Hivi ni nani mshauri wa Mbowe na Dr Slaa..?

Hivi ni nani mshauri wa Mbowe na Dr Slaa..?

Yeye ndo alikuwa anawashauri na ndo maana chama kilikuwa kinaenda vema. Baada ya kutoka tu wamebaki wahuni tu na ndo maana chama kinaenda mrama

Na wewe uwe na adabu mda mwingine usiwe kama kichaa akiona jalala tu anajua katajirika

Huyu mtoto ni nyoka nyie mpeni mda tu, kama aliweza kushawishika na kuanzisha chama ndani ya chama kwenu atashindwa fanya hivyo? Kuweni makini nae
 
Unafanya kazi kubwa sana kuwafundisha chadema siasa safi. Hongera unafaa!!!
 
Haka ka binti hivi CDM mlikapaga nini? maana kakinywa maji kanawaona kwenye glass!!, hakalali bali kanawaota nyie tu - mtakuwa na dawa aisee!!

Tunaomba muitengue hiyo dawa ili sasa kaanze kufanya kazi huko kaliko, vinginevyo watakafukuza na huko iwe tatizo lingine.
 
Wakati ukiwa chadema kama kiongozi kabla hujahamia nyumba ya jirani ambako huna cheo chochote, hao viongozi walikuwa wanashauriwa na nani?

Mbona watu mnakuwa wepesi wa kusahau fadhira? Maisha ni zaidi ya siasa, ngoja tuone mwisho wa future yako maana sie wengine toka mababu zetu mpk mama zetu walikuwa huko huko ila leo sisi ndiyo tunawasaidia kwa hali na mali

Mnatumia pesa nyingi sana kuua upinzani nchini wakati mnauwezo wakupeleka mswaada bungeni wa kufuta kabisa vyama vya upinzani mkabakia nyie tu, maana mmeshindwa hata kuhudumia watanzania na kuwapa maisha bora kwa sababu pesa inatoka bila mahesabu na nyingi inapelekwa kwenye mbinu za kimafia za kuua ama kuhonga viongozi wa vyama vya siasa

To be honest chama cha mapinduzi kinatengeneza chuki ya ajabu sana kwa siku za mbeleni, tutakuja shindwa hata peana mikono sababu ya chuki zenu na ubinafsi uliyowajaa mpk puani, trust me hamtakaa madarakani milele
Katika jambo ambalo haulijui ni kuwa tupo kwenye siasa ya vyama vingi. Hivyo imehalalishwa kwa vyama vya siasa kushindana ili mbabe atakayeshinda wenzake aweze kuongoza dola.

kulalamika kuwa CCM inauangamiza upinzani, ni sawa na CCM kulalamika Upinzani Unawamaliza. Ni ujinga uliopindukia kulaumu watu ambao wanapaswa wafanye unachokilalamikia ili waendelee kuwepo na wapate mafanikio.

Kama nyie mmeridhia kuwa fedha ya ruzuku ajikopeshe babu na nyingine achukue mbowe aende picnic Dubai mnategemea nini..?

Ni ujinga kuilaumu CCM kuwa inaua Upinzani, kwani huko ndiko kuimarika kwake.
 
Katika vigezo muhimu na utaratibu unaofaa wa uongozi ulio bora ni pamoja na kuwa na ushauri. Kiongozi bora ni yule mwenye washauri bora, kupwaya kwa kiongozi yeyote ni matokeo ya kupwaya kwa washauri wake.

Nimeanza kwa utangulizi huo nikienda sambamba na anuani ya thread yangu juu ya washauri wa viongozi wawili wa juu wa chama cha demokrasia na maendeleo Chadema). Nimefikia hatua ya kujiuliza hayo kutokana na mwelekeo mbovu na kile kinachodhihirika kuwa kufa kwa Chadema kama chama kikuu cha upinzani hapa nchini.

chadema inakufa na inakufa kwa kasi ambayo haijatarajiwa, inakufa haraka sana. Kwani sasa ni kawaida kila uchao kusikia kuna mmoja wa kiongozi anaachia ngazi achilia mbali wanachama ambao wanarudisha kadi kwenye mikutano na wale ambao wamwamua kutupa kadi zao kimya kimya.

Hali ni mbaya kwani hata wale ambao hawakuwa wanachama bali walivutiwa na chama hiko huku mitaani nao wamepoteza mwelekeo na kukosa matumaini na Chama iko.

Miongoni mwa sehemu muhimu na ambazo zilikuwa zinatoa mwelekeo kwa Chadema ni kujiimarisha kwake katika eneo la vyuo vikuu, kwani katika jamii yetu wanazuoni ni watu ambao wanatoa mwelekeo kwa jamii nyingine ambayo inawasikiliza na kuwaamini. Lakini ni ukweli ulio bayana kuwa hakuna taasisi yeyote ya chuo ambayo inaielewa chadema tena, matamshi ya wanazuoni wakati wa bunge la katiba ambayo yamekuwa yakiiunga mkono CCM, serikali za wanafunzi kuwa chini ya CCM na hata wanafunzi kujiunga kwa wingi na CCM ni ushuhuda kuwa CCM inaimarika vyuoni na Chadema imekufa vyuoni. Mkutano wa Nape juzi na wanavyuo wa SAUT mwanza, sehemu ambayo ilikuwa ni Ngome ya CDM ni uthibitisho tosha, achilia mbali mkutano wa Riz Kikwetena wanavyuo wa Morogoro.

Lakini turudi kwenye vyombo vya habari ambako ndiko kuliibeba sana CDM katika kipindi chote cha uhai wake.Nako hali ni tofauti kabisa, leo ni kana kwamba chadema ama chama chochote cha upinzani hakipo kwani wanaoripotiwa ni CCM tu. Na ukweli kuhusu Chama Cha Siasai ni huu If u don't exist in media u don't exist kabisa. P. A ni sehemu muhimu katika Siasa na Chadema wameshachemka kabisa katika hili.

BAVICHA nako ni majanga matupu wamebaki watu wasiojielewa hawana harakati, hawana muamko wala hawajitumi. Wanasubiri maelekezo ya kushughulikia watu badala ya kufanya kazi za jumuiya ili kusaidia Chama.

LAKINI nikiwa ni mwanasiasa ambaye naiona na nimefanya siasa za upinzani na sasa chama tawala nautazama huu kuwa ni udhaifu wa viongozi wa juu wa Chama, udhaifu unaotokana na ushauri mbovu. Na ndipo ninapojiuliza nani hasa mshauri wa wakuu hao.

Kauli za Dr zinaonyesha kupoteza kabisa mwelekeo na kushindwa. Kujitoa kwa CDM kushiriki siasa za Zanzibar ni hatua moja kubwa ya kukifuta chama hiko katika vichwa vya wazanzibar kabisa ambao ni sehemu muhimu ya jamhuri.

Matendo ya Mbowe kukacha misiba ya viongozi wenzake wa juu na mengineyo inadhihirisha kukosa ushauri bora. Maamuzi yanayofanywa na viongozi kutokana na hulka binafsi mara nyingi huwa sio maamuzi sahihi lakini maamuzi yatokanayo na Ushauri mara zote yamekuwa maamuzi sahihi.

Umefika wakati sasa kwa Chadema kuunda THINK TANK kwa maendeleo ya Chama hicho, ni wakati wa kuwapuuza wapiga debe na kuacha kuwaangalia vijanawanaojipendekeza kwa viongozi kuwa ndio wenye msaada kwa viongozi hao, vijana wa NDIO MZEE hawana tija tena ndani ya Chadema. Watafute watu, vijana makini ambao wanauwezo wa kuchambua mambo na kutoa ushauri wenye kufaa, vijana ambao hawatahofu kuwaambia Mzee hapa umekosea na ili twende sawa fanya haya.

Naendelea kuwafunza Siasa, ikiwa tu mpo tayari kujifunza.
For the first time I have to agree with you Juliana,Kweli unaonyesha bado una mapenzi na CHADEMA.Nikiwa kama Organizational analyst maelezo yako yamegusa kwenye kiini hasa yaani CHADEMA kuwategemea mno sheep followers and abandoning independent & critical followers.Kwa mwenye kukitakia mema Chama atakuunga mkono
 
We binti unaonekana una majonzi kweli kuiacha Chadema. ya nini husirudi upewe angalau hata kadi uwe mwanachama tu maana kazi ya siasa huwezi tena. Unaweza kuwa mmoja wa kuipigia kura tu. Vipi lakini ebu tujulishe, uko Lumumba wanawanyima nini mpaka unatamani kurudi Chadema na unataka uone Chadema inastawi? Hata hivyo bado unaweza kufikiriwa kupata kadi yako ya uanachama ila ukirudi fyata mdomo wako
Naihurumia sana chadema kwa kuwa na watu wa aina yako. Najiuliza ikiwa wewe ndie mtu ambae chama kimekuona unafaa kupewa kazi ya kukisemea chama katika mitandao ya kijamii, chama hiko kitakuwa kimepoteza mwelekeo kiasi gani.

Nyie ni watu ambao mnaharibu Chama, mnafanya chama kikose support kutoka kwa watu wa maana, ambao wakiona maandishi yenu hapa wana-conclude kuwa Chadema ni sehemu yenye watu wa hovyo ambao kazi kubwa wanaoiweza ni matusi.
 
hana fadhira kwani mlimzaa mlimlea mlimsomesha alizaliwa na mama yake alilelewa na wazazi wake na alisomeshwa na serikali tena ya ccm

Watoto wa lumumba kwa kurukia treni kwa mbele hamjambo, hako katoto unakajua vzr ww ama unaropokwa tu?
 
Katika jambo ambalo haulijui ni kuwa tupo kwenye siasa ya vyama vingi. Hivyo imehalalishwa kwa vyama vya siasa kushindana ili mbabe atakayeshinda wenzake aweze kuongoza dola.

kulalamika kuwa CCM inauangamiza upinzani, ni sawa na CCM kulalamika Upinzani Unawamaliza. Ni ujinga uliopindukia kulaumu watu ambao wanapaswa wafanye unachokilalamikia ili waendelee kuwepo na wapate mafanikio.

Kama nyie mmeridhia kuwa fedha ya ruzuku ajikopeshe babu na nyingine achukue mbowe aende picnic Dubai mnategemea nini..?

Ni ujinga kuilaumu CCM kuwa inaua Upinzani, kwani huko ndiko kuimarika kwake.
Na wewe ni mwanasiasa au unafuata tu haujui ni nini unafanya.msaliti wewe imani ya usaliti inaanza kukutana.hona sasa
 
Watu wengine bure kabisa....kutoka makamu mwenyekiti wa vijana kwa chama kikuu cha upinzani hadi kuwa mzururaji wa Chama tawala usiye na majukumu maalum ukibebwa bebwa tu ili usijisikie vibaya na uendelee kuwatukana akina Mbowe waliokulea na kufanya walau hao manyang'au wakuone ni mtu.........

Unaishi kwa ahadi sasa while ukiwa makamu mwenyekiti wa chama kikuu cha upinzani ulikuwa ukiishi ndoto zako........subiri wakati ufike akili zikukae sawa......
 
THINK TANK nadhani ni kitengo ambacho watendaji wake ni waajiriwa, kwa nini wewe usiombe hiyo kazi.

Nipo mahali salama kisiasa kuliko CHADEMA, sina haja ya kutangatanga. Nimefika sehemu ambayo mchango wangu unathaminiwa na kuheshimiwa.

Nimepokelewa kwa mikono miwili, nimefunzwa siasa na kuandaliwa njia ya mafanikio.

Naendelezwa kielimu, kwani katika siasa za Sasa watu wana-invest katika knowledge. Nyie mnatumika bure huko UFIPA huku sie tunaokwa kuwa viongozi bora wa baadae. Ni mjinga tu ambae hatjitambui ndie atatoka CCM na kujiunga na Chadema.
 
Huyu binti alipoombwa kuisaliti CHDEMA aliahidiwa kupewa ukuu wa Wilaya, usanii wa JK uliishia kumkumbatia tu, siku alipo pokelewa kwenye chama cha mizalilishaji. Julian ameusubiri ukuu wa Wilaya mpaka ameathilika Kisaikojia. Hivi sasa anahangaika kumshambulia Dr. Slaa, akifikili JK atamkumbuka, kumbe ilikuwa ahadi hewa lol.

attachment.php
 
Nipo mahali salama kisiasa kuliko CHADEMA, sina haja ya kutangatanga. Nimefika sehemu ambayo mchango wangu unathaminiwa na kuheshimiwa.

Nimepokelewa kwa mikono miwili, nimefunzwa siasa na kuandaliwa njia ya mafanikio.

Naendelezwa kielimu, kwani katika siasa za Sasa watu wana-invest katika knowledge. Nyie mnatumika bure huko UFIPA huku sie tunaokwa kuwa viongozi bora wa baadae. Ni mjinga tu ambae hatjitambui ndie atatoka CCM na kujiunga na Chadema.

Kama ukoo wa mapanya (ccm) unaweza kuwekeza kwa zero brain kama wewe, basi huko kwenye ukoo wenu wa mapanya kuna tatizo kubwa kuliko nilivyokuwa nafikiria. No wonder mwenye-chair wenu anatambulika kama "Mr. Dhaifu".
 
Naihurumia sana chadema kwa kuwa na watu wa aina yako. Najiuliza ikiwa wewe ndie mtu ambae chama kimekuona unafaa kupewa kazi ya kukisemea chama katika mitandao ya kijamii, chama hiko kitakuwa kimepoteza mwelekeo kiasi gani.

Nyie ni watu ambao mnaharibu Chama, mnafanya chama kikose support kutoka kwa watu wa maana, ambao wakiona maandishi yenu hapa wana-conclude kuwa Chadema ni sehemu yenye watu wa hovyo ambao kazi kubwa wanaoiweza ni matusi.

Hivi we, kwani wewe ndiyo unaisemea ccm kwenye mitandao?ndiyo kazi waliyokupa,wamekudharau sana, na hata hivyo bado hau-peform,bora hiyo nafasi wapewe lizabon au msalani. Sijui unakuwaga bize wapi?
 
jike dume

Naihurumia sana chadema kwa kuwa na watu wa aina yako. Najiuliza ikiwa wewe ndie mtu ambae chama kimekuona unafaa kupewa kazi ya kukisemea chama katika mitandao ya kijamii, chama hiko kitakuwa kimepoteza mwelekeo kiasi gani.

Nyie ni watu ambao mnaharibu Chama, mnafanya chama kikose support kutoka kwa watu wa maana, ambao wakiona maandishi yenu hapa wana-conclude kuwa Chadema ni sehemu yenye watu wa hovyo ambao kazi kubwa wanaoiweza ni matusi.

Cdm ingekua inakufa sI ingekua mna hanya hanya mitandaoni.ccm ndo itakufa kwa kutegemea viazi kama ww
 
Khaaa! haka kasichana tena??! Kakilala, kakiamka kanaota CDM! Sijui kaliingizwa "choo cha kike" sasa kanataka kurudi au kamekosa attention huko magambani...hata sielewi.
Wewe mtoto una jina zuri la mdogo wangu, acha porojo za kujidhalilisha. Uko CCM sasa, endelea achana na CDM. Ushauri tu.

hii ni hatari..ikiwa unashindwa hata kutofautisha kati ya porojo na hoja makini. Wewe ni mzigo katika jamii na mzigo hapa JF.
 
Haka ka binti hivi CDM mlikapaga nini? maana kakinywa maji kanawaona kwenye glass!!, hakalali bali kanawaota nyie tu - mtakuwa na dawa aisee!!

Tunaomba muitengue hiyo dawa ili sasa kaanze kufanya kazi huko kaliko, vinginevyo watakafukuza na huko iwe tatizo lingine.
Bado anakipenda Chama kwa dhati na alichokizungumza hapo ni ukweli mtupu na msipobadilika kuwasaidia viongozi kuu kukirudisha CHADEMA kwenye mstari si tu akina Mbowe watalaumiwa bali hata nyinyi WanaCHADEMA mtalaumiwa kwa kuchangia Chama kupoteza mwelekeo.Umefika wakati sasa muwaambie viongozi wenu ukweli pale wanapokosea kwasababu wao sio malaika.Kuwatetea hata kwa makosa dhahiri wanayoyafanya na ni sawa na kuwaaminisha kuwa kila walifanyalo ni sahihi hata kama lina madhara makubwa ya kisiasa kwa Chama.
 
Back
Top Bottom