Mkunde Original
JF-Expert Member
- Jul 20, 2013
- 807
- 647
Habari zenu wote kwa mpigo,
Hope mu wazima, hamjambo, mmeamka salama na mnaendelea na shuhuli za kutafuta shekeli kama si kulijenga taifa na kuleta maendeleo kwako binafsi au kwa familia.
Nina shida moja ambayo ningependa niiongelee hapa na kila mtu aiongelee jinsi yeye inavomtokea.
Nimekuja kugundua siku nikiwa na hasira au nimegombana na mume wangu basi hasira zitaishia kwa watoto na watu wote walioko nyumbani like housegirl, house boy, ndugu ndugu tunaokaa nao basi kila mtu akinikalia vibaya siku hiyo ntambwatukia hata kwa kosa dogo tuu.
Nimejiuliza bila sababu, hii imejirudia tena jana, tumerumbana na mume wangu na kupishana kiswahili kila mtu akawa busy na mambo yake yeye baada ya kurudi home anaenda zake kupata moja mbili akirudi anaoga anakula ana lala mie sasa siwezi enda baa na kukaa nakuwa home basi siku hiyo hasira zile nikikuta mtoto hajafanya home work ni kufinywa hadi wanakoma, ambae hajabrush viatu vya shule kwenzi, ambae hajapanga kabati lake au nimekuta nguo zake hazijakunjwa kabatini mabao yaani ni full kugomba.
Nikiingia jikoni nikikuta kosa dogo tuu dada ntamsema na kumgombeza hadi najistukia. Yaani najikuta nagomba na kila mtu ndani hadi naingia kulala kila mtu nae ndani analala na hasira.
Hivi na nyie wenzangu huwa inawakumba hii? Nimejiuliza maana hata wakati niko mdogo kuna siku mama alikuwa anagomba bila hata kuelewa sababu ni nini, sasa nikirecall na hii inayonitokea ndo naanza kuelewa inawezekana na yeye alikuwa anakasirishwa na baba na maybe nimejikuta nimekopi hiyo hali. Wewe huwa inakutokea hii hali? unaikabili vipi? Kibinafsi siipendi nataka hasira isiende kwa wengine ila najikuta tuu.
Karibuni tusaidiane na siku njema.