Hivi ni kwa nini inanitokea hivi...

Hivi ni kwa nini inanitokea hivi...

Hebu jaribu na hiii wewe nenda kaombewe tu ni roho ya hasira itaondoka na utakuwa mwamke mpole mwenye furaha daima.".....lile ninalotaka kulitenda silitendi na nisilotaka kulitenda ninalitenda ni kwa sababu ya dhambi inayokaa ndani yangu"
Hakuna roho ya hasira. Hasira ni hisia na binadamu wote wana hisia ikiwemo hasira - hata Mungu ana hasira. Na tumeambiwa (sisi wakristo) iweni na hasira ila msitende dhambi. Dada ameshagundua kuwa anatenda dhambi kutokana na hasira. Sasa dhambi hii haiwezi kuondoka kwa kuombewa kanisani kwani si pepo. Kama ana imani amwambie Mungu wake kuwa anataka kubadilika - na aanze kwa vitendo yeye mwenyewe huku akiwa na imani kuwa ataweza kwa msaada wa Mungu kwani hana linalomshinda endapo mhusika ataamini. Kubadili tabia ni safari hata kama umeokoka.
 
Aiseee kuuuuuuuuuuuuuuuuuuuumbeeeeeeeeeeeeeeeeeeee:A S-alert1:
 
asante ntalifanyia kazi hili, hata nawe niombee pia na jumapili hii ntaenda nikaombewe pia maana ni hali inayonikera kwa kweli.

Amina nitakuombea jmosi ili ukienda j2 huko ukutane na Bwana,maana sasa naendelea na tenda nyingine ziko mezani......."Mungu hatamtesa mtu hata milele ajapomhuzunisha atamfurahisha kwa kadri ya wingi wa rehema zake"
 
Hakuna roho ya hasira. Hasira ni hisia na binadamu wote wana hisia ikiwemo hasira - hata Mungu ana hasira. Na tumeambiwa (sisi wakristo) iweni na hasira ila msitende dhambi. Dada ameshagundua kuwa anatenda dhambi kutokana na hasira. Sasa dhambi hii haiwezi kuondoka kwa kuombewa kanisani kwani si pepo. Kama ana imani amwambie Mungu wake kuwa anataka kubadilika - na aanze kwa vitendo yeye mwenyewe huku akiwa na imani kuwa ataweza kwa msaada wa Mungu kwani hana linalomshinda endapo mhusika ataamini. Kubadili tabia ni safari hata kama umeokoka.

Mkuu unaweza kuwa uko sahihi mimi pepo na roho wachafu huwa na waweka kapu moja na nina hasira sana nao hata sasa washindwe kwa jina la Yesu Kristo wa Nazarethi.

Hata hivyo kwa vile mimi ni kuhani na mfalme lazima nimuombee na Bwana atatenda...nimeona wengi amewarehemu.
 
hilo la wafanyakazi kukaripiwa sidhani kwama liko kwako peke yako nahisi ni wanawake wengi huwa na tabia hizo,coz wao hawna usemi wjuu yenu coz nyie ndo mabosi wao so hasira zenu mnawamalizia wao mi nahisi kitu cha kwanza ni kuwapa upendo na kuwafanya wao ni part ya familia kwa kufanya hivyo kidogo utagundua umuhimu wao,cha pili kuhusu kupunguza hasira mi nakushauri kama umekassirikiana na mmeo cha kufanya toka nyumbani nenda kwa mashoga zako mpige stori usikae nyumbani tu ila msipige stori za ugomv na mmeo bali nyingine hii itapunguza walau kumuwaza mmeo na kukumbuka jinsi gani mlivyogambana by the way ugomvi katika ndoa sio mzuri uwe unjaitahidi kuepusha ugomvi kwa gharama yeyote na ikiwezekana hata ujishushe mbele ya mumeo ili uepeushe mikwaruzano sometimes hata kama kosa likiwa lake ikifikai hatua mwanaume anapachukia nyumbani anataka kuja kulala tu hiyo ni hatari
 
Itabidi nitengeneze music room maana pia napenda mziki hasa dancing kwasababu ukiwa umekorofishana na mume halafu ukisema unaenda mziki mahali kucheza ugomvi utakao zuka hapo balaa, thanks much best.

Ni kawaida, kinachotokea ni kwamba automatically nafsi yako imejiwekea ukomo wa ugomvi/malumbano na mumeo!! Ila hasira bado zinaendelea kuwepo moyoni so zinaishia kwa wale wanaojipendekeza mbele yako ilhali ni wanyonge kwako au kwa ni kwamba una uwezo wa kuwakabili bila mipaka.

Inachotakiwa tafuta mkabala wa hasira zako, kama mumeo anamalizia kwenye pombe basi wewe unaweza kumalizia kwenye music, games au kucheza na watoto.

Mie huwasipendi ugomvi, mke wangu akinikwaza hasira namalizia kwenye music kama sina mpango wa kutoka au ndo nimerudi home!! Nafungulia music mzito sana then natulia zangu tu baada ya muda hasira zinakuwa zimeisha hasa kuna aina ya nyimbo nikisikiliza especially country music.
 
aisee mama si vizuri hivyo unatakiwa msubiri mumeo umuwashie moto nasi watoto aisee ... mimi mama akigombana na baba huwa anatuweka karibu sema ukikosea kidogo unalo kipigo chake na pia alikuwa anatoa angalizo,... tulivyojua mchezo unaendaje aisee tukisikia tu malumbano tunaanza kujipendekeza kwa mama
moto kuuwasha kwa mume tena huku mshagombana inakuwa ngumu maana hata kuongea unaona kero kama si kumuona, tatizo watoto wakijipendekeza ndo inakuwa balaa bora wakae mbali maana akikaa karibu hata anapita tuu unaweza jikuta umempiga bao na kumwambia kwa nini unatembea kama goi goi tembea vizuri, yaani ni tabu tupu
 
inawezekana ndugu, mie hunitokea lakini nowadays nimeipatia jawabu ni kujifungia ndani tu hata chakula nalia chumbani, ila siku hiyo nyumba nzima wanajua mama hayuko sawa
 
mh kwa imani yako ni bora ukikasirishwa upige magoti umsihi mungu wako akupe busara ya kuhimili hali hiyo
 
mara nyingi siku ikiisha na hasira zinakuwa zimeisha kwa watoto na wengine ila linabaki moyoni tuu kulimaliza na mume wangu siku ya siku tukiliongea ila hadi huwa nawaonea huruma watoto wanavopata mkong'oto bila hatia ila najikuta tuu nshawapiga na kuwagombeza. Najitahidi sana kutulia na kudhibiti hasira
jitahidi sana, ulie mwenyewe sio watoto tafadhali, vinginevyo unawafunza vibaya watoto, saikolojia ya watoto inatuambia hivyo....
 
Jaribu Kukaa Na Utulie In Short Upumzishe Akili Na Kingne Uskae Na Karbu Watt Utakuja Uwauwe Bure
 
Yaani sijui kwa nini huwa inakuwa hivi, inafahamika kuwa wamama ndo wako karibu sana na watoto na watoto wakiwa na shida ni rahisi kuzipeleka shida kwa mama kuliko kwa baba sasa inapokuja kwenye hasira si kuwa mama anakuwa anawachukia watoto ni kuwa ile hasira naona kama na wao wamechangia baba yao kuniudhi sijui kunakuwa na hormoni gani ambayo inapeleka hasira hivi, natamani ingekuwa hasira irudi kwa mume lakini huwa haiko ivo..... inaudhi sana kwa kweli
ubaya ndo huo na tunakuja kuelewa ukubwani ila utoton tunaona mama katoa adhabu kubwa kuliko kosa lililofanywa. Inabid ukiudhiwa mtoto ndo awe faraja na siyo kitolea hasira. Jitahid sana mamie mkunde kujizuia
 
Last edited by a moderator:
moto kuuwasha kwa mume tena huku mshagombana inakuwa ngumu maana hata kuongea unaona kero kama si kumuona, tatizo watoto wakijipendekeza ndo inakuwa balaa bora wakae mbali maana akikaa karibu hata anapita tuu unaweza jikuta umempiga bao na kumwambia kwa nini unatembea kama goi goi tembea vizuri, yaani ni tabu tupu

aisee mama duh! punguza stress bwana kataa hiyo hali
 
Habari zenu wote kwa mpigo,
Hope mu wazima, hamjambo, mmeamka salama na mnaendelea na shuhuli za kutafuta shekeli kama si kulijenga taifa na kuleta maendeleo kwako binafsi au kwa familia.

Nina shida moja ambayo ningependa niiongelee hapa na kila mtu aiongelee jinsi yeye inavomtokea.

Nimekuja kugundua siku nikiwa na hasira au nimegombana na mume wangu basi hasira zitaishia kwa watoto na watu wote walioko nyumbani like housegirl, house boy, ndugu ndugu tunaokaa nao basi kila mtu akinikalia vibaya siku hiyo ntambwatukia hata kwa kosa dogo tuu.

Nimejiuliza bila sababu, hii imejirudia tena jana, tumerumbana na mume wangu na kupishana kiswahili kila mtu akawa busy na mambo yake yeye baada ya kurudi home anaenda zake kupata moja mbili akirudi anaoga anakula ana lala mie sasa siwezi enda baa na kukaa nakuwa home basi siku hiyo hasira zile nikikuta mtoto hajafanya home work ni kufinywa hadi wanakoma, ambae hajabrush viatu vya shule kwenzi, ambae hajapanga kabati lake au nimekuta nguo zake hazijakunjwa kabatini mabao yaani ni full kugomba.

Nikiingia jikoni nikikuta kosa dogo tuu dada ntamsema na kumgombeza hadi najistukia. Yaani najikuta nagomba na kila mtu ndani hadi naingia kulala kila mtu nae ndani analala na hasira.

Hivi na nyie wenzangu huwa inawakumba hii? Nimejiuliza maana hata wakati niko mdogo kuna siku mama alikuwa anagomba bila hata kuelewa sababu ni nini, sasa nikirecall na hii inayonitokea ndo naanza kuelewa inawezekana na yeye alikuwa anakasirishwa na baba na maybe nimejikuta nimekopi hiyo hali. Wewe huwa inakutokea hii hali? unaikabili vipi? Kibinafsi siipendi nataka hasira isiende kwa wengine ila najikuta tuu.
Karibuni tusaidiane na siku njema.

Jifunze kutafuta amani kwa kusuluhisha na kupatana na mwenzako. Si waju dhambi ikipata upenyo inazaa vitu vingi?
 
Tuko wengi, hata mie ni hivyo hivyo, mie hata mtu akinipigia simu nitambwatukia mbaya, so hata simu huwa sipokei

watoto ndo kipigo, wengine ni kugombezwa, mume wangu inaishia kurumbana tuu na hapo tunaposhindwa kuelewana ndo hasira inamalizikia kwa wengine huku chini
 
Kwa upande wangu nimejaliwa sina hilo tatizo

Ila kwa asilimia kubwa nimeona wengi sana anapokuwa na hasira zake baada ya kuzimaliza kwa aliemkasirisha anaenda kuzimalizia kwa ambao hawajamfanyia lolote baya

Na mara nyingi wanapokuwa wamevurugwa hasira zao wanazitoa kwa makelele(wanapayuka) unaweza stuka kuna nini hapa
 
Back
Top Bottom