Ndugu zangu nimekutana na msemo huu mitaani kuwa hata mtu asiyesoma ulaya ana uwezo mkubwa kuliko hata profesa wa afrika.
Mzungumzaji anasema eti sababu ni mazingira ndio humshepu mtu na akadai kwa afrika mazingira yaliyojengwa hata wataalamu wanaacha utaalamu na kufanya ujinga lakini akadai kwa ulaya kwa mazingira waliyojijengea wajinga wabadilishwa na mifumo yao na kuelekea kwenye kujua.
Mwanzoni nilitaka kumpiga kibao kwa msemo huu lakini baada ya utangulizi huo nikahisi sijaelewa nikamuambia hebu fafanua tena.
Akaniambia ndugu yangu kwa afrika mifumo iliyotengenezwa sheria hazifanyi kazi, moral value hazifanyi na haya hubeba sana taaluma na kama hivyo vitu havifanyi kazi basi taaluma inakuwa mashakani lakini kule ambako sheria na moral value vinafanya kazi basi hata yule asiye na taaluma analazimika kufuata taaluma zinasemaje.
Nikamuuliza sasa kama mtu hana taaluma unataka kuniambia atafuataje taaluma?Akaniambia hoja ni sheria inasemaje na kama mtu anagundua sheria inachokitaka hakijui basi huwauliza wanaojua nini cha kufanya.
Akaniambia unajua tatizo la afrika wanataka malipo bila kazi nikamuuliza unamaanisha nini?Akanijibu waafrika ukiwaambia ukweli kama huu wanakasirika na wanataka useme tofauti na kile wanachokifanya kwa maana wao wanadhani wasifiwe kwanza ndio wataachana na upuuzii na sio kurekebisha mifumo yao ikawaelekeza kufuata utaalamu na wakafanya vizuri ndio watasifika kwa yale waliyoyafanya.
Nikamuuliza inamaana unadhani waafrika hawafanyi lolote?
Akasema hoja sio hawafanyi lolote bali wanachokifanya kina value gani?
Akasema wakati afrika inapoteza rasilimali kupitia rushwa, na uozo wa serikali zao bado wanaandika papers kwenda kudai wao hawawezi kuendelea bila kupewa misaada.
Akaniambia ni aibu kwa wataalamu wa afrika kuburuzwa na wapumbavu kufuata upumbavu badala ya wataalamu kuwabadilisha wapumbavu kufuata utaalamu.
Watu weupe hawana akili kuliko weusi. Ukiangalia historia, watu weusi walistaarabika kwanza kabla ya weupe (westerners / Caucasians). Ustaarabu na dominance ya westerners umetokea kwa wagiriki --> Warumi --> Renaissance --> British Empire --> U.S.A/ E.U
Ukiangalia Wagiriki walipata mengi sana kutoka Egypt na the crescent region.
Ukiangalia Egypt yenyewe ilipata ujstaarabu wake kutoka kusini zaidi.
Majibu ya maswali yako yote yapo katika mazingira zaidi kuliko akili. Ukitaka maelezo zaidi nitakufafanulia..
Wakati Wagiriki walipokuwa wanachochea open discussion na innovation, wa Egypt walikuwa wanachochea elitism na secret societies.
Kuna watu kama kina Imhotep, Hesy-Ra na Merit-Ptah wa Egypt ya kale waliogundua mengi wakati weupe wanaishi kwenye mapango. Kina Pythagoras na Erasthothenes walikuja kujifunza Egypt. Eratosthenes aliweza kuupima mzingo wa dunia katika kisima kilicho Syene katika Tropic of Cancer, tatizo la vumbuzi nyingi zinazosemwa kuwa ni za Wagiriki leo, originally zilikuwa za wa Egyptians ila system yao ya secret societies haikuruhusu publishing so to speak, kwa hiyo Wagiriki wakawa wanakuja kuchukua ujiko kirahisi tu.
Huu ndio ulikuwa mwanzo wa decline ya Africa na rise of the west.
Inakuwaje pale ambapo mko darasani na Wazungu na katika mitihani unawatupa mkono Wazungu walio wengi katika matokeo? Sidhani kama hivyo vigezo ulivyotumia (kututawala, kuwa na maendeleo kuliko sisi na hili la uvumbuzi si kweli kuna weusi wengi tu waliofanya uvumbuzi mbali mbali muhimu hapa duniani ambao umesaidia katika maendeleo ya nchi za Wazungu) Hivyo kuhitimisha kwamba Wazungu wana akili sana kuliko weusi si sawa hata kidogo.
Bubu, sidhani kama kutumia akili za darasani kama kigezo ni sawa kwa sababu hilo limeshakuwa debunked siku nyingi sana. Lakini pia hata tukitumia mambo ya shule na darasani, utakuta mengi hasa yale ya kisayansi unayoyasoma, unakutana na wazungu wengi tu walioshiriki kwa kiasi kikubwa kuendeleza fani flani. Uongo? Nitajie fani ya kisayansi ambayo haina lizungu hata limoja...
Sikubaliani kwa sababu wako weusi wengi pia wameshiriki katika kuvumbua mambo mbali mbali ambayo yana umuhimu mkubwa hapa duniani.
Si kweli. Tatizo la sisi weusi ni kukosa au kutopata opportunities za kuonyesha akili zetu kwetu au nje.
Tukipewa chance huwa tunaonyesha akili zetu...fikiria sisi tulio wengi tumejifunza kuongea na kuandika lugha zao..wao ni wachache sana ambao wanaweza kuongea lugha zetu!!
Mkuu hapo kwenye nyekundu inamaanisha kua sisi tunajifunza lugha za kwa sababu tunatafuta oppotunities....sasa wao wajifunze za ketu kwashida ipi? labda ka anataka kuja kukaa kwa muda then ndo aajifunza!Si kweli. Tatizo la sisi weusi ni kukosa au kutopata opportunities za kuonyesha akili zetu kwetu au nje. Tukipewa chance huwa tunaonyesha akili zetu...fikiria sisi tulio wengi tumejifunza kuongea na kuandika lugha zao..wao ni wachache sana ambao wanaweza kuongea lugha zetu!! Pia, mazingira tunayosemea sisi ni magumu kulinganisha na hawa wenzetu.
Mimi naona jinsi ya kulinganisha hili ni kuweka wote kwenye mazingira na oppurtunities sawa.
anamaanisha na hao waliotuzidi Akili...teh teh tehNani katukosesha hizo "opportunities" ?
Tukipewa "chance" na nani?
Je ni kweli kwamba whites wanaakili kuliko sisi (blacks).
Sasa kwa nini nchi nyingi za weusi au sehemu nyingi za weusi kote hapa duniani ziko nyuma sana kimaendeleo kulinganisha na sehemu za wazungu? Chukulia kwa mfano Haiti ni nchi ambayo ilianzishwa na weusi waliokuwa utumwani. Lakini angalia maisha yao. Sasa hebu linganisha Haiti na New Zealand kwa mfano, nchi kisiwa iliyoanzishwa na wahamiaji wengi wa kutoka Uingereza na sehemu zingine za ulaya. Mbona wao wameendelea zaidi...
Opportunity upewe na nani?Si kweli. Tatizo la sisi weusi ni kukosa au kutopata opportunities za kuonyesha akili zetu kwetu au nje. Tukipewa chance huwa tunaonyesha akili zetu...fikiria sisi tulio wengi tumejifunza kuongea na kuandika lugha zao..wao ni wachache sana ambao wanaweza kuongea lugha zetu!! Pia, mazingira tunayosemea sisi ni magumu kulinganisha na hawa wenzetu.
Mimi naona jinsi ya kulinganisha hili ni kuweka wote kwenye mazingira na oppurtunities sawa.
Hili hatuwezi kulithibisha kwa sababu sisi tunaenda na kile tunachokisoma tu kwenye mavitabu ya historia. Na historia huandikwa kwa mtazamo wa yule anayeiandika. Kwa hiyo kama huyo mwandishi wa historia anatudanganya, sisi hatuwezi kujua wala kuthibitisha kwa namna moja ama ingine ya kile alichokiandika.
Tunarudi kulekule kwenye historia. Unless wewe ulikuwepo na kushuhudia yote hayo, huwezi kulijua hilo kwa uhakika.
Tunarudi kule kule.
Naomba ufafanuzi tafadhali. Mazingira yepi hayo unayoyazungumzia bwana Kiranga.
Huko Egypt wakati huo walikuwa wanaishi watu gani?
Hao Wagiriki walifikaje huko Egypt? Walitembea? au walikuwa na vyombo vya usafiri?
Duh! Basi kama ni hivyo Afrika imekuwa kwenye decline muda mrefu sana. Kwa nini lakini? Au labda Waafrika wa wakati huo walikuwa na akili zaidi kupita Waafrika wa waliowafuatia?
Mkuu hapo kwenye nyekundu inamaanisha kua sisi tunajifunza lugha za kwa sababu tunatafuta oppotunities....sasa wao wajifunze za ketu kwashida ipi? labda ka anataka kuja kukaa kwa muda then ndo aajifunza!
Mi naamini utamaduni unachangia kwa kiasi kikubwa kuto kuendelea kuliko akili. Tamaduni zetu za kiafrika zina tabia ya kurithika sana na mazigira kuliko kutafuta njia ya kuboresha maisha.