Hivi ni kweli kuna watu 400 wameuawa mkoa wa Lindi kama Tundu Lissu anavyotangaza huko Marekani?

tatum

JF-Expert Member
Jan 16, 2018
5,786
4,490
Tundu Lissu Mbunge wa Singida Mashariki amekuwa kwenye ziara isiyo rasmi huko Marekani akitokea nchini Ubeligiji ambako ndiko anakopata matibabu baada ya kutoka Nairobi nchini Kenya baada ya kupigwa risasi Dodoma atrehe 7 September 2017.

Akiwa Marekani kwenye majimbo taofauti akiongea na watanzania waishio huko yaani Diaspora amekuwa akielezea tukio lake la kupigwa risasi na namna Bunge lilivyoshughulikia tatizo hilo pasipo kummpa msaada wowote ingawa Bunge nalo limekuwa litoa taarifa kuhusu utaratibu wa wabunge kutibiwa ambapo Lissu hakufuata utaribu huo.

Lakini katika moja ya maongezi yake na watanzania huko Marekani Mhe Tundu Lissu amekuwa akirudia mara kwa mara kuwa kuna watu wasiopungua 400 wameuwawa au kupotea huko mkoa wa Lindi na watu hao wameuwawa na serikali yetu.

Kiukweli kama namba 400 ya watu wameuwawa au kupota ni idadi kubwa sana kiasi kwamba jamii ya huko Lindi tungeona hayo malalamiko hadharani kabisa lakini sijawahi kusikia suala hilo kabisa kwenye tv zetu redio zetu hata magazeti yetu hata ushahidi wake wa tukio hilo.

Lakini Lissu ndiyo moja ya ujumbe ambao anaeneza huko Magharibi je RPC wa Lindi amelisia hilo?

Maswali:

  1. Kunataarifa yoyote iliyopo Polisi kwa maana ndugu kuripoti Polisi kuhusu kupotea kwa idadi hiyo ya watu huko Lindi?
  2. Vyombo vya habari vimehai kuwahoji ndugu waliopotewa na ndugu zao huko Lindi kwa ushahidi?
  3. Je kuna yoyote yule huko Lindi mwenye kujua hata mmoja yoyote yule aliyeuwawa au kupotea?
  4. Viongozi wa Dini huko Lindi wamewahi kupokea taarifa yoyote ya familia zilizopotelewa na ndugu zao ktk kufanya maombi au dua?
  5. Kuna taasisi yoyote hasa hizi za haki za binadamu na ustawi wa jamii imewahi kufanya utafiti mdogo wa taarifa kama hiyo ya watu 400 kupota au kuuwawa?
  6. Kuna yoyote yule aliyewahi kuona hata maiti za hao watu au makaburi ya hao watu kuthibitisha hilo?
 
mkuu unakuwa kama free will man wakati inajulikana kabisa upo blinded na serikali...tetesi ama taarifa zozote kuhusu mauaji na mateso kwa raia haupaswi kuzipinga. Ulitegemea CPYRIAN MSIBA aandike? ulitaka CHANEL 10 waoneshe ama ulitaka Le MUTUS blogs wakujuze?
 
Tutajuaje hayo wakati vyombo vya habari vimepigwa pini?

Vyombo vyetu vya habari vimeelekezwa kusifu tu hata mkuu akinywa damu ya mtu vyenyewe vinatakiwa kusifu.
Tumeona kiongozi wa serikali kumpiga mtu risasi huko Singida akiwa kanisani na tukio hilo likafunikwa kwa muda mrefu mwisho ikasemekana sio yeye aliyemuua.

Kadhalika matukio ni mengi nchi hii ambayo hayaruhusiwi kuwa public

Kuna siku yoyote yametolewa maelezo au kufanywa uchunguzi juu ya uhalifu aliofanyiwa kwenye viunga vya bunge mbunge wetu kipenzi Tundu Lisu?
Kuna siku yoyote yametolewa maelezo au uchunguzi juu ya aliko kijana mwenzetu Ben saanane?

Kuna siku yoyote yametolewa maelezo au kufanywa uchunguzi juu ya makumi ya maiti zinazookotwa baharini na mitoni?

Kwanini tusiamini anachokisema Tundu lisu kama hali ya usalama ndio hii ndani ya nchi yetu?

Serikali hii imeshindwa lakini haitaki kukubali!
Imeshindwa tena ni ya kuvurusha kama avurushwavyo jambazi.
 
Hayo yote uliyotaja yalishatolewa maelezo Tena Kwa kina na wahusika labda Kama haupo nchini

Hakuna chombo Cha habari kilichopigwa marufuku
 
Huenda kweli watu waliuawa huko MKIRU but with good exagretion ya idadi. Kipindi hiki ni cha wewe kujiongeza dont assimilate kila kitu unaambiwa

400÷ idadi ya vijiji (MKIRU)=UHALISIA(Missing people)

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom