Hivi ni kwanini Typhoid haiko kwenye bima ya afya?

Ruyama

JF-Expert Member
Sep 6, 2019
367
561
Jana niliamka vibaya sana kwani mwili ulikuwa na joto kali mnoo,kwenda Hospital nikawaeleza ninavyojisikia,Daktari akasema kapime malaria na UTI, nikamwambia jee naweza kupima Typhoid akasema lipia,duumfukoni balance haitoshi.

Majibu yanatoja naambia nina UTI ila sina Malaria, sasa leo tokea saa 10 alfajiri ninahisi joto lipo juu na hii hali ni usiku tu mchana niko vizuri.
 
Majibu yanatoja naambia nina UTI ila sina Malaria,sasa leo tokea saa 10 alfajiri ninahisi joto lipo juu na hii hali ni usiku tu mchana niko vizuri.
Wanalipa ukifanya kipimo cha culture na siyo kwa kipimo cha widal test. Vituo vingi vinatumia widal test ambayo inaweza kuleta majibu yasiyo sahihi. Kwa sababu hata ukiwa na ugonjwa mwingine ambao unaweza kupata widal positive. Kumbe siyo Typhoid ni ugonjwa mwingine, Bima wanashauri kufanya Culture.
 
Mkuu umeniacha patupu
 
Kapime maabara ya private mkuu afya yako ni muhimu zaidi, mimi ndo namalizia dozi ya Cipro hapa nlilipia kipimo buku mbili.
Japo kiafrika ni Mungu anasaidia maana unaweza kula maembe yako tumbo likavuruga ukaenda hospitali ukapigwa dozi ya typhoid.
 
Mkuu umeniacha patupu
Wewe ukienda kupima choo majibu yake unayapata hapohapo sio? Sasa hiyo anayozungumzia jamaa hapo juu unaacha choo chako hospitali kinasindikwa kama mbegu za mahindi zinazo oteshwa kwenye maji 😂😂😂 hapo nasikia kinakaushwa baadaw kinasagwa kisha ndio kinapimwa kisha unaitwa siku nyingine kuchukua majibu yako
 
Kuna siku nafikiri nilimsikia daktari mmoja wa wizara akijibu swali ili,yeye alichosema ni kwamba, Typhoid kwa muongozo wa wizara,mahospital wanatakiwa kuwa na vipimo viwili ili kuweza kupima hii Typhoid ili upate majibu ya uhakika kama mgonjwa anayo typhoid au hana.
1. Kipimo cha kwanza ambacho mahospital karibia yote wanatumia gharama yake ni ndogo,hiki kila hospital wanacho.
2. Kipimo cha pili ambacho ndio kitathibitisha kwa asilimia 100 kama mtu anayo Typhoid au lah, hiki ni gharama kubwa sana na mahospital mengi hawana hiki kipimo.

Ili mahospital wasiingie kwenye mtego wa wizara,wanaona bora kipimo cha Typhoid kisiwepo kwenye bima, kwasababu kama umempima mgonjwa,bila kufuata muongozo wa wizara kama unavyosema wanaweza kupata matatizo.

Kwa kifupi hospital wanatupa majibu ya typhoid bila yakuwa na uhakika wa asilimia 100 kwasababu hawana kipimo cha pili cha kuthibitisha ilo.
 
Jana niliamka vibaya sana kwani mwili ulikuwa na joto kali mnoo,kwenda Hospital nikawaeleza ninavyojisikia,Daktari akasema kapime malaria na UTI, nikamwambia jee naweza kupima Typhoid akasema lipia,duumfukoni balance haitoshi.

Majibu yanatoja naambia nina UTI ila sina Malaria, sasa leo tokea saa 10 alfajiri ninahisi joto lipo juu na hii hali ni usiku tu mchana niko vizuri.
kama kwenye dose yako umepewa Ciprofloxacin ... inaweza kukusaidia pia kwa Typhoid .. Ungeongea na Daktari wako akakusaidia
 
Kapime maabara ya private mkuu afya yako ni muhimu zaidi, mimi ndo namalizia dozi ya Cipro hapa nlilipia kipimo buku mbili.
Japo kiafrika ni Mungu anasaidia maana unaweza kula maembe yako tumbo likavuruga ukaenda hospitali ukapigwa dozi ya typhoid.
Mungu Yuko Afrika.Hapa unakula chips pale pana kuna chemba ya kinyesi inacheua mtori.
 
Wanalipa ukifanya kipimo cha culture na siyo kwa kipimo cha widal test. Vituo vingi vinatumia widal test ambayo inaweza kuleta majibu yasiyo sahihi. Kwa sababu hata ukiwa na ugonjwa mwingine ambao unaweza kupata widal positive. Kumbe siyo Typhoid ni ugonjwa mwingine, Bima wanashauri kufanya Culture.
hii culture inafanywa kwenye hospitali zip za rufaa au za wilaya
 
Mungu Yuko Afrika.Hapa unakula chips pale pana kuna chemba ya kinyesi inacheua mtori.
Habari,
Upimaji wa typhoid upo wa aina tatu, nitahitaji kusahihishwa kama nimekosea.
1: Semi quantitative
Ambayo hutumia slide. Majibu yake siyo ya kuaminika. Ili upate majibu halisi inabidi upime mara mbili. Siku ya kwanza na baada ya masaa 24 ili uone kuongezeka kwa titre/kiasi cha chemikali inayopimwa. Vituo vingi vya afya hufanya kipimo cha aina hii na kutoa majibu kwa siku moja ambayo si ya uhakika.

2: Quantitative method
Hii huusisha titration kwenye test tube.
Wizara hutoa vigezo na cheti kwa maabara zenye uwezo wa kufanya hivyo.
Majibu yake yanaaminika. Hapa ndo hitaji la NHIF pia lilipo. Uwe na cheti cha Wizara kuthibitisha uwezo huo wa maabara husika.

3: Kipimo cha choo
Stool antigen test ambayo pia majibu yake yanaaminika.

Ushauri:
Nakushauri mgonjwa urudi hospitali.

1: Daktari apate historia yako vizuri pamoja na tiba unayotumia kwa sasa. Ikijumuisha kama una mafua au kikohozi au koo kuwasha.

3: Binafsi, ningependa ufanye
a: Full blood picture:
ili nijue homa hii ni ya bacteria au virus
b: Rudia kipimo cha malaria kwani, unaweza pima malaria mapema unapopata dalili majibu yakawa negative na ukirudia baada ya zaidi ya masaa sita, ukapata majibu tofauti.
 
Jana niliamka vibaya sana kwani mwili ulikuwa na joto kali mnoo,kwenda Hospital nikawaeleza ninavyojisikia,Daktari akasema kapime malaria na UTI, nikamwambia jee naweza kupima Typhoid akasema lipia,duumfukoni balance haitoshi.

Majibu yanatoja naambia nina UTI ila sina Malaria, sasa leo tokea saa 10 alfajiri ninahisi joto lipo juu na hii hali ni usiku tu mchana niko vizuri.
Sio kwenye kupima tu hata dawa zingine hawatoi sijui kama body ya bima ya afya huwa ina keti na ku fikiria ku update list yao ya dawa kutokana usugu wa magonjwa na allergy ya mtu. mfano nikinywa dawa ya malaria yenye salfa natokewa na vipele, pia dawa za malaria walizoweka zisizidi sh 1500. dawa zisizo na salfa zinauzwa bei zaidi hawakupi. kuna haja ya bodi kupanga upya na sio kubana matumizi.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom