Hivi nani mwingine anakereka na hili swali toka kwa wife?

"Bebi Leo tunakula nini?"

Hivi chakula nimenunua, Maharage, mchele, unga, viazi, nyama, samaki vyote viko kwenye kitchen Den na kwenye friji kuna kila kitu.

Sasa kwanini uniulize tunakula nini? Wewe huwezi kujiongeza kweli kufanya assortment ya chakula cha kupika.

Kwa mama n'tilie ilikuwa ukifika tu unaletewa directly msosi wa siku ?

Wapumzisheni wake zenu na malalamiko, hamkosi cha kulaalamikia.
 
Kuwaza Cha kupika huwa ni kazi ngumu hata kukiwa na kila kitu, nakumuuliza mume nikujua anapenda nini kipikwe nisije kupika kitu asichokipenda. So kusaidiana mawazo kuhusu msosi ni Jambo zuri na linapunguza mzigo kwa mpigaji na njia rahisi ni kuwa na ratiba ya msosi
Hiv wale tunaokula chochote kilichopikwa huwa tunakosea wapi?
 
"Bebi Leo tunakula nini?"

Hivi chakula nimenunua, Maharage, mchele, unga, viazi, nyama, samaki vyote viko kwenye kitchen Den na kwenye friji kuna kila kitu.

Sasa kwanini uniulize tunakula nini? Wewe huwezi kujiongeza kweli kufanya assortment ya chakula cha kupika.
Mimi bado sijaoa lakini asije jichanganya kuniuliza hivyo maana;
Sili nyama ya aina yoyote sasa atakula maharage daily maana ndio mboga yangu namba 1 niwe na hela au nisiwe nazo.
 
🤣😂😂 Nilijua ni mimi tu nakereka na ili swali kumbe tupo wengi, wife anajua mi ni mpenzi wa pilau na supu au michemsho ila lazima daily aulize na anajua lazima nichague kati ya hivyo vitatu
 
Mimi kero yangu nyingine pamoja na hiyo ya kuuliza chakula, ni kulala kwenye kochi na kunilalia kila napo ka karibu nae duh, hawezi kuangalia move au tv bila kulalia sofa, inakera arafu huwezi kumkemea atasema hooo! you ur not romantic, wanaumme hampendeki nk..........inekera sana plz wake zetu regulate your habits plz
tabia mbaya tu, sasa tukadeke wapi jamani...!
 
kweli aliyesema binadamu hatuna chema hakukosea kabisa. Sasa mkuu kuna ubaya gani kuulizwa hivyo aisee. Si unamjibu tu unachojisikia kula siku hiyo kaka. Tena kakuuliza kimahaba kabisa aisee.

Laiti ungejua kiasi cha raia kisichoulizwa hayo maswali na wanaombea kiasi gani waulizwe!
Raha ya chakula ufanyiwe assortment na mke! Tatizo wake zetu wengi sio wabunifu nakumbuka marehem mama alikuwaga na cook books kabisa yani na alikuwa na hobby ya kupika basi anajipikilisha wee! Sasa kutana na hivi vizazi vya chips kuku yani wao nje ya wali, ugali na pilau hana anachojua😅
 
Moyo usio na shukrani unachukia kila kitu, kama unakereka mjulishe kwamba mke wangu we unachokitaka tule siku hiyo ndio upike me nitakipenda tu, maana wenyewe hapo mara nyingine mnakuja kusema wake hawajiongezi, kumbe anapokuuliza maana yake mkeo kajinyima ili ale we unachokipenda, machaguo yake kayaweka pembeni, halafu unatuambia swali hili hulipendi, inaonyesha ume mu underestimate mkeo kwa mengi sana, acha huo utoto. Kama hajapika kwa wakati anakusubiri that means wewe ni mlalamishi huna mwelekeo kwamba huwa unapenda nn kula
Hamna wala sio ulalamishi! Ni uvivu wake wa kufikiri tu mie hata akipika mavi ntakula tu sababu ndio chakula chetu cha siku hio!

Anajua fika sipendi mchicha na kabeji😅!

Hayo mengineyo akipika haina shida. Sema uliza mara moja moja we kila siku unauliza tu hujui kuwa ni kero? Mwanaume raha upikiwe bana ukifika we ni kusifia tu leo mke wangu pishi tamu sana😅 sio unafika unaanza kumenyeshwa vitunguu swaumu!
 
Sasa wangu mi hapendi kabisaa ugali anapenda tuu ndizi za kwao Marangu. So mkipika ugali na ndizi zake ziwepo.Hakuna kitu kigumu kama kuwaza una pika nini aisee ni kazi ngumuu

Jamaa anaonekana wa ajabu sana. Yani anachukia ugali hao ndio wale daddy im going!

Ukiwa huna hobby ya kupika ni kazi ngumu kweli! Ila if you are creative there are a million dishes yani! Na vitu ni vile vile tu ila unatwist kidogo tu unapata new dish. Unaongeza kidogo inakuwa kitu amazing.

Nunua vijarida vya mapishi vitakusaidia kuto run out of ideas! Mie sijui tatizo nina dada anapenda mapishi yani nikifikaga kwa shemeji yangu namuonea wivu anavyopikiwa vitu vizuri vizuri yani kama yuko 5 star hotel😂😂😂
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom