Uhakika Bro
JF-Expert Member
- Mar 29, 2022
- 2,703
- 3,228
Unataka kuwa na akili?
Tena kimsingi sio kutaka kuwa na akili, bali ni je? Unataka kuzitumia akili ambazo tayari unazo?
Na je Unataka mwanao aweze kutumia akili alizojaaliwa kwa kuzaliwa tu akiwa Homo sapiens a wise humanoid?
Je unataka awe mwenye uwezo wa kujifunza?
Ni kweli matumizi akili ya mtu hutegemea baiolojia na mazingira anayokulia. Lakini chukulia kwamba kibaiolojia wooote tumezaliwa na Homo sapiens hivyo akili tayari tunazo kwa urithi wa ubinadamu wetu.
Kinachobaki kututofautisha ni kiwango cha matumizi kitakachotegemea saana mazingira ya mtoto na mtoto, mtu na mtu.
Kuna vitu unaweza kuviandaa ili kumfanya mwanao atumie akili yake zaidi ikisaidiwa na hisia, machale sijui bahati. Vyote atatumia lakini akili ndio itawale maisha yake.
Can you inspire your childs inner genius?
Katika kupima ukweli wa jambo na ushikamanifu wake tunaweza kutumia vijiukweli vilivyokwisha kuaminika tayari (well established facts)
Kanuni ni moja tu visipingane. Na hata visipopingana sio lazima vikubaliane, bali yatosha tu hata vioane.
Kuna kauli mbili au tatu ninazozifahamu kuhusiana na akili; moja inasema 'wasiwasi ndo akili'; na kuna kauli ya pili inasema 'kuuliza si ujinga'. Ya tatu yenyewe ni ya kisukuma inasema 'masala kulangwa'
Tukizichambua zaidi kauli hizi kwa upande wa wasiwasi. Wasiwasi imekaribiana zaidi na hofu kuliko akili. Imekaribiana zaidi na hisia na silika kuliko hekima. Hivyo basi kama utamlea mtoto katika misingi ya awe na wasiwasi (aogope) vitu fulani basi jua unamtengeneza mwanadamu wa chini zaidi (kama mu Homo erectus tu) atakayetumia silika na hofu kuyakimbia mambo mabaya ili asipotezwe maisha (survival). Hii ni kwa wazazi wenye imani ya wasiwasi ndio akili. Huwezi pata jiniazi hapo, hawapo 'smart' hata wao wenyewe.
Kauli ya pili ambayo nayo sijaipenda sana, hapana nimeipenda nusu ( kikamilifu baada ya kuiweka sawa) ni hii; KUULIZA SI UJINGA.
Sijataka kuifafanua kabla sijairekebisha maana ipo hasi sana. Basi tuweke kisawe na kinyume cha neno moja ili tupate kauli ilonyooka zaidi:
Udadisi ni kisawe cha kuuliza na akili ni kinyume cha huo ujinga. Hivyo badala ya kusema 'kuuliza si ujinga' tutasema 'udadisi ndo akili'
Katika kuishi kwangu nimegundua kuwa 'vitu' hivi vitatu mtu huwa havimiliki kama tunavyomiliki nyumba au kompyuta. Maana kiukweli hizi ni hali na sio vitu 'per se';
Utajiri
Akili na
Afya
Tunasema mtu mwenye afya, lakini kumbe kiukweli ni yule mtu ambaye kila siku anafanya mambo ya kuitafuta afya. Atafanya mazoezi, atakula vizuri, usafi na atapumzisha mwili wake. Kila siku anaijenga afya yake na ndio anakuwa mwenye afya🤔. Siku anapoacha kujijenga kiafya ndipo anapogonjeka.
Tunasema mtu mwenye utajiri na kumbe utajiri ni ile hali endelevu ya kutafuta na kuwekeza kwenye mali. Siku anapoacha kutafuta (hata 'passively') ndipo anapofilisika!!
Basi ndugu zangu hata akili nayo ni hivyohivyo. Mtu anayeitwa ni mwenye akili kiulweli sio kwamba tu basi kiajabu amekuwa na vitu/'materials' vingi kichwani. La. Ukweli ni kwamba ni tabia yake ya kila siku kujifunza vitu mbalimbali. Karibu kila uzoefu anaopitia maishani anautumia kujifunza. Muda mwingine anajifunza hadi vitu vya ziada kabisa. Na mwishowe anaweza kuunganisha funzo la hapa na la pale na akapata kitu kipya kabisa!. Udadisi, huo utafutaji wa maarifa ndio akili yenyewe. Mmeelewa sasa?
Huu ndio uzoefu wangu mimi na haya ni majibu ya swali linaloulizwa. Kwamba mtu anafanyeje hadi anakuwa na akili? Jibu ni sawa katika kipengele cha afya na hata kile cha utajiri.
Kwa wazazi wenye watoto angalizo;
Udadisi unapatikana penye utulivu
Udadisi unapatikana penye amani
Udadisi unasisimuliwa na vitu asili vya kuvutia na kushangaza.
Peleka mtoto kwenye shule yenye mazingira mazuri. Watoto wa mashuleni wafanye tour zitakazosisimua udadisi iwe ni kwa wanyama, au viwandani huko. Viwandani iwe ni kwa ajili ya kukata kiu ya udadisi wa 'hivi gari zinaundwaje?', mabati na nondo au karatasi zinaundwaje? Sio tu za twende kiwanda cha soda na mikate kunywa soda. Ujinga huu ukome. Mtoto aende kujibu swali la hivi soda na mikate vinatengenezwaje. Waalimu mnaweza kuileverage hii penda tamtamu ya watoto ili kuwaongeza udadisi. Mfano unanunua vifaa wanaenda kiwandani kujifunza recipe halafu mnakuja darasani mnatengeneza keki, mikate na soda mnakunywa wote.
Tengeneza mazingira ya mtoto kuona maua na wadudu mbalimbali, wanyama eeh! Kiufupi tengeneza ka 'Edeni' nyumbani kwako.
Badili 'approach' ya ukali na mafokeo kuwa uthabiti na maelekezo. Ukali unasisimua uoga tu unazalisha li Homo erectus. Lakini pia maelekezo yanazalisha skilled workers tu unazalisha li Homo habils. Ili uzalishe ka jiniazi kenye hekima hebu karuhusu kajaribu, kabebe majukumu na katatue matatizo madogomadogo ukisaidia knowledge za hapa na pale. Kakiweza kuharmonize knowledge unayokapatia hapo umepata a leader, a thinking man a Homo sapiens indeed.
Kiufupi mazingira yawe ni yanayomruhusu mtoto mwenyewe kujifunza maana msemo wa tatu unaojazia na kufunga ni 'Masala Kulangwa' yaani akili ni kufundishwa/kujifunza zaidi na zaidi.
Nb: mniwie radhi nimeandikaa mwisho nikachoka sikuwa na muda tena wa kuiperfect lugha. Pambaneni tumieni akili zenu maana mnazo tele