Hivi ni kwa nini inanitokea hivi...

Hivi ni kwa nini inanitokea hivi...

Kweli kabisa mkuu, yaani unaweza ukagomba, ukapayuka hadi watoto wakakushangaa na kujishangaa mwenyewe, huwa najitahidi kuicontol hii hali baut nashindwa kabisa, hata nikisema nitoke kwa muda but baadae lazima tu nirudi home so hali inarudi palepale

Kwa upande wangu nimejaliwa sina hilo tatizo

Ila kwa asilimia kubwa nimeona wengi sana anapokuwa na hasira zake baada ya kuzimaliza kwa aliemkasirisha anaenda kuzimalizia kwa ambao hawajamfanyia lolote baya

Na mara nyingi wanapokuwa wamevurugwa hasira zao wanazitoa kwa makelele(wanapayuka) unaweza stuka kuna nini hapa
 
Kweli kabisa mkuu, yaani unaweza ukagomba, ukapayuka hadi watoto wakakushangaa na kujishangaa mwenyewe, huwa najitahidi kuicontol hii hali baut nashindwa kabisa, hata nikisema nitoke kwa muda but baadae lazima tu nirudi home so hali inarudi palepale
Najua ngumu sana kwa upande wako kuepukana na hali hiyo sababu necha ndio inayofanya kazi hapo, inakuwa ngumu sana kuiepuka ila jitahidi tu

Jitahidi mkuu halafu inaelekea wewe upo karibu sana na Mungu(mtu wa dini) jitahidi uwe unasali (usiwe mbali na biblia yako) unapokuwa katika hali kama hiyo
 
watoto ndo kipigo, wengine ni kugombezwa, mume wangu inaishia kurumbana tuu na hapo tunaposhindwa kuelewana ndo hasira inamalizikia kwa wengine huku chini
Ukishajiona una hasira namna hiyo jiweke mbali na kila mmoja hata kama kuna kitu unataka kuelekeza ahirisha fanya siku nyingine. Hasira humtokea kila mmoja wetu ktk maisha lkn tunatofautiana namna tunavyohandle. Jitahidi kukaa mbali na watoto au jipumzishe chumbani kwako usitoke mpaka utakapojiona uko sawa iwapo hasira zako hudumu kwa siku moja. Kama hudumu zaidi ya siku moja basi jitahidi kutouliza chochote hata kama unaona kuna makosa. Nakumbuka niliwahi kuweka mkakati wa kuto adhibu mtoto nikiwa na hasira wala kuuliza chochote kwa hg pindi nijionapo na hasira badala yake huwa nakaa chumbani na kujifanyia mambo mengine.
 
Mtu ukijigundua wapi unakosea ndipo unakuwa unafaham jinsi ya kujisahihisha,sasa wewe umejua wapi unakosea af unajiuliza tena baada ya kufikiria nini ufanye ujiweke sawa...
 
Umeleta mada nzuri sana..! Kwanza mimi siyo mwanamke, tuwekane sawa hapo kwanza!

Nimeoa na mada yako imenigusa sana kwa kuwa hali uliyoisema huwa naiona kwa mke wangu; tukiwa tumetofautiana kidogo tu zogo utalisikia kwa wadada wa kazi na watoto. Hapo mimi nakuwa karibu na mtoto wetu mmoja ambaye mara nyingi anakuwa victim of the prevailing atmosphere! Utasikia wewe nanilii umeshaandaa nguo zako za shule za kesho, homework umeshafanya?, chumbani kwako umepanga?, n.k., hapo kipigo kinakuwa karibu sana, sasa hapo inabidi kukaa jirani kumwepusha na kipigo kisicho cha lazima!

Pili kazini pia kama una boss mwanamke, utagundua tu kama nyumbani hakuko sawa; kiujumla akina mama mlio katika ndoa jifunzeni kutenganisha ugomvi wako na mumeo tena bedroom na watu wasiohusika iwe kazini au nyumbani.
 
pole mkuu
ila ningekushauri kuwa jitahidi kuwa mtu wa maombi itasaidia kuondokana na tatizo hilo
kwani ukimshirikisha Mungu ataliondoa tatizo la kugomba kila wakati utakuwa mtu mwema
hivyo jitahidi ukiona hiyo hali inakujia fanya sala kwani hiyo roho na inajitahidi kukumeza
hivyo wewe jitahidi kuomba uvipige vita vya imani utashinda.
 
Mpaka wanao wajue kuwa mmegombana! Hakikisha kila mkigombana mnapiga gemu, problem litakuwa solved!
 
Sure, siku nyingine najifungiaga rum, naweka nyimbo za dini nafungulia kwa sauti kubwaaaa, angalau napata relief

Najua ngumu sana kwa upande wako kuepukana na hali hiyo sababu necha ndio inayofanya kazi hapo, inakuwa ngumu sana kuiepuka ila jitahidi tu

Jitahidi mkuu halafu inaelekea wewe upo karibu sana na Mungu(mtu wa dini) jitahidi uwe unasali (usiwe mbali na biblia yako) unapokuwa katika hali kama hiyo
 
Back
Top Bottom