Hivi ni kwanini jina la ubini / ukoo linatumika la baba?

Hivi ni kwanini jina la ubini / ukoo linatumika la baba?

Mama ana kazi nzito tangu alivyobeba ujauzito kujifungua mpaka kulea ni yeye ndo anaye play big part kwanini ubini usitumike wa kwake mfano Asha Rose Migiro.

Kuna kabila wanatumia ubini wa mama jina limenitoka kidogo nikikumbuka nitaliweka hapa ila most of us tunatumia ubini wa baba kwanini?

Mama ana majukumu mazito sana alipaswa kupewa heshima kwa kutumia ubini wake.
njoo unyakyusa ujifunze jinsi kwa jadi majina yanavyotoka upande wa mama,ukisikia mnyakyusa anaitwa david mwakyusa ujue bibi yake na baba yake alitwa ..... kyusa.wanaume wanaongeza prefix mwa.kama ni bint anaitwa kissa ijande ,ujue bibi yake mzaa baba anaitwa ..... ijande.
 
Kuwa pathetic ni kuona kwamba Spain wana utamaduni mzuri wa kufata ukoo kwa mama. Sikatai ila kwani kuna ubaya gani ukoo ukiwa kwa baba? Kila kitu kwa mama thats why mitoto ya siku hizi walaini unakuta dume zima kila kitu kwa mama, hata limeoa lakini linataka kumshirikisha mama kwenye ndoa yake, ndio maana wake zenu wanawaona wanaume suruali. Kuwa kama mwanaune pale unapotakiwa kuwa mwanaume mjomba sio kila kitu apewe mwanamke mtagawa hadi jinsia zenu mwishowe.just be a man bana

Mkuu, rudia kusoma. Spain wanatumia majina matatu. La kwanza la mhusika, la pili la baba na la tatu la mama. Hawatumii la mama peke yake!

Golikipa maarufu wa Spain anaitwa Iker Casillas Fernández. Casillas kwa baba na Fernandez kwa mama yake. Kwenye nyaraka rasmi lazima yote yaonekane.
 
Mkuu, rudia kusoma. Spain wanatumia majina matatu. La kwanza la mhusika, la pili la baba na la tatu la mama. Hawatumii la mama peke yake!

Golikipa maarufu wa Spain anaitwa Iker Casillas Fernández. Casillas kwa baba na Fernandez kwa mama yake.

Ok ila sikubaliani na huo utamaduni
 
Mama ana kazi nzito tangu alivyobeba ujauzito kujifungua mpaka kulea ni yeye ndo anaye play big part kwanini ubini usitumike wa kwake mfano Asha Rose Migiro.

Kuna kabila wanatumia ubini wa mama jina limenitoka kidogo nikikumbuka nitaliweka hapa ila most of us tunatumia ubini wa baba kwanini?un

Mama ana majukumu mazito sana alipaswa kupewa heshima kwa kutumia ubini wake.
wanyakyusa
 
Mama ana kazi nzito tangu alivyobeba ujauzito kujifungua mpaka kulea ni yeye ndo anaye play big part kwanini ubini usitumike wa kwake mfano Asha Rose Migiro.

Kuna kabila wanatumia ubini wa mama jina limenitoka kidogo nikikumbuka nitaliweka hapa ila most of us tunatumia ubini wa baba kwanini?

Mama ana majukumu mazito sana alipaswa kupewa heshima kwa kutumia ubini wake.

we katumie la mama tu hukatazwi.tutaanza kuona unaitwa "the worldisnotfair kidawa"na wewe unaitika naam
 
Point kubwa apa ya kwnn watu tunatumia ubin wa baba ni kwa sababu ya identification tu...kwa upande wa mama haina shida ni iko wazi tu kuwa mtoto husika ni wa kwake kwa sababu ni yeye ndie aliyeibeba mimba ya huyo mtoto na pia ndie aliyemzaa na jamii inayomzunguka pia inaelewa ivo,tatizo ni kwa upande wa baba kwa sababu kam halijatumika jina lake husika ambalo litamtambulisha huyo mtot kuwa ni wa baba flani basi kuna uwezekano mkubwa wa huy baba kuibiwa huy kiumbe au ata kumkosa kabisa kwa njia yoyote ile as hakuna documentary evidence n identification evidence inayoonesha kuwa huyo mtot na wa huy baba...kwa iyo ni vema kutumia ubin wa baba ili kuepusha migogoro isiyo ya lazima ktk familia na jamii kwa ujumla juu ya uhalali wa umiliki wa huy mtot kw baba flani.

kuibiwa kupo palepale; mama ndo anajua mtoto ni wa nani labda awe kicheche sana jina haliwezi kuzuia kuibiwa!
 
we katumie la mama tu hukatazwi.tutaanza kuona unaitwa "the worldisnotfair kidawa"na wewe unaitika naam

Hata hao wanaotumia jina la mama hawatumii jina lake la kwanza! Wanatumia jina la ukoo wa mama! Mfano Kijana anaitwa Juma. Baba yake anaitwa Hamisi Mbonde na mama Kidawa Kingwande.
Jina kamili la kijana litakuwa Juma Mbonde Kingwande!
 
Sasa jina la ukoo wa mama unaanzaje kulitumia? Halafu kama ishu ni hiyo nadhani utakuta jina la ukoo wa mama linatoka kwa babu yako ambaye ni mwanaume. Halafu kwa nini uhangaike kulazimisha kutumia jina la ukoo la mama yako au huyo baba sio babako? Au mamako ana pesa saaana kumzidi babako sasa unaona hauna haja ya kuwa na baba? Au huyo mamako keshakuonyesha babako mwingine? Au huyo mamako alijipa ujauzito wako bila huyo babako? Maswali ni mengi sana
 
Mara nyingi sheria na kanuni huwa zinavunjwa hivyo hta suala hili lazima livunjwe ili kuwepo mkanganyiko

mm mwenyewe nimebadili jina natumia ubini wa mama
kimsingi wadada wa mawazo kama hayo wapo wengi ila huwa wanasahau jambo 1 kuwa mtt hana ufanani wa damu na mama hyo ni dunian kote, hvyo ukitaka ku justify mtt lazima utumie dna ya baba, so huyo mama na wengine wote mtt hatambuliki kwa mama ila kwa baba

pia ni agizo la mungu, kwamba watt watambuliwe kwa ukoo wa kiume,
 
Sasa jina la ukoo wa mama unaanzaje kulitumia? Halafu kama ishu ni hiyo nadhani utakuta jina la ukoo wa mama linatoka kwa babu yako ambaye ni mwanaume. Halafu kwa nini uhangaike kulazimisha kutumia jina la ukoo la mama yako au huyo baba sio babako? Au mamako ana pesa saaana kumzidi babako sasa unaona hauna haja ya kuwa na baba? Au huyo mamako keshakuonyesha babako mwingine? Au huyo mamako alijipa ujauzito wako bila huyo babako? Maswali ni mengi sana

It seems arguing with you is an exercise in futility. Soma kitu uelewe ndio mengine yafuate. Nimetoa mfano wa watu au nchi wanaojuisha jina la mama kwenye jina kamili la mtu. Sasa hayo ya kwenye RED yanatoka wapi?

Tembea uone. Dunia sio Tanzania. After all, nani analazimisha Tanzania tuige hayo? Vitu hivyo huwa vina evolve vyenyewe taratibu. Na je unajua Tanzania hii hii kuna makabila ambayo uzito upo kwa wajomba kuliko baba wakubwa na wadogo?
 
mi nnavyoona bora walichagua jina la baba litumike ili angalau mtoto atambue uwepo wa baba maana kwakuwa ukaribu wa mama na mtoto ni mkubwa baba anaweza sahaulika

Jina la ukoo litatumika la baba pekee mpaka pale mwanamke atakapo kuwa na uwezo wa kujidunga mimba yeye mwenyewe...bila ya mbegu za kiume.....
Idea zenu zinafanana mmenichekesha sana kumbe kuna uwezekano wa kusahaulika hata kama tuta provide service namna gani kwa watoto, wewe si unaona tu tukiumia kidogo utasikia ''mama yangu'' au ukikoswakoswa na gari barabarani utasikia ''mama yangu'' likitajwa jina lingine ni ''yesu wangu'' au ''mtume'' wachache watasema ''baba yangu'' hivyo kama hakuna sehemu limekuwa documented tutasahaulika.
 
issue hapa sio idea mkuu ni nature ilivyo mtu anatembea nawewe tumbon karibia mwaka, vinguo vyake vyakuoendeza havai tena tumbo lake umefanya room yako, likiwa kubwa kulala hawezi anahema kama ana pumu. loo naturally kuna kamuumhaniko fulani.
baba kupendwa na watoto real bila kusahaulika inakubidi uwe na juhudi kwelikweli tena uwepo karibu na mtoto saana laa sivyo.....
 
It seems arguing with you is an exercise in futility. Soma kitu uelewe ndio mengine yafuate. Nimetoa mfano wa watu au nchi wanaojuisha jina la mama kwenye jina kamili la mtu. Sasa hayo ya kwenye RED yanatoka wapi?

Tembea uone. Dunia sio Tanzania. After all, nani analazimisha Tanzania tuige hayo? Vitu hivyo huwa vina evolve vyenyewe taratibu. Na je unajua Tanzania hii hii kuna makabila ambayo uzito upo kwa wajomba kuliko baba wakubwa na wadogo?

Suala la mfano ulioutoa halihitaji kutembea sana nchi za watu, nafahamu kuna kitu inaitwa matrilineal na patrilineal families. Hata hapa bongo zipo ndugu yangu nachokataa ni kama wewe uwe patrilineal halafu uone haifai. By the way kupishana kimtazamo ndio maendeleo usichoke kujenga hoja.
 
Back
Top Bottom