Hivi ni kweli hadi leo NIDA hawana ujuzi wowote wa mtu kuijua namba yake kimtandao?

Rwaz

JF-Expert Member
May 3, 2013
1,968
3,320
Nimefikiria kwa kina taaruki ya NIDA kutofanikisha waliojiandikisha kupata namba zao hadi sasa. Nimefikiria kwa kina vyuo vyote vya IT tulivyonavyo. Nimefikiria uwezo wa kiuchumi wa Tanzania. Nimefikiria uwezo wa kiuongozi na kiutawala tulionao.

Nimefikiria taaruki ilivyo hadi sasa. Nimefikiria makampun ya mtandao yanayofanyakazi nchini. Hivi kweli vichwa vyote hivi vimekaa na suti zao na kufikiri kwa weredi wote na bado ikathibitika hivi kwamba hawana uwezo wa mtu kupata No yake ya NIDA kwa njia ya mtandao?

Yaani nikiona watu walivo smart kwa nguo na haiba za usomi nafikiria ..KWELI NDO HAWA! Serikali imeamua kuamin iliajiri vilaza wa IT kias hiki kweli? Maana hakuna njia hata moja inafanyakazi kwa ufanis hadi leo. Ni her hata wasingeweka njia hizo.

Yani hata namba za kupiga uwezo wao ni kutopokelewa milele! Tunakwama wapi? Basi tuazime hata akili kwa muda nchi yoyote , hao wale tu mshahara mana serkali haina wa kumtupia huo mzigo wake.
 
Nilijiandikisha mwezi wa kumi.
Mwezi wa kumi na moja nilijaribu kutumia link walioitoa ya kupata namba mtandaoni nikapata namba yangu bila kurudi NIDA. Na mke wangu pia.

Tusiwe watu wa kutupa lawama tu.
 
Wewe ulifungua mtandao upi mana portal yao hata haifunguki! Njia ya kutuma sms inakula tu pesa hailet majibu! Kwenye app ndo kabisa imejaa ads kama talking walls hadi huwez tumia!. No za sim hazipatikan! Kama una hakika ifungue na uweke link hapa.
 
Akiweka link naomba nitag mkuu, asante.
 
Kuna app play store ukiipakua unaweka taarifa zako then hapo hapo inakupa namba na pia ni easy kuitumia

Nmeijaribu na namba nkazipata saa hiyo hiyo..

Wewe ulifungua mtandao upi mana portal yao hata haifunguki! Njia ya kutuma sms inakula tu pesa hailet majibu! Kwenye app ndo kabisa imejaa ads kama talking walls hadi huwez tumia!. No za sim hazipatikan! Kama una hakika ifungue na uweke link hapa.
 
Vipi mkubwa umejaribu *152*00# na 15096
Ila tuwe wakweli tuko nyuma sana kiteknolojia na sidhani kama hawa nida wataweza kulinda taarifa zetu nyeti walizoingiza kwenye server zao
 
Pia kuna kitu nimejiuliza mwenyewe bila kupata jibu lolote hivi hawa raia Wa kigen wanaoishi nchini kwetu watawezaje kumiliki line za Sim pasipo kua na kitambulisho cha taifa?
Au kuna utaratibu gani uliowekwa kwa hawa raia Wa kigen waishio nchini mwetu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Utapataje copy bila kuwa na namba(NIN)
Kuna option ya kupata namba ya Nida na option ya kupata ya copy ya kitambulisho. Ukichagua kupata namba ya nida (NIN) kuna taarifa zako unajaza kisha inaletewa namba yako ya NIN. Ukienda kwenye option ya kupata copy ya kitambulisho utaambiwa uweke namba yako ya Nida kisha utajaza na taarifa zako zingine watakazokuletea kisha ndio utaletewa option ya ku-download. Binafsi nilifanikiwa kupata copy ya kitambulisho

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom