Hivi ni kweli Palestina hawana Jeshi?

hivi mkuu hamas wapo chini ya iran ama syria maana drone na baadhi ya silaha zao zina fanana na za iran
hamas ni wasuni so hawaezi iva kabisa na iran...na ndio tatizo la waarabu linaanzia hapo...usuni na ushia...na hyo ndio silaha israel anayotumia kuwachapia
 
Sasa kwanini hao Hamas wasitanuke hadi huko Westbank wakati ni Palestina yote?
Hawawezi, katikati ya West Bank na Gaza kuna Israel
Hata hao Hamas wakifanikiwa kufika West Bank wasingeruhusiwa kufanya jambo lolote la kijeshi kwani West Bank imedhibitiwa vikali na jeshi la Israel
 
Po
Yes!

Ni Mungu aliwapa kwa sababu waliopewa kihalali waliikataa nchi na walipinga kumtumikia Mungu. Wakamhasi Mungu! Wakafanya ibada za sanamu.

Sasa Mungu afanyeje?
na onyo aliwapa hao waliomuhasi kuwa namnukuu

"Mkinihasi nitanyanyua hata mawe yaniabudu" ndo hao walionyanyuliwa na Mungu na kweli sehemu zote za kumbukumbu ya Mungu zimetunzwa mpaka leo toka Yesu anazaliwa.
Mipalestina ilikosea kuleta uislamu tuuu! Ikasahau sehemu nyeti km hizi za bethlehemu!
Ivo msiwaonee wivu babu zenu walishindwa vibaya kumtii Mungu ndo maana mnalia leo na mtalia sana!! Cha moto mtakiona

Mungu Alisema hamtarudi tena pale kwa nchi ya asali na maziwa kabla hajakuja. Aliwapa mkashiba mkamnyea!
Akawatupa utumwani mpaka leo mlio wengi hamjitambui. Nyie ni nani!!! Mnaamini mmetokana na nyani. Na bado!!!

Sisi tunaojua kidogo Mungu ametupa wepesi na unafuu wa maisha km hivi make tumesha jua na kutubu walio fanya babu zetu. tatizo ni nyie milipuko!
Pole sana na chuki zako, kwani ukristo alianzia wapi?
 
Hellow,

Wakuu naomba kujuzwa kuhusu habari hii tajwa hapo juu ama kama kuna threads ilishawai kuzungumzia Palestina pamoja army power yake tafadhali.

Kuna mahala nilisikia kwamba Palestina hawana Jeshi zaidi ya Jeshi la Polisi pamoja na intelligence na kitengo cha kumlinda Rais.

Wajuzi wa Mambo naomba mtiririke

Karibuni
Wana jeshi maarufu la kigaidi
 
Palestina si NCHI.....

Palestine haiwezi kuwa na JESHI RASMI LA KINCHI.....

Ila kuna vikundi vibebavyo silaha....kimoja wapo kikiwa HAMAS.....

Halafu kisichojulikana na wengi ni kuwa WAPALESTINA SI WAARABU....62% ya damu yao ni walevante!!!

Mwisho kabisa Palestina si NCHI na haijawahi kuwa NCHI na kustahili kuwa na JESHI RASMI.....
 
Kwanza kabisa lazma ujue kuwa kwa sasa palestina siyo nchi, bali ndiyo inapigania kwenye umoja wa mataifa ili ipewe title ama kutambuliwa kama nchi

Ndiyo maana kwa sasa huitwa "Mamlaka ya palestina" na siyo "nchi ya palestina".

Nchi yao walishanyang'anywa na wayahudi (Israel) tangu tar 14 mwezi May mwaka 1948 (siku ambayo israel ilijitangazia uhuru wao kam taifa rasmi).

Kwa hiyo, kwa sasa jeshi rasmi yaani (national army) hakuna.

Ila tu kuna kikundi cha wapiganaji cha "Hamasi" ndo hutumika kama jeshi la palestina ambapo kikundi hcho cha wapalestina cha hamasi hutazamwa na israel kama kundi la kigaidi maana huwalenga wayahudi.
Sasa mbona mataifa makubwa kama marekani huunga mkono na kushirikiana kijeshi na Israel kuihujumu Palestina ambayo mnadai hawana jesh ni kikundi kiduchu tu cha hamas walichonacho?
 
Nafikiri ukifanya tafti vizuri ukajua taifa la Israeli lilianzishwaje mwaka 1948 wala usingeniuliza swali kama hili.

Ila anyway ngoja nikusaidie tu kwa haraka iko hivi : Israel ni Adui wa nchi zote za kiarabu na siyo tu nchi za kiarabu niseme nchi zote za kiislamu hazipatani na Israel,na hii ni kwa sababu Wanaichukulia Israel ni kama Dola vamizi ambalo limekuja kuwavamia wapalestina na kuwanyang'anya nchi yao na kuanza kuwatesa/kuwaonea.

Na nyuma ya uvamizi huo hadi Likaanzishwa taifa la Israel la sasa (mwaka 1948) kulikuwa na sapoti kutoka USA(Marekani) na Uwingereza (Great Britain).
Ndiyo maana mpaka leo Marekani yupo karibu sana na Wayahudi kwa sababu ni mshirika wake muhimu sana na wanasaidiana kwa mambo mengi sana.

NB : Israel ina teknolojia ya juu sana kijeshi kiasi kwamba hakuna nchi yeyote ya mashariki ya kati inaweza kuivamia kirahisi, we hujawahi hata kujiuliza kwanini Magaidi hawawezagi kuishambulia Israel wakati wanafanyaga mashambulizi kwenye nchi kama marekani, ufaransa hata uwingireza ila ni nadra sana kuskia Israel imevamiwa na Magaidi, You know Why ?

Na kingine kumbuka tu kwamba huu mgogoro pia upo kidini zaidi, kwa hiyo mara nyingi unakuta nchi nyingi za kikristo zinaisapoti Israel na zile za Kiislam na kikomunisti zina isapoti palestina, kwa hiyo ndo maana unaona hata Mgogoro huo hauishi kirahisi ni vita kila kukicha tangu 1948 ilipoanzishwa Israel ni vita tu mpaka sasa, wanachofanya huwa wanapumzika tu wakila wakishiba wanarudi tena vitani.
 
Mimi suala langu ni tokea 1948 Palestine wanashambuliana na dola vamizi la Israel likiungwa mkono ni Marekani kwa sababu ya ushirika wao wa Kanisa (kidini) kama ulivyoeleza, hii miaka ni mingi sana kupigana na mataifa hayo hayo uliyoyataja yenye nguvu (Great Britain) inawazekanaje Palestine kuwa hawana jeshi bali ni kikundi kiduchu tu cha Hamas kuwa mpaka leo Palestina iko hai? Nguvu ya Palestine iko wapi kuweza kuhimili vita hiyo tokea miaka hiyo mpaka sasa kuwa bado wapo?
 
Mkuu kwenye "kuhasi" una maanisha kile kitendo cha kuzihujumu korodani za mnyama? Kama ndivyo hao unaowaongelea waliwezaje kumuhasi mungu! Naye anakuwaga nazo?
chanya na Hasi unazijua WEYE?

Ebu nipe maana ya HAMAS ili nikujibu
 
Mimi suala langu ni tokea 1948 Palestine wanashambuliana na dola vamizi la Israel likiungwa mkono ni Marekani kwa sababu ya ushirika wao wa Kanisa (kidini) kama ulivyoeleza, hii miaka ni mingi sana kupigana na mataifa hayo hayo uliyoyataja yenye nguvu (Great Britain) inawazekanaje Palestine kuwa hawana jeshi bali ni kikundi kiduchu tu cha Hamas kuwa mpaka leo Palestina iko hai? Nguvu ya Palestine iko wapi kuweza kuhimili vita hiyo tokea miaka hiyo mpaka sasa kuwa bado wapo?

😁😁😁 Kwanza naomba nikusahihishe naona kuna mahali hujanielewa vizuri.

Sijasema marekani inaisadia Israel kwa sababu za kidini hapana, bali nimesema marekani inamsaidia muyahudi (Israel) kwa sababu ni mshirika wake kwenye mambo mengi tu ila sija-specify kuwa ni dini.

Israel ni mshirika muhimu sana kwa marekani hasa kwenye masuala ya teknolojia Marekani inamtegemea sana muyahudi kwa kiasi kikubwa.

Trust me kuna uwezekano mkubwa hata uchumi wa marekani usingekuwa hapo ulipo bila wayahudi,inawezekana kabisa marekani isingekuwa kuwa super power of the world bila wayahudi.

Hawa watu (wayahudi) ni watu wenye bahati sana ya kuzaliwa na akili automatically (siyo za kuzipata kwa kwenda darasani) ndiyo maana wanasumbua sana dunia hawa watu.

So kwenye suala la dini nimekuja ku-generalize mwishoni kwamba mara nyingi Mataifa ya kikristo yamekuwa yakiiunga mkono Israel kwenye huo mgogoro na vilele Mataifa ya Kiislam yamekuwa yakiiunga mkono palestina kwenye huo mgogoro, ila sija-specify kwamba Marekani na uwingereza zinaisadia Israel kwa sababu za kidini kama ulivyonielewa hapo mwanzo.

Kingine umesema imekuwaje tangu mwaka 1948 israel ikipewa sapoti na Marekani na uwingereza wanapigana na palestina mpaka leo wakati palestina haina jeshi.

Kwanza inabidi unielewe kwamba tangu 1948 mpaka leo kumekuwa na mlolongo wa vita kadhaa (zikiwa zimetaja majina yake) kati ya Israel na palestina, na katika vita hizo karibu vita zote Israel imekuwa ikishinda.

Kwa hiyo kusema palestina ni nani tangu 1948 mpaka leo bado inapigana na mataifa makubwa si kweli kwa sababu Palestina imeshindwa karibu mlolongo wa vita zote ndiyo maana unaona kuna maeneo kibao ya wapalestina yanaporwa na wayahudi karibu kila vita wanayopigana, na siyo tu maeneo ya palestina, kuna maeneo mengine Israel imepora kutoka Syria, misri, Jordan na Lebanon na mpaka leo yako chini ya Israel.

Kwa hiyo Tangu 1948 mpaka sasa Palestina imepoteza maeneo yake mengi sana kwa wayahudi kwa sababu ya kushindwa vita na ndiyo maana unaona hata mwaka juzi hapa hata Ile Jeresalem mashariki ambayo ilikuwa chini ya Wapalestina saivi imetekwa yote imekuwa chini ya Israel hadi ule msikiti wa Alqsa (Quds tukufu) ambayo ni mojawapo ya misikiti mitakatifu sana kwenye dini ya kiislam.

Na kitu kingine ambacho hukunielewa ni kwamba Israel haipigani tu na palestina bali inapigana na nchi zote za kiarabu ambazo zinapinga uwepo wake mashariki ya kati na wala si palestina tu, palestina haina nguvu yeyote ndiyo maana inapewa sapoti na washirika wake wa kiarabu ambao nao wameshindwa pia na wameanza kusalim amri mmoja mmoja kwa Israel, mfano unaweza kuona sasahivi Misri, United Arab Emirates,Behrain, Saudia Arabia na Uturuki zote zimefunguaga balozi zao Kule Tel-Aviv wameamua tu wawe na uhusiano na Israel ingawa waarabu wenzao wanaona kama ni usaliti.

NB : Ninaposema Israel inapewa sapoti na Marekani na Uwingereza, simaanishi kuwa kuna wanajeshi wa marekani ama uwingereza wanachukuliwa wanapelekwa kwenye uwanjwa vita kuwasaidia hapana, ni kwamba tu msaada kama kifedha, silaha na mengine ya kijeshi kama yatahitajika ila siyo Active personel anapelekwa pale kwenda kupigana, na Hivyo hivyo kwa Upande wa palestina wanapewa msaada wa silaha hasa na Irani (maana huyu ndiye mtetezi halisi wa wapestina aliyebaki wengine wote wanafiki tu, mfano Saudia Arabia ni mnafiki namba moja wa waarabu na kibaraka wa marekani yule).

Na kumbuka tu kuwa historically; Israel na palestina ni ndugu (Wote walitokana na uzao wa mzee Ibrahim wa kwenye Biblia ambao ni Isaka na Ismael ) kwa hiyo ni ndugu ambao vita yao pia imesemwa kwenye vitabu vya dini kana kwamba haitaisha hadi kiama.
 
Nimekuelewa umetiririka vizuri sana mara hii lakini ngoja nende deep zaidi nithibitishe hichi ulichokiandika.,
 
Good, jaribu kuchimba na wewe ili usijelishwa matango pori maana kila mtu anaandika lake humu kwa stori tu anazosikia kwenye vijiwe vya kahawa
 
hamas ni wasuni so hawaezi iva kabisa na iran...na ndio tatizo la waarabu linaanzia hapo...usuni na ushia...na hyo ndio silaha israel anayotumia kuwachapia
mkuu koseme vizuri maana hamas na iran ni pete na kidole drone zote za hamas ni made in iran kiongozi wa hamas alikuwepo kwenye mazishi solueiman
 
Uko sahihi.

Iran inaunga mkono makundi yote duniani yanayopinga uwepo wa Israel Mashariki ya kati.

Mojawapo ya makundi hayo ni Hezbollah la Lebanon ambalo walipigana vita Israel mwaka 2006, vita ilichukua mwezi mmoja ila viliitoa Jasho Israel maana walishangaa makombora ambayo Hezbollah walikunayo yalikuwa yanaweza kufika hadi Tel-Aviv na yote yalikuwa MADE IN IRAN.

Ndiyo maana kwa sasa Israel inaitazama Iran kama Adui yake namba moja Duniani maana Iran inatishia uwepo wa Israel Middle East.
 
Wakiruhisiwa kununua hata vifaru ishirini na ndege mbili tu Israel haitapumua sembuse wawe na jeshi.
Vifaru ishirini na ndege mbili??? 🤔🤔🤔Hivi unaikumbuka ile vita ya siku tatu, nchi tatu, ya Israel, walivyoliza wanaume, sasa vifaru ishirini na ndege mbili, si ukwaju huo, yaani hapo haiwezekani kufanya lolote, itakuwa wame 'scratch' tu. Vita si vizuri mjue
 
Vifaru ishirini na ndege mbili??? 🤔🤔🤔Hivi unaikumbuka ile vita ya siku tatu ya Israel, walivyoliza wanaume, sasa vifaru ishirini na ndege mbili, si ukwaju huo, yaani hapo haiwezekani kufanya lolote, itakuwa wame 'scratch' tu. Vita si vizuri mjue
Hahaaa😅
 
Back
Top Bottom