Hivi ni kweli kuna watu 400 wameuawa mkoa wa Lindi kama Tundu Lissu anavyotangaza huko Marekani?

Ameulizwa ataenda the heague akasema kesi hiyo haiendi the heague kisheria, wakati kesi ya uhalifu dhidi ya binadamu zinasikilizwa the heague. Ndo mjue lisu shida yake sio haki za binadam bali urais tu

Sent using Jamii Forums mobile app
kwani Tanzania kuna watu wameandaliwa kuwa marais na waliondaliwa kuwa washangiliaji tu? Je ikiwa rais hawezi hawezi kuleta hicho unachotaka akifate the Hague?
 
Lissu mpayukaji sasa amegeuka kibaraka wa watetezi wa mashoka na mabeberu. Habari za kuaminika mapokezi yake marekani yamepooza sana wenyeji wake wamegundua ni mtu mjinga hawezi kua na faida kubwa kwao. Anatoa taarifa za uongo wa kijinga na ana chuki na kisasi kwa jpm wakati hana ushahidi nani aliyemtwanga risasi mambo ambayo hayana msaada kwa hao mabeberu na wapenzi wa ushoga.
Watanzania ni watu wanaopenda amani kwa hivyo tunamsihi lissu arudi atulie nyumbani kama ni urais atausikia tu kwenye bomba maana hana sifa ya kua rais wa tanzania.
Hivi bila kuwa na akili za kiccm unaweza kumuuliza au kutegemea kuwa Lissu atatoa ushahidi wa waliompiga risasi?Mimi nilidhani ushahidi unapatika kwa kufanya upelelezi either kwa kutumia jeshi la police au private investigators
 
Lakini katika moja ya maongezi yake na watanzania huko Marekani Mhe Tundu Lissu amekuwa akirudia mara kwa mara kuwa kuna watu wasiopungua 400 wameuwawa au kupotea huko mkoa wa Lindi na watu hao wameuwawa na serikali yetu.
Lissu ameshakua kituko,huwezi kuropa mbele ya watu wenye akili kuwa kuna watu 400 wameuawa na serikali,ukiwa huna jina hata moja la marehemu
Lissu huyo huyo kawaambia wamarekani eti kuna masheikh 200,wamefungwa kwa ugaidi,kasahau kua kitengo cha kuzuia ugaidi marekani kinawajua watuhumiwa wote hao na majina yao
 
Tundu Lissu Mbunge wa Singida Mashariki amekuwa kwenye ziara isiyo rasmi huko Marekani akitokea nchini Ubeligiji ambako ndiko anakopata matibabu baada ya kutoka Nairobi nchini Kenya baada ya kupigwa risasi Dodoma atrehe 7 September 2017.

Akiwa Marekani kwenye majimbo taofauti akiongea na watanzania waishio huko yaani Diaspora amekuwa akielezea tukio lake la kupigwa risasi na namna Bunge lilivyoshughulikia tatizo hilo pasipo kummpa msaada wowote ingawa Bunge nalo limekuwa litoa taarifa kuhusu utaratibu wa wabunge kutibiwa ambapo Lissu hakufuata utaribu huo.

Lakini katika moja ya maongezi yake na watanzania huko Marekani Mhe Tundu Lissu amekuwa akirudia mara kwa mara kuwa kuna watu wasiopungua 400 wameuwawa au kupotea huko mkoa wa Lindi na watu hao wameuwawa na serikali yetu.

Kiukweli kama namba 400 ya watu wameuwawa au kupota ni idadi kubwa sana kiasi kwamba jamii ya huko Lindi tungeona hayo malalamiko hadharani kabisa lakini sijawahi kusikia suala hilo kabisa kwenye tv zetu redio zetu hata magazeti yetu hata ushahidi wake wa tukio hilo.

Lakini Lissu ndiyo moja ya ujumbe ambao anaeneza huko Magharibi je RPC wa Lindi amelisia hilo?

Maswali:

  1. Kunataarifa yoyote iliyopo Polisi kwa maana ndugu kuripoti Polisi kuhusu kupotea kwa idadi hiyo ya watu huko Lindi?
  2. Vyombo vya habari vimehai kuwahoji ndugu waliopotewa na ndugu zao huko Lindi kwa ushahidi?
  3. Je kuna yoyote yule huko Lindi mwenye kujua hata mmoja yoyote yule aliyeuwawa au kupotea?
  4. Viongozi wa Dini huko Lindi wamewahi kupokea taarifa yoyote ya familia zilizopotelewa na ndugu zao ktk kufanya maombi au dua?
  5. Kuna taasisi yoyote hasa hizi za haki za binadamu na ustawi wa jamii imewahi kufanya utafiti mdogo wa taarifa kama hiyo ya watu 400 kupota au kuuwawa?
  6. Kuna yoyote yule aliyewahi kuona hata maiti za hao watu au makaburi ya hao watu kuthibitisha hilo?
Mkuu usihangaike na huyo mgonjwa akili bado hazijakaa sawasawa huyo! Anayeweza kumwamini huyo mgonjwa atakuwa naye ni mgonjwa! Watu 400 kuuwawa siyo mchezo dunia nzima ingekuwa inapiga kelele. Nafikiri amewaona hao anaowahutubia ni wajinga wasiojuwa kufuatilia mambo. Ndiyo maana mtangazaji wa BBC Hard Talk alipoona anamuaibia palepale kwa kumwambia aache inflammatory allehations.
 
Mleta mada mwenye mashaka angalia video hii ya mbunge bungeni akilalamika uonevu jimboni kwake katika operesheni pana inayohusiana na MKIRU mikoa ya kusini:

Nadhani labda ana refers ile ya Operation MKIRU ile ya akina Azory....!!

Je uliwahi kusikia taarifa yeyote ya polisi kuhusu ile operation MKIRU? IGP Sirro alisema tu kuwa alimaliza kazi na hakuelezea zaidi ya hapo!!! Katika operation kama ile hudhani kuwa kulikuwa na wahanga? Kwanini polisi haikutoa teport ya operation?
 
Hivi bila kuwa na akili za kiccm unaweza kumuuliza au kutegemea kuwa Lissu atatoa ushahidi wa waliompiga risasi?Mimi nilidhani ushahidi unapatika kwa kufanya upelelezi either kwa kutumia jeshi la police au private investigators
Mkuu,
nchi hii viongozi aanaamini wananchi hawana akili na kwamba hawatakiwi kuhoji kazi yao ni kulipa kodi tu na kupelekwa kama ng'ombe..

Serikali inasema matukio ya mauaji yanafanywa na "wasiojulikana" maana yake ni kwamba wameshindwa kuwajua,
Wakiambiwa wasaidiwe kufanya upelelezi na vyombo vya nje wanasema hapana tunaweza kufanya wenyewe..hii hofu inatoka wapi? Why?

Mbona matukio mengine huko nyuma walisaidiwa upelelezi kwanini sasa wanakataa?
Kuna nini wanaficha?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Leta majina acha hizo inflammatory allegations!

Kwa mujibu wa mheshimiwa Bungala , mmoja wa waliouawa ni Ismaili Bweta aliyeuawa katika msikiti huko chumo, na mwengine kutobolewa jicho, na aliyetobolewa jicho alimbeba hadi kwa waziri mkuu kumuonyesha kiwango cha attrocity walichokifanya polisi huko, waziri mkuu alilia machozi alipoona na kuambiwa yaliyojiri , unaweza kumsikiliza katika hii video ifuatayo kuanzia dakika ya 7:45

Nakuelewa sana mkuu.Lakini haya yote tumeyataka sisi wenyewe .tukiamua kusema hapana huu ujinga utaisha kabisa na serikali zote zitakazofuata zitakuwa na adabu kwa walipa kodi
Mkuu,
nchi hii viongozi aanaamini wananchi hawana akili na kwamba hawatakiwi kuhoji kazi yao ni kulipa kodi tu na kupelekwa kama ng'ombe..

Serikali inasema matukio ya mauaji yanafanywa na "wasiojulikana" maana yake ni kwamba wameshindwa kuwajua,
Wakiambiwa wasaidiwe kufanya upelelezi na vyombo vya nje wanasema hapana tunaweza kufanya wenyewe..hii hofu inatoka wapi? Why?

Mbona matukio mengine huko nyuma walisaidiwa upelelezi kwanini sasa wanakataa?
Kuna nini wanaficha?

Sent using Jamii Forums mobile app[/QUOTl
 
Tundu Lissu Mbunge wa Singida Mashariki amekuwa kwenye ziara isiyo rasmi huko Marekani akitokea nchini Ubeligiji ambako ndiko anakopata matibabu baada ya kutoka Nairobi nchini Kenya baada ya kupigwa risasi Dodoma atrehe 7 September 2017.

Akiwa Marekani kwenye majimbo taofauti akiongea na watanzania waishio huko yaani Diaspora amekuwa akielezea tukio lake la kupigwa risasi na namna Bunge lilivyoshughulikia tatizo hilo pasipo kummpa msaada wowote ingawa Bunge nalo limekuwa litoa taarifa kuhusu utaratibu wa wabunge kutibiwa ambapo Lissu hakufuata utaribu huo.

Lakini katika moja ya maongezi yake na watanzania huko Marekani Mhe Tundu Lissu amekuwa akirudia mara kwa mara kuwa kuna watu wasiopungua 400 wameuwawa au kupotea huko mkoa wa Lindi na watu hao wameuwawa na serikali yetu.

Kiukweli kama namba 400 ya watu wameuwawa au kupota ni idadi kubwa sana kiasi kwamba jamii ya huko Lindi tungeona hayo malalamiko hadharani kabisa lakini sijawahi kusikia suala hilo kabisa kwenye tv zetu redio zetu hata magazeti yetu hata ushahidi wake wa tukio hilo.

Lakini Lissu ndiyo moja ya ujumbe ambao anaeneza huko Magharibi je RPC wa Lindi amelisia hilo?

Maswali:

  1. Kunataarifa yoyote iliyopo Polisi kwa maana ndugu kuripoti Polisi kuhusu kupotea kwa idadi hiyo ya watu huko Lindi?
  2. Vyombo vya habari vimehai kuwahoji ndugu waliopotewa na ndugu zao huko Lindi kwa ushahidi?
  3. Je kuna yoyote yule huko Lindi mwenye kujua hata mmoja yoyote yule aliyeuwawa au kupotea?
  4. Viongozi wa Dini huko Lindi wamewahi kupokea taarifa yoyote ya familia zilizopotelewa na ndugu zao ktk kufanya maombi au dua?
  5. Kuna taasisi yoyote hasa hizi za haki za binadamu na ustawi wa jamii imewahi kufanya utafiti mdogo wa taarifa kama hiyo ya watu 400 kupota au kuuwawa?
  6. Kuna yoyote yule aliyewahi kuona hata maiti za hao watu au makaburi ya hao watu kuthibitisha hilo?

Mkuu kwani we idadi yako Ni kiasi gani?

Zitto alitoa takwimu Bungeni zaidi 369 akatishwa na story ikaishia hapo. Akasema anaouthibitisho 183 confirmed cases anaendelea na uchunguzi.

Hata wangekuwa watu 20 yatosha walau tuna watu watatu dunia inafahamu Been Saanane, Azory na Mkiti wa Wilaya Kakonko missing todate.

Lakini hakuna majibu ya walikua wanaokotwa Coco Beach na mto Ruvu Ni kina Nani.

Yatosha kusema Kuna mauaji yanatokea pasipo kujua muuaji.
 
Kulikuwa na Nini katika hiyo operation
Baadhi ya wanadiaspora Marekani wampingana na Mhe Tundu Lissu ktk majadiliano hadharani - JamiiForums
sasa naamini kuna watu mapunguani hawana evudence lakini wapo hapa kwa kutumwa na kulipwa buku 7
mwenzenu kapigwa risasi
matibabu hamumpi lkn Wabunge na viongozi wengine wanalipiwa matibabu na hawarudi
sasa LISSU anawaumbua kwanini msikae kimya km yeye ni kichaa hamjui mnamuongezea umaarufu?
hao Diaspora wote wako nyuma yake
 
Kumbe walipokuwa wanauwawa wananchi waliokuwa hawana hatia na hao mnaowatetea mliona sawa tu!! Tumeshawajua!!
Hao wasio na hatia waliuwawa na nani, je siku hizi serikali ndo imeamua kujichukulia sheria mkononi?je siku sisi wananchi tukiamua kujichukulia sheria mkononi watalalamika kuwa tunataka kuingoa madarakani serikali halali?
 
Back
Top Bottom