Hivi ni kwa wa Tanzania tu?

LISAH

Senior Member
Jan 28, 2012
108
24
Jamani kunatabia inanikera katika jamii yetu
Utakuta ndugu yenu anaugua anakosa pesa ya kwenda hospitali , ndugu wanajikausha wakati uwezo wanao
wakumsaidia.
Akifa ndipo kila ndugu anjitia kutonyesha msaada .
Jinsi ya kupamba mazishi nakutoa mchango mkubwa kwaajili ya mazishi.

Jamani wa TZ tubadilike, tujivunie kutoa misaada kwa ndugu wanapo kuwa wanaumwa sio wakati wamekufa. \
\
 
We mleta mada unanitia uchungu maana nina kijana hapa alituomba msaada wa Tsh.2,000,000/= wa kufanyiwa upasuaji toka Sept.2011 nikaanzisha vikao vya hapa na pale kusaka hizo pesa kwaa ndugu zake wa hapa mjini wapo kama ndugu 50 hivi lakini mpaka mwaka huu yaani leo nimekusanya laki tatu tu.Mpaka leo upasuaji bado na kijana anateseka.
 
Pole ndugu, Sasa subiri afe uone hao nduguzo watakavyochanga mihela hiyo-ya kusafirishia mpaka huko kwao, kamera, muziki kwa waombolezaji, corona la kubebea na sanduku liliopambwa, chakula kutoka kwa katara (catere) maarufu, viti vya kukodi, mpambaji wa eneo la msiba na mengineyo bila kusahau kamera mazikoni
 
We mleta mada unanitia uchungu maana nina kijana hapa alituomba msaada wa Tsh.2,000,000/= wa kufanyiwa upasuaji toka Sept.2011 nikaanzisha vikao vya hapa na pale kusaka hizo pesa kwaa ndugu zake wa hapa mjini wapo kama ndugu 50 hivi lakini mpaka mwaka huu yaani leo nimekusanya laki tatu tu.Mpaka leo upasuaji bado na kijana anateseka.

Ngoja afe utakusanya milioni tano kwa nusu siku.
Yaani wa TZ LAANA HII, CJUI TUMEITOA WAPI!
 
Cheki bajeti ya mazishi sasa.1. Najitolea sandu la m 1,2. Mpambaji m.1na nusu,3. Cartering svc m.4. Vipaza sauti laki 5, vinywaji m.3! Jamani hii ni akili au majivu! Mgonjwa kaomba laki 5 tu za tiba wapi!
 
Kweli kwa hili tumelaaniwa!
Wakati wa msiba hadi T-shirt maalum zinatengenezwa, bali wakati angali mzima yu mgonjwa tunamkimbia!
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom