Mungu Yuko Afrika.Hapa unakula chips pale pana kuna chemba ya kinyesi inacheua mtori.
Habari,
Upimaji wa typhoid upo wa aina tatu, nitahitaji kusahihishwa kama nimekosea.
1: Semi quantitative
Ambayo hutumia slide. Majibu yake siyo ya kuaminika. Ili upate majibu halisi inabidi upime mara mbili. Siku ya kwanza na baada ya masaa 24 ili uone kuongezeka kwa titre/kiasi cha chemikali inayopimwa. Vituo vingi vya afya hufanya kipimo cha aina hii na kutoa majibu kwa siku moja ambayo si ya uhakika.
2: Quantitative method
Hii huusisha titration kwenye test tube.
Wizara hutoa vigezo na cheti kwa maabara zenye uwezo wa kufanya hivyo.
Majibu yake yanaaminika. Hapa ndo hitaji la NHIF pia lilipo. Uwe na cheti cha Wizara kuthibitisha uwezo huo wa maabara husika.
3: Kipimo cha choo
Stool antigen test ambayo pia majibu yake yanaaminika.
Ushauri:
Nakushauri mgonjwa urudi hospitali.
1: Daktari apate historia yako vizuri pamoja na tiba unayotumia kwa sasa. Ikijumuisha kama una mafua au kikohozi au koo kuwasha.
3: Binafsi, ningependa ufanye
a: Full blood picture:
ili nijue homa hii ni ya bacteria au virus
b: Rudia kipimo cha malaria kwani, unaweza pima malaria mapema unapopata dalili majibu yakawa negative na ukirudia baada ya zaidi ya masaa sita, ukapata majibu tofauti.