ushauri mara zote yamekuwa maamuzi sahihi.

Umefika wakati sasa kwa Chadema kuunda THINK TANK kwa maendeleo ya Chama hicho, ni wakati wa kuwapuuza wapiga debe na kuacha kuwaangalia vijanawanaojipendekeza kwa viongozi kuwa ndio wenye msaada kwa viongozi hao, vijana wa NDIO MZEE hawana tija tena ndani ya Chadema. Watafute watu, vijana makini ambao wanauwezo wa kuchambua mambo na kutoa ushauri wenye kufaa, vijana ambao hawatahofu kuwaambia Mzee hapa umekosea na ili twende sawa fanya haya.

Naendelea kuwafunza Siasa, ikiwa tu mpo tayari kujifunza.
 
Wakati ukiwa chadema kama kiongozi kabla hujahamia nyumba ya jirani ambako huna cheo chochote, hao viongozi walikuwa wanashauriwa na nani?

Mbona watu mnakuwa wepesi wa kusahau fadhira? Maisha ni zaidi ya siasa, ngoja tuone mwisho wa future yako maana sie wengine toka mababu zetu mpk mama zetu walikuwa huko huko ila leo sisi ndiyo tunawasaidia kwa hali na mali

Mnatumia pesa nyingi sana kuua upinzani nchini wakati mnauwezo wakupeleka mswaada bungeni wa kufuta kabisa vyama vya upinzani mkabakia nyie tu, maana mmeshindwa hata kuhudumia watanzania na kuwapa maisha bora kwa sababu pesa inatoka bila mahesabu na nyingi inapelekwa kwenye mbinu za kimafia za kuua ama kuhonga viongozi wa vyama vya siasa

To be honest chama cha mapinduzi kinatengeneza chuki ya ajabu sana kwa siku za mbeleni, tutakuja shindwa hata peana mikono sababu ya chuki zenu na ubinafsi uliyowajaa mpk puani, trust me hamtakaa madarakani milele
 
Wakati ukiwa chadema kama kiongozi kabla hujahamia nyumba ya jirani ambako huna cheo chochote, hao viongozi walikuwa wanashauriwa na nani?

Mbona watu mnakuwa wepesi wa kusahau fadhira? Maisha ni zaidi ya siasa, ngoja tuone mwisho wa future yako maana sie wengine toka mababu zetu mpk mama zetu walikuwa huko huko ila leo sisi ndiyo tunawasaidia kwa hali na mali

Mnatumia pesa nyingi sana kuua upinzani nchini wakati mnauwezo wakupeleka mswaada bungeni wa kufuta kabisa vyama vya upinzani mkabakia nyie tu, maana mmeshindwa hata kuhudumia watanzania na kuwapa maisha bora kwa sababu pesa inatoka bila mahesabu na nyingi inapelekwa kwenye mbinu za kimafia za kuua ama kuhonga viongozi wa vyama vya siasa

To honest chama cha mapinduzi kinatengeneza chuki ya ajabu sana kwa siku za mbeleni, tutakuja shindwa hata peana mikono sababu ya chuki zenu na ubinafsi uliyowajaa mpk puani, trust me hamtakaa madarakani milele
Yeye ndo alikuwa anawashauri na ndo maana chama kilikuwa kinaenda vema. Baada ya kutoka tu wamebaki wahuni tu na ndo maana chama kinaenda mrama
 
Khaaa! haka kasichana tena??! Kakilala, kakiamka kanaota CDM! Sijui kaliingizwa "choo cha kike" sasa kanataka kurudi au kamekosa attention huko magambani...hata sielewi.
Wewe mtoto una jina zuri la mdogo wangu, acha porojo za kujidhalilisha. Uko CCM sasa, endelea achana na CDM. Ushauri tu.
 
Wakati ukiwa chadema kama kiongozi kabla hujahamia nyumba ya jirani ambako huna cheo chochote, hao viongozi walikuwa wanashauriwa na nani?

Mbona watu mnakuwa wepesi wa kusahau fadhira? Maisha ni zaidi ya siasa, ngoja tuone mwisho wa future yako maana sie wengine toka mababu zetu mpk mama zetu walikuwa huko huko

hana fadhira kwani mlimzaa mlimlea mlimsomesha alizaliwa na mama yake alilelewa na wazazi wake na alisomeshwa na serikali tena ya ccm
 
Khaaa! haka kasichana tena??! Kakilala, kakiamka kanaota CDM! Sijui kaliingizwa "choo cha kike" sasa kanataka kurudi au kamekosa attention huko magambani...hata sielewi.
Wewe mtoto una jina zuri la mdogo wangu, acha porojo za kujidhalilisha. Uko CCM sasa, endelea achana na CDM. Ushauri tu.
Muwe na utamaduni wa kujadili mada nyie misukule
 
Unataka kuomba kazi ya ushauri? Na kama inakufa Chadema si ndio uende mitaani ukasherehekee, kinakuuma nini utake Chadema iwe imara. Je huoni ikiwa imara na kuangusha Chama cha Interehamwe utakosa kazi hapo Lumumba.
Wewe kweli unajua kushirikisha ubongo wako na vidole vinavyoandika haya uliyoweka.
Hivi we binti mbona unaangusha walimu wako inaonekana walikupa degree kwa kuwatolea pichu au basi mitihani yako na assignment ulifanyiwa na vijana ili wapate....
 
jike dume

Naihurumia sana chadema kwa kuwa na watu wa aina yako. Najiuliza ikiwa wewe ndie mtu ambae chama kimekuona unafaa kupewa kazi ya kukisemea chama katika mitandao ya kijamii, chama hiko kitakuwa kimepoteza mwelekeo kiasi gani.

Nyie ni watu ambao mnaharibu Chama, mnafanya chama kikose support kutoka kwa watu wa maana, ambao wakiona maandishi yenu hapa wana-conclude kuwa Chadema ni sehemu yenye watu wa hovyo ambao kazi kubwa wanaoiweza ni matusi.
 
Last edited by a moderator:
Sasa kama ni hivyo si akae atulie anachotafuta Chadema nini uko. Kama CCM inamlea vizuri kwa nini anaangaika mno kama kuku anayetaga
hana fadhira kwani mlimzaa mlimlea mlimsomesha alizaliwa na mama yake alilelewa na wazazi wake na alisomeshwa na serikali tena ya ccm
 
Back
Top Bottom