Hivi ni kwa nini inanitokea hivi...

Hivi ni kwa nini inanitokea hivi...

Kisirani cha ugomvi kati ya mume na mke ni kibaya sana. Wengine huwa wanaenda navyo kazini, kibaruani hata barabarani unakuta anabwatuka tu. Ndio pale unakuta nesi anachoma sindano kama ugomvi, mwalimu anachapa kama anapiga ng'ombe, boss anaropokea wafanyakazi na wafanyakazi wanaropokea wateja.

Nwy, maadam umeshagundua tatizo lako kila unapokuwa na hasira na mumeo fikiria kwamba yeye pekee ndio anaestahili hiyo hasira. Ukijikuta unataka kugomba na mtu mwingine bila sababu ya msingi vuta pumzi ufikirie jinsi ambavyo unakuwa unfair. Usiruhusu hasira za chumbani zikuendeshe nje ya chumbani. Mume wako ye ni mjanja maana anakuacha wewe umevimba nyumbani ye anaenda kucheka zake bar. Kwa ufupi ni kwamba yeye anajipa ahueni, wewe unazidi kufura na ndio maana anakuignore maana yeye hahitaji mazungumzo ya kutulizana baada ya ugomvi, tofauti na wewe.

Acha kisirani. Mkizinguana fanya kitu unapenda. Sio lazima na wewe uende bar. Nenda katembee hata kwa rafiki au ndugu (usizungumzie ugomvi wenu), nenda kaangalie movie au shopping kama hela inaruhusu, kale out n.k. Nyumbani kuwa karibu na watoto wako as if hamna tatizo. Usiwafanye wawe victims wa kisirani ambacho hawajahusika kukupa. Cheka, furahi, ongea nao, cheza nao. Hata mume wako akirudi akakuta una furaha na mlikorofishana earlier atabaki kukushangaa tu. Kama ni kuonyesha kisirani onyesha chumbani.

Jifunze kutokuonyesha waziwazi matatizo yako ya ndani. Sio vizuri kila mtu ajue leo mama/bosi/shoga ndani kwake kumewaka moto.
 
ni kawaida kwa wengi.ila jitahidi kushusha hasira.control your thought.

najitahidi kuondoa hasira shida mazingira yanajikuta tuu ushatembeza mkong'oto mkali kwa kosa dogo tuu na maneno makali yasiyoisha kwa kitu amabcho hakikustahili hata kugomba. Najitahidi lakini maana siipendi hii hali, thanks.
 
nakumbuka kuna siku nlipata kipigo na mama kwa sababu isiyo eleweka wakati huo baba alikuwa anataka kuoa mke wa pili, nyumba ilikuwa ya moto aisee. Sijaolewa bado ila najua hiyo inatokea 'ukipata mbabe wako, hasira zaishia kwa mnyonge wako'

Yaani sijui kwa nini huwa inakuwa hivi, inafahamika kuwa wamama ndo wako karibu sana na watoto na watoto wakiwa na shida ni rahisi kuzipeleka shida kwa mama kuliko kwa baba sasa inapokuja kwenye hasira si kuwa mama anakuwa anawachukia watoto ni kuwa ile hasira naona kama na wao wamechangia baba yao kuniudhi sijui kunakuwa na hormoni gani ambayo inapeleka hasira hivi, natamani ingekuwa hasira irudi kwa mume lakini huwa haiko ivo..... inaudhi sana kwa kweli
 
From no where tu mtu anakuomba hela wakati umefulia!
Na ukiwa na hela hawaji. U feel completely useless na lazima huyo mtu alipe!
Ukigombana na mmeo, we jipe outing tu, hugombani na mtu. Jipeleke movie/dinner/music n.k na friends, basi maisha barida kabisa.

Mie hugomba nikiwa sina hela, afu mtu ananiomba hela kihasara hasara tu.
 
Dawa ya hasira n serious tears..

Jifungie room kwako, cry as much

then, ukishapoa, wash your body,

have a smooth air!

Usipofuata hiyo procedure, basi yatatokea hayo yanayotokea kwako!

Learn from developed people!
 
" muwe na hasira ila msitende dhambi" halafu jua lisizame hasira haijaisha
Muombe mungu akusaidie katika hili.
 
Umeshagundua tatizo...hence problem solved.!
 
yahitaji uvumilivu kiasi, na ikiwa sasa hivi umejigundua unatatizo basi ndio mwanzo wa kuisha hilo tatizo, je hiyo hali inakwisha baada muda gani...?
lakini cha msingi nikutulia ili uweze kumudu hizo hasira, waweza kuja kufanya kitu kibaya zaidi....
mara nyingi siku ikiisha na hasira zinakuwa zimeisha kwa watoto na wengine ila linabaki moyoni tuu kulimaliza na mume wangu siku ya siku tukiliongea ila hadi huwa nawaonea huruma watoto wanavopata mkong'oto bila hatia ila najikuta tuu nshawapiga na kuwagombeza. Najitahidi sana kutulia na kudhibiti hasira
 
uzuri ni kwamba ushalijua tatizo basi ukiona hali hiyo inaanza kamata biblia kama wewe ni mkristo tafuta somo linalozungumzia upendo na jinsi tunavyotakiwa kuwatendea wengine katika kila hali itakuwa inakuondelea hiyo hali

asante ntafanya hivo
 
pole dada. kwanza usikubali hasira zi kutawale bali zitawale wewe. Ukiona una asira jaribu kufunya kazi ambayo itakufanya uchokw hiyo siku au fanya mazoezi uchoke ili uondo mawazo ya ugomvi wako na mumeo.

Pili. Ukigombana na mumeo au mtu yoyote, usijibishane naye
jaribu kujifanya wewe umekosea na kuomba msamaha hata kama aujakosea.
nimekuja kugundua pia tatizo liko hivi, unakuwa umerudi na hasira zako ambazo mmegombana na mume, huku ukiwa umefura mtoto anapita analia lia bila sababu ukimnyamazisha hasikii analilia kitu ambacho hawezi kukipata usiku huo mara dada anakwambia usiku huo mchele umeisha au sukari imeisha au sabuni ya kuogea watoto haman hata ya kuwaogeshea asubuhi hamna, hapo napandwa na hasira zaidi kwa nini hukusema mapema nikanunua, kwanini zinakuwa kwa nini basi ni kugomba hadi saa ya kulala.
Asante najitahidi sana nisimalizie hasira kwa watoto kwani baadae najikuta nawaonea huruma.
 
Hebu jaribu na hiii wewe nenda kaombewe tu ni roho ya hasira itaondoka na utakuwa mwamke mpole mwenye furaha daima.".....lile ninalotaka kulitenda silitendi na nisilotaka kulitenda ninalitenda ni kwa sababu ya dhambi inayokaa ndani yangu"

asante ntalifanyia kazi hili, hata nawe niombee pia na jumapili hii ntaenda nikaombewe pia maana ni hali inayonikera kwa kweli.
 
Pole dada. Ni tatizo la kawaida nadhani wenyewe wanasaikolojia wanaita "anger projection". Unapeleka hasira zako kwa wanyonge wako. Halina uhusiano na umri - hata mtoto mdogo akiudhiwa na mamake anaweza kwenda kupiga paka mateke. Mimi pia nimeshajigundua nina tatizo hili hata kama sijaudhiwa na mtu. Nikiwa na mawazo hata ya hela tu wananikoma huko ndani. Baada ya kujua, dalili zikianza nawapa tahadhari wakae mbali na mimi, waniache nitafakari mambo yangu, mara nyingie natoka nje ya nyumbani, nikirudi niko fresh. Nimejifunza pia kuomba msamaha hata kwa mtoto wangu maana hasira zikishaisha nikitafakari mambo niliyowafanyia naona aibu na huruma. Kila mtu ana jinsi yake ya kudhibiti hasira. Waweza ku-google kuhusu "anger management".
 
Mimi hii nimeiexperience tofauti. Mama yangu mlezi ni mwalimu wa shule ya msingi. sasa term atakayopangiwa kufundisha watoto wa madarasa ya chini kama la kwanza mpaka la tatu basi siku wanafunzi wake wakimvuruga huko shule basi hasira zitaishia kwa watoto nyumbani. Akipangiwa madarasa ya juu kiasi huwa anakuwa yupo kawaida sana,,,,,,,
 
Yaani sijui kwa nini huwa inakuwa hivi, inafahamika kuwa wamama ndo wako karibu sana na watoto na watoto wakiwa na shida ni rahisi kuzipeleka shida kwa mama kuliko kwa baba sasa inapokuja kwenye hasira si kuwa mama anakuwa anawachukia watoto ni kuwa ile hasira naona kama na wao wamechangia baba yao kuniudhi sijui kunakuwa na hormoni gani ambayo inapeleka hasira hivi, natamani ingekuwa hasira irudi kwa mume lakini huwa haiko ivo..... inaudhi sana kwa kweli
ba nso 09:35 Today
kwani ushafikia menopause? tuanzie apo
 
Ukigombana na mmeo, we jipe outing tu, hugombani na mtu. Jipeleke movie/dinner/music n.k na friends, basi maisha barida kabisa.

Mie hugomba nikiwa sina hela, afu mtu ananiomba hela kihasara hasara tu.

tatizo mazingira hayaruhusu, kama jana jioni ndo nimegombana na mumewangu sasa kufika home yeye kabadili katoka zake kupata mbili tatu walau hasira zake zinakuwa zimepoa anarudi anakula analala, mie sasa siwezi usiku huo kuanza kutoka out naanzia wapi, na isitoshe siku inayofuata ni siku ya kazi, nikienda dinner mwenyewe naanzaje kuaga na ndo utakuwa mzozo mwingine kwanza jinsi tulivorumbana hata hutaki kuanza kumuongelesha kuwa mie naenda out dinner au muvi.
Hilo la kuombwa hela ukiwa huna hela nalo lishanikuta sana au unakuwa na matatizo ya kusolve yanayohitaji hela halafu huna hela yaani huwa nakuwa mkali bila sababu kitu chochote hata mtu akichana tambara la deki home nawaka kuwa unapoteza hela kuharibu tambara la deki sijui kwa nini yaani natamani nikiwa na hasira watu wajue wasinisonge ili nisiwamwagie hasira zangu.
Itabidi mjengo wangu ninaojenga niweke dancing floor home ili nikiudhika naingia room ya dancing najifungia naweka sound proof nafungulia mziki hadi mwisho nikitoka huko hasira zimeisha looh
 
Wengi hua tupo hivyo ni kujizuiaa tu uwe unakunywa maji mengi au unaenda unalalaaa tu kuepusha msongamano halaf hayo makwenzi uwe unayamalizia chumban na mumeo banaa
 
Hasira hasara. Usikubali hasira zako zikutawale, unaweza kufanya watoto wako ndio wakusaidie kukuondolea hasira, mimi kwangu watoto ndio wanaoweza kuniondolea stress, watoto hawachoshi
 
He he he, nikiwa nazo za ziada waniombe ama wasiniombe, lazima wapate cheche za hela. Full shoping ndogondogo, vicheko mia mia, ushirikiano wa siafu haunikuti.

From no where tu mtu anakuomba hela wakati umefulia!
Na ukiwa na hela hawaji. U feel completely useless na lazima huyo mtu alipe!
 
Back
Top Bottom