Hivi ni kweli kuna watu 400 wameuawa mkoa wa Lindi kama Tundu Lissu anavyotangaza huko Marekani?

CCM imeingilia kivipi vyombo vya uchunguzi

..sasa kwanini uchunguzi haufanyiki kubaini wananchi hao wamepotea vipi.

..Mbunge ametoa ushahidi wa wananchi wake kuuwawa wakiwa MSIKITINI.

..Je, ni haki Polisi kuua ktk nyumba za ibada?
 
Kama unalijua hilo umeleta huu uzi hapa wa kazi gani?,si ukae kimya kama unavyodai...
sio kila kitu kinachotamkw ana mtu basi kinahitaji majibu mengine unapuuza tu na kuendelea na kazi zako kama kawaida......huwezi kila siku kufanyia kazi taarifa za kuzusha tu.....maeneo yote hayo ya TISS na wanajua ukweli wake ndiyo maana watu wanaendelea na kazi kama kawaida na yale mauaji ya viongozi yalishakomeshwa kitu ambacho kilikuwa hakiwapi kabisa viongozi usingizi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tutajuaje hayo wakati vyombo vya habari vimepigwa pini?

Vyombo vyetu vya habari vimeelekezwa kusifu tu hata mkuu akinywa damu ya mtu vyenyewe vinatakiwa kusifu.
Tumeona kiongozi wa serikali kumpiga mtu risasi huko Singida akiwa kanisani na tukio hilo likafunikwa kwa muda mrefu mwisho ikasemekana sio yeye aliyemuua.

Kadhalika matukio ni mengi nchi hii ambayo hayaruhusiwi kuwa public

Kuna siku yoyote yametolewa maelezo au kufanywa uchunguzi juu ya uhalifu aliofanyiwa kwenye viunga vya bunge mbunge wetu kipenzi Tundu Lisu?
Kuna siku yoyote yametolewa maelezo au uchunguzi juu ya aliko kijana mwenzetu Ben saanane?

Kuna siku yoyote yametolewa maelezo au kufanywa uchunguzi juu ya makumi ya maiti zinazookotwa baharini na mitoni?

Kwanini tusiamini anachokisema Tundu lisu kama hali ya usalama ndio hii ndani ya nchi yetu?

Serikali hii imeshindwa lakini haitaki kukubali!
Imeshindwa tena ni ya kuvurusha kama avurushwavyo jambazi.
huyu hapa hayuko ulaya yupo hapa hapa na aliyasema haya bila kificho. mwambie na yeye ni mwongo
 
Mara ya mwisho Zitto alileta list ya watu 380.

Na hakufunguliwa mashtaka kwa uchochezi ingawa alizungumzia hadharani! Haijalishi wako wako wangapi; hoja ni kuwa kuna madai ya watu kupotea au kuuawa na serikali inawajibika kuchukua hatua. Haijapata kutokea serikali ya nchi hii kutuhumiwa kuua raia na kunyamaza. Kukaa kimya maana yake ni kuruhusu raia kuamini kuwa madai hayo ni ya kweli.
 
Tuwekee ushahidi was mauaji sio maneno tu....maneno hata kasuku anaongea

Be serious! Hoja umeleta wewe; tena hoja nzito sana halafu unafanya mzaha! Ushahidi gani unaoweza kuwekwa hapa jf? Tuhuma za watu kupotezwa ni nzito; siyo kitu cha kurahisisha kwa kusema weka ushahidi. Zitto alipata kuorodhesha idadi kubwa ya hao watu waliopotea; zaidi ya 300. Je, amepata kujibiwa? Sikumbuki. Mwandishi wa habari wa Mwananchi amepotea akijaribu kufuatilia hizi habari. Kupotea kwake kunaonekana kutowasumbua viongozi wetu; wanachukulia kama wanajua mahali alipo na kuna siku atarudi kwa familia yake! Je, hilo haliongezi hofu kwa raia? Kama wewe huna tofu basi utakuwa na bahati kubwa sana.
 
Guys nilishasema na ninarudia tena kusema. Dawa za usingizi huwa zina kiasi flan cha cocaine, operation 23 sio chache lazima dawa bado zimo kichwani mwa mheshimiwa, anayeongea sio yeye, maana anaulizwa mkate unapande ngapi, yeye anajibu kitumbua huwa cha raundi. Hapa ndo huwa nagundua mpendwa wetu huyu bado mgonjwa. Leo nimeona anahojiwa na redio moja ya kiswahili wakamuuliza ukiondoa political differences na magu, nje ya hapo maelewano yako na yeye yakoje. Habari aloibuka nayo anaanza kuongelea msiba wa dada yake, na rambirambi alizotoa rais, akaulizwa tena kuzurura kooote ukilicbafua taifa la watanzania, what is your interest, akaanza kusema serikali inaua watu sana, nlitegemea wamuulize kama anaweza kusema nani aliuawa na serikali

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hayo yote uliyotaja yalishatolewa maelezo Tena Kwa kina na wahusika labda Kama haupo nchini

Hakuna chombo Cha habari kilichopigwa marufuku
Unaishi dunia gani, kwakuwa umejivika cheo cha msemaji wa sisiemu nikuulize...

Kama hakuna chombo kilichopigwa marufuku

1.Liko wapi gazeti pendwa la Mwanahalisi?

2.Vipi kuhusu Mawio?

Najiuliza kama gazeti la musiba (Tanzanite) linavyochapisha matusi wahusika wanaliona au wapo kwaajili ya upande fulani?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Unaishi dunia gani, kwakuwa umejivika cheo cha msemaji wa sisiemu nikuulize...

Kama hakuna chombo kilichopigwa marufuku

1.Liko wapi gazeti pendwa la Mwanahalisi?

2.Vipi kuhusu Mawio?

Najiuliza kama gazeti la musiba (Tanzanite) linavyochapisha matusi wahusika wanaliona au wapo kwaajili ya upande fulani?

Sent using Jamii Forums mobile app
Hakuna msemaji was ccm hapa mimi ni mwana JF

Magazeti hayo yalikiuka sheria ya magazeti na ndiyo maana huyaoni.
 
Tundu Lissu Mbunge wa Singida Mashariki amekuwa kwenye ziara isiyo rasmi huko Marekani akitokea nchini Ubeligiji ambako ndiko anakopata matibabu baada ya kutoka Nairobi nchini Kenya baada ya kupigwa risasi Dodoma atrehe 7 September 2017.

Akiwa Marekani kwenye majimbo taofauti akiongea na watanzania waishio huko yaani Diaspora amekuwa akielezea tukio lake la kupigwa risasi na namna Bunge lilivyoshughulikia tatizo hilo pasipo kummpa msaada wowote ingawa Bunge nalo limekuwa litoa taarifa kuhusu utaratibu wa wabunge kutibiwa ambapo Lissu hakufuata utaribu huo.

Lakini katika moja ya maongezi yake na watanzania huko Marekani Mhe Tundu Lissu amekuwa akirudia mara kwa mara kuwa kuna watu wasiopungua 400 wameuwawa au kupotea huko mkoa wa Lindi na watu hao wameuwawa na serikali yetu.

Kiukweli kama namba 400 ya watu wameuwawa au kupota ni idadi kubwa sana kiasi kwamba jamii ya huko Lindi tungeona hayo malalamiko hadharani kabisa lakini sijawahi kusikia suala hilo kabisa kwenye tv zetu redio zetu hata magazeti yetu hata ushahidi wake wa tukio hilo.

Lakini Lissu ndiyo moja ya ujumbe ambao anaeneza huko Magharibi je RPC wa Lindi amelisia hilo?

Maswali:

  1. Kunataarifa yoyote iliyopo Polisi kwa maana ndugu kuripoti Polisi kuhusu kupotea kwa idadi hiyo ya watu huko Lindi?
  2. Vyombo vya habari vimehai kuwahoji ndugu waliopotewa na ndugu zao huko Lindi kwa ushahidi?
  3. Je kuna yoyote yule huko Lindi mwenye kujua hata mmoja yoyote yule aliyeuwawa au kupotea?
  4. Viongozi wa Dini huko Lindi wamewahi kupokea taarifa yoyote ya familia zilizopotelewa na ndugu zao ktk kufanya maombi au dua?
  5. Kuna taasisi yoyote hasa hizi za haki za binadamu na ustawi wa jamii imewahi kufanya utafiti mdogo wa taarifa kama hiyo ya watu 400 kupota au kuuwawa?
  6. Kuna yoyote yule aliyewahi kuona hata maiti za hao watu au makaburi ya hao watu kuthibitisha hilo?
Kama si kweli kwanini Polisi hawajaleta marejesho??
 
Tuwekee ushahidi was mauaji sio maneno tu....maneno hata kasuku anaongea
Unataka ushahidi gani kwa mfano,maana haya maswali yenu ya viroba hayaeleweki,je unataka aweke picha za maiti au video zinazoonesha namna wanavyopigwa na kufa au aweke taarifa ya wauaji inayoonesha ni watu wangapi wameua au unataka taarifa ya police? Be specific
 
Back
Top Bottom