Hivi ni kweli kuna watu 400 wameuawa mkoa wa Lindi kama Tundu Lissu anavyotangaza huko Marekani?

Mauaji ya watu 400 haiwezi kuwa siri
Waulize watu wa Ruvu na Bagamoyo..viroba vilikuwa vya kumwaga...Mwigulu akadai wahamiaji haramu..Leo yamemfika anaomba watu wamuombee...nasema nitamuombea punda aliyemgonga
 
Mliotaka orodha si ndiyo hiyo imewekwa nakumbuka aliomba iundwe tume ikachunguzwe ikakataliwa ndipo serikali ikapiga marufuku hata magazeti kuandika Habari za kibiti ndo ukawa mwisho wa kusikia Habari za huko. Kwakweli mauwaji hayo yalilalamikiwa sana nashangaa wanaosema hawakusikia sijui walitaka wasikiaje. Haya mambo leo yanafunikwa lakini iko siku uchunguzi utafanyika na itajulikana waliouwawa ni wangapi na nani aliwauwa.
 
Tundu Lissu Mbunge wa Singida Mashariki amekuwa kwenye ziara isiyo rasmi huko Marekani akitokea nchini Ubeligiji ambako ndiko anakopata matibabu baada ya kutoka Nairobi nchini Kenya baada ya kupigwa risasi Dodoma atrehe 7 September 2017.

Akiwa Marekani kwenye majimbo taofauti akiongea na watanzania waishio huko yaani Diaspora amekuwa akielezea tukio lake la kupigwa risasi na namna Bunge lilivyoshughulikia tatizo hilo pasipo kummpa msaada wowote ingawa Bunge nalo limekuwa litoa taarifa kuhusu utaratibu wa wabunge kutibiwa ambapo Lissu hakufuata utaribu huo.

Lakini katika moja ya maongezi yake na watanzania huko Marekani Mhe Tundu Lissu amekuwa akirudia mara kwa mara kuwa kuna watu wasiopungua 400 wameuwawa au kupotea huko mkoa wa Lindi na watu hao wameuwawa na serikali yetu.

Kiukweli kama namba 400 ya watu wameuwawa au kupota ni idadi kubwa sana kiasi kwamba jamii ya huko Lindi tungeona hayo malalamiko hadharani kabisa lakini sijawahi kusikia suala hilo kabisa kwenye tv zetu redio zetu hata magazeti yetu hata ushahidi wake wa tukio hilo.

Lakini Lissu ndiyo moja ya ujumbe ambao anaeneza huko Magharibi je RPC wa Lindi amelisia hilo?

Maswali:

  1. Kunataarifa yoyote iliyopo Polisi kwa maana ndugu kuripoti Polisi kuhusu kupotea kwa idadi hiyo ya watu huko Lindi?
  2. Vyombo vya habari vimehai kuwahoji ndugu waliopotewa na ndugu zao huko Lindi kwa ushahidi?
  3. Je kuna yoyote yule huko Lindi mwenye kujua hata mmoja yoyote yule aliyeuwawa au kupotea?
  4. Viongozi wa Dini huko Lindi wamewahi kupokea taarifa yoyote ya familia zilizopotelewa na ndugu zao ktk kufanya maombi au dua?
  5. Kuna taasisi yoyote hasa hizi za haki za binadamu na ustawi wa jamii imewahi kufanya utafiti mdogo wa taarifa kama hiyo ya watu 400 kupota au kuuwawa?
  6. Kuna yoyote yule aliyewahi kuona hata maiti za hao watu au makaburi ya hao watu kuthibitisha hilo?
Kama source ni mwehu Lisu, nenda kamuulize mwenyewe! Huyu si ndio alisemaga rais wetu mpendwa hajui hata kuongea sentensi moja ya kiingereza…kitu ambacho ni uongo hata shetwani alimcheka kwa kugalagala!
 
Kama source ni mwehu Lisu, nenda kamuulize mwenyewe! Huyu si ndio alisemaga rais wetu mpendwa hajui hata kuongea sentensi moja ya kiingereza…kitu ambacho ni uongo hata shetwani alimcheka kwa kugalagala!
OK
 
Back
Top Bottom