Wazazi pia ni chanzo kikuu cha wanafunzi kufeli.. Achilia mbali serikali na ukosefu wa waalimu!!

Excel

JF-Expert Member
Jul 8, 2011
19,745
10,078
Habari zenu wana jukwaa!

leo tutoke kitofauti kidogo! tutazame hasa nini sabau hasa ya ongezeko kubwa la watoto wetu kufeli mitihani yao ngazi tofauti tofauti katika elimu?

wana jf, kuna sababu nyingi sana ambazo huwa zinapelekea watoto wetu kufeli, tena sababu hizi zimelalia sana upande wa wazazi, achilia mbali serikali na matatizo yake ya ukosefu wa waalimu na vifaa vya kufundishia.

kwanza, wazazi ama walezi wengi sana katika jamii yetu ya kitanzania wamekuwa nyuma sana katika kufuatilia maendeleo ya watoto wao mashuleni na hata majumbani mwao ambapo wanaishi nao! mzazi huyu huyu ambae anailalamikia serikali kwamba inafelisha watoto, amesahahu wajibu wake kuwa, anatakiwa kuwa mstari wa mbele kukagua madaftari ya mwanae, kupata maelezo nini hasa mwanae amesoma katika siku tofauti tofauti pamoja na kufuatilia kwa kina ufanyikaji wa homeworks na assignments mbalimbali za mwanafunzi awapo nyumbani! sasa je, mtoto anapodumbukia katika vilinge vya kihuni na uvutaji bangi, nani atakuwa responsible?

pili, wazazi wamekuwa wakishindwa watoto wao hasa lijapo suala la uongozi wa muda. Mtoto anakuwa anajihusisha saaana na michezo kuliko masomo. mzazi huyo huyo pia anakuwa wa kwanza kumweka bize mtoto wake na mambo ambayo hayana msingi wowote na elimu yake badala ya kuwa wa kwanza kumsisitiza juu ya masomo yake! watoto wanakuwa na muda mrefu sana wanapokuwa majumbani hasa siku za mwishoni mwa juma! huu ndio muda muafaka kabisa wa mtoto kupitia yote yale ambayo aliyasoma shuleni na kufanya masahihisho mbalimbali!
lakini sasa, utakuta wazazi wengi wanakuwa vipaumbele katika kupeleka wanao katika sehemu za starehe na kufanya mambo meengi yasiyokuwa na tija, hatukatai starehe... ila kila jambo liwe na wakati wake!!! kama vitabu vya dini vinavyosema!!! wakati wa masomo, uwe wa masomo tu!! na wakati wa starehe nao uwepo!


mtoto kama mtoto, jinsi umleavyo, ndivyo anavyokua! ukimlea katika mazingira ya kujisomea sana, basi na yeye atakua katika mazingira ya kujisomea sana na hii itamsaidia katika elimu endelevu pia ikiwemo eleimu ya juu! hapo tutapunguza wasomi tegemezi ndugu zangu!! wasomi wetu wa siku hizi wamekuwa wazembe sana wa kufunua vitabu vikubwa! wengi wetu tumeshazoea kupitia summaries za akina nyambari, tunaona hapo ndipo mwisho kabisa wa kuisaka elimu! je, hii itaongeza maarifa?

wazazi hao hao, wanailaumu sana serikali kwamba inafelisha watoto huku wao wanajisahau kwamba wana wajibu wa kuwatimia mahitaji mbali mbali watoto wao ambayo yatakuwa kivutio katika elimu! kwa mfano, unampa mwanafunzi nauli tu! aende shule, kuanzia asubuhi mpaka jioni hajaonja chochote, je huyo utategemea akuletee matoekeo mazuri mwisho wa mwaka?? je, wewe endapo utashinda na njaa kazini kwako kwa masaa manane, utafanya kazi kwa ufanisi mzuri? mjue kitu hapa, kusoma ni moja kati ya kazi nzito ambazo huumiza sana ubongo! hivyo watoto wenu wanahitaji chakula ambacho kinatakiwa kukuza ubongo jamani!!! tekelezeni hilo!!

kwa wale wazazi mlioko vijijini! mna mifugo mingi tu ambayo inawatoa jasho kila leo kuanzia asubhi mpaka jioni, mnashindwa nini kuwanunulia usafiri kama baisikeli watoto wenu waondokane na tatizo la kutembea kilomita 10 kila siku ??? jamani kusoma si kazi nyepesi!! kupokea matokeo hasi nayo ni kazi ngumu!!! msione watoto wanajinyonga ama kujiua kwa sumu, ukadhani walipenda, kuna sababu nyingi sana!! mojawapo ni nyie wazazi kuwa wazembe sana kupitiliza!! tena wengine mna uwezo mkubwa tu, basi mnajifanya kuwa vichwa vigumu!!! BADILIKENI TUOKOE TAIFA!!

wanafunzi wengi wanaoishi mijini na kwenye majiji makubwa, je, kuna haja kweli kuwa na ufaulu mbovu wakati kuna kila kitu jamaniiii???? materials mbalimbali za kujisomea zipo! kwanini wazazi hamjichangi hasa kwa kipindi hiki kifupi ambacho watoto wenu wako shule waweze kuupata urithi wao wa milele??? hivi tutadhalisha watoto wa mbwa mwitu wangapi katika taifa hili?? WAZAZI/WALEZI NA JAMAA MBALIMBALI, TUBADILIKE JAMANI!

KUNA MENGI SANA YA KUZUNGUMZA!! JAZIENI PALIPO ACHWA WAZI!
 
Hongera sana kwa mada nzuri Excel................

mie nomba niongeze jambo moja tu ambalo limesahaulika nalo ni NIDHAMU.

wazazi ama walezi tumejisahau juu ya kuwafunza wanetu kuwa na nidhamu kwenye kila jambo.
kikawaida kabisa mtu hupaswa kauwa na nidhamu ya kila kitu iwe muda, mwili, kwa wenzie, kwa wakubwa, kwa kuongea etc sasa sisi wazazi hili twaliona kama halituhusu vile na wala sio accompaniment kwenye ufaulu ama uelewa wa watoto wetu.

binafsi huwa naamin iwapo0 mwanafunzi ana nidham kwenye muda, kwawatu wote, lugha, mavazi, na hata anavyokaa basi huyu uwezo wa kufundishika na akaelewa ni mikubwa sana.
 
Last edited by a moderator:
Hongera sana kwa mada nzuri Excel................

mie nomba niongeze jambo moja tu ambalo limesahaulika nalo ni NIDHAMU.

wazazi ama walezi tumejisahau juu ya kuwafunza wanetu kuwa na nidhamu kwenye kila jambo.
kikawaida kabisa mtu hupaswa kauwa na nidhamu ya kila kitu iwe muda, mwili, kwa wenzie, kwa wakubwa, kwa kuongea etc sasa sisi wazazi hili twaliona kama halituhusu vile na wala sio accompaniment kwenye ufaulu ama uelewa wa watoto wetu.

binafsi huwa naamin iwapo0 mwanafunzi ana nidham kwenye muda, kwawatu wote, lugha, mavazi, na hata anavyokaa basi huyu uwezo wa kufundishika na akaelewa ni mikubwa sana.

umesema vyema kabisa gfsonwin! nidhamu ni silaha kwa mwanafunzi..! suala la nidhamu nalo ni la msingi kabisa! wazazi nao wamejisahau mno rafiki yangu! unajua, mzazi ambae anaweza kumfundisha nidhamu mwanae, ni yule ambae ana nidhamu pia! Tusidanganyane, mzazi anapofanya mambo ya hovyo hovyo mbele ya mwanae, usidhani kama anaweza kumfunza mwanae akaelewa..!

hebu fikiria, leo umekuja umelewa, umempiga mkeo, umekojoa sebuleni, umemwaga chakula chote, umeninyima nauli ya kwendea shule, umeingiza mwanamke ndani na mambo mengineyo ya kishenzi shenzi..

je, unategemea unifunze nifunzike?? na, unanifunza ukiwa katika hali gani??
 
Last edited by a moderator:
Mkuu naunga mkono %. Hata dini nayo inamchango kwenye hilo.

Mtoto ukimlea kwenye maadili ya dini yoyote, inaleta hofu ya mungu. Hofu ya mungu itamletea nidhamu kama alivyosema gfsonwin
 
Mkuu naunga mkono %. Hata dini nayo inamchango kwenye hilo.

Mtoto ukimlea kwenye maadili ya dini yoyote, inaleta hofu ya mungu. Hofu ya mungu itamletea nidhamu kama alivyosema gfsonwin

ahsante mkuu kwa kuunga mkono..
 
Back
Top Bottom