Hivi na hawa hawaendi mbinguni?

Ujio wa Yesu na kazi Ya msalaba inajibu swali hilo kwamba na wao wanafika mbinguni kwani roho ya yesu ilishuka kuzimu na huko ilifanya kazi tatu,mosi kuwahubilia walioko kule yaani waliokufa toka wa kwanza mpaka yule aliyekufa pamoja naye,pili kunyang'a mamlaka ya shetani ambaye alimiliki roho hizo na tatu ni kuuwa kifo kwa kuwaunganisha na mbingu kwa wao kwenda na yesu Mbinguni
Yesu aliposhuka kuzimu alichukua muda wa siku ngapi kuwahubili watu waliokuwa huko kuzimu???
 
Kama hawajawahi kupata habari za dini sahihi na uwepo wa mola Muumba watasamehewa ila kama walipata kupata kuambiwa basi hawatasamehewa.
kuambiwa na wale waliokuja kufanya biashara za utumwa au kuambiwa na nani maana kulikua hkuna technolojia ya kupata taarifa
 
15. Anaye ongoka basi anaongoka kwa ajili ya nafsi yake. Na anaye potea basi anapotea kwa khasara yake mwenyewe. Wala habebi mbebaji mzigo wa mwengine. Wala Sisi hatuadhibu mpaka tumpeleke Mtume.(QURAN 17:15)
6. Na kwa yakini tutawauliza wale walio pelekewa Ujumbe, na pia tutawauliza hao Wajumbe.(QURAN 7:6)

KUNA WALIOFIKIWA NA MITUME/UJUMBE WA MUNGU MMOJA LAKINI......
87. Na hakika tulimpa Musa Kitabu na tukafuatisha baada yake Mitume wengine. Na tukampa Isa, mwana wa Mariamu, hoja zilizo waziwazi, na tukamtia nguvu kwa Roho Takatifu. Basi kila walipo kufikieni Mitume kwa yale ambayo hayapendwi na nafsi zenu, mlijivuna; wengine mkawakanusha, na wengine mkawauwa.(QURAN 2:87)

WALIO FIKIWA NA UJUMBE WAKAPINGA KWA NAMNA MBALIMBALI(KUKUFURU)
49. Na wale waliomo Motoni watawaambia walinzi wa Jahanamu:Mwombeni Mola wenu Atupunguzie siku moja ya adhabu. 50.Watasema: Je, hawakuwa wanawafikieni Mitume wenu kwa Ishara zilizo wazi? Watasema: Ndiyo! Watasema:Basi ombeni(wenyewe). Lakini maombi ya makafiri hayawi ila kupotea bure.(QURAN 40:49-50)
8.Karibu upasuke kwa hasira. Kila mara litakapotupwa humo kundi walinzi wake watawauliza: Je, hakuwafikieni Mwonyaji?9.Watasema: Naam! Alitufikia Mwonyaji, lakini tulikadhibisha na tulisema:Mwenyezi Mungu Hakuteremsha chochote, ninyi hammo ila katika upotevu mkubwa.(QURAN 67:8-9)

MWISHO NIKWAMBA
44. Hakika Mwenyezi Mungu hawadhulumu watu kitu chochote; lakini watu wenyewe wanajidhulumu nafsi zao.(QURAN 10:44)
281. Na iogopeni Siku ambayo mtarudishwa kwa Mwenyezi Mungu, kisha kila nafsi italipwa ilicho chuma. Nao hawatadhulumiwa.(QURAN 2:281)
25. Basi itakuwaje tutakapo wakusanya Siku ambayo haina shaka kuja kwake? Na kila nafsi italipwa kama ilivyo chuma, bila ya kudhulumiwa.(QURAN 3:25)
17. Leo kila nafsi italipwa kwa iliyo chuma. Hapana dhulma leo. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwepesi wa kuhisabu.(QURAN 40;17)
NA ALLAH ANAJUA ZAIDI
 
1Petro 4:6 Maana kwa ajili hiyo hata hao waliokufa walihubiriwa Injili, ili kwamba wahukumiwe katika mwili kama wahukumiwavyo wanadamu Bali wawe hai katika roho kama Mungu alivyo hai.
 
Dini ni kuamini kuna Mungu/miungu (uislamu, ukristu, ubuddha, ushinto etc).
Imani ni njia ya kumuamini Mungu/miungu (Muhammad SAW, Yesu, Buddha, Bahaulah etc).

Labda mnapowahukumu mababu wa kiafrika kwamba walikuwa wajinga kufanya tamaduni za Miungu yao tofauti na Mungu wa Kizungu, mjiulize je mababu wa kizungu ambao hawakumjua Mungu wao nao itakuaje (mwaka 1 AD kurudi nyuma)!?..
Wewe kwenye definition ya dini umeweka Imani, and vice vesa
 
Wewe kwenye definition ya dini umeweka Imani, and vice vesa
"Imani yako itakuokoa" unaielewaje hii sentensi!?.
Au Yesu aliposema "ukiwa na Imani kama punje ya haladari utaweza hamisha mlima" uliielewaje!?.
 
"Imani yako itakuokoa" unaielewaje hii sentensi!?.
Au Yesu aliposema "ukiwa na Imani kama punje ya haladari utaweza hamisha mlima" uliielewaje!?.
Wote tunaweza tukawa na imani ya Mungu mmoja, lakini namna ya kumuabudu huyo Mungu mmoja ndio tunakuwa na dini tofauti..
 
Ni kwa muda mrefu sana nimekuwa nikijiuliza hivi mababu zetu waliokuwepo kabla ya dini zetu kuu yaani ukristo na uislamu haujaingia nchini wataenda mbinguni?
Maana kwa asilimia kubwa walikuwa wanafanya matendo ambayo dini zetu zinazuia mathalani...kutoa kafara kwa miungu, kuuana kwa kigezo cha mila na desturi nakadhalika.

Ukiangalia vigezo vingi vya mtu kuwa msafi wa kiimani mengi hawakuyafanya mababu zetu.

Kwa watu wanaojua vizuri mafundisho ya dini naombeni msaada katika hili maana mimi Nebuchadinezzer sina ujuzi katika hili.

ASANTENI.
UKiwa muislamu, wte wasio waislamu ni Motoni. Na ukiwa mkristo, wote wasio wakristo ni Motoni.
ILa sijawahi kusikia kauli kwa MASTAFARI.
Kazi kweli kweli
 
Wote tunaweza tukawa na imani ya Mungu mmoja, lakini namna ya kumuabudu huyo Mungu mmoja ndio tunakuwa na dini tofauti..
Mfano Ulokole, ukatoliki, mashahidi wa yehova ni Imani tofauti au Dini tofauti!?..
 
Ni kwa muda mrefu sana nimekuwa nikijiuliza hivi mababu zetu waliokuwepo kabla ya dini zetu kuu yaani ukristo na uislamu haujaingia nchini wataenda mbinguni?
Maana kwa asilimia kubwa walikuwa wanafanya matendo ambayo dini zetu zinazuia mathalani...kutoa kafara kwa miungu, kuuana kwa kigezo cha mila na desturi nakadhalika.

Ukiangalia vigezo vingi vya mtu kuwa msafi wa kiimani mengi hawakuyafanya mababu zetu.

Kwa watu wanaojua vizuri mafundisho ya dini naombeni msaada katika hili maana mimi Nebuchadinezzer sina ujuzi katika hili.

ASANTENI.
hawaendi hizo sadaka za kimila zipo chini ya mungu wa dunia yaani shetani, waliwezaje kumjua mungu wa giza lakini wasijue kuwa kuna Mungu aliye waumba! hakuna kitu kama hicho!
 
Toka kuumbwa kwa binadamu wa kwanza (Adamu) MUNGU amekua akimuongoza binadamu nadhani Musa ndio mtu wa mwisho kuongea ana kwa ana na MUNGU.
Zip dini nyingi sana dunia hii lakini zote zinamwabudu MUNGU mkuu wa yote.
 
Mkuu nataka kujua vigezo ambavyo vitatumika siku ya kiama kwa mababu zetu ambao walikuwepo kabla kuja kwa hizi dini tulizonazo kwa sasa maana asilimia kubwa mababu zetu walifanya vitu ambavyo ni haramu kwa dini zetu.
MOLA MLEZI hatamuadhibu yeyote ambae mpka anakufa hajafikiwa na mtu wa kumfundisha kumuonya na kumkhabarisha juu ya uwepo wa MOLA MLEZI,, kwahiyo kama huyo Babu unaemsema hajafikiwa na ujumbe huo basi yeye atabakia kuwa salama, je watasalimika wangapi kama hapa kwetu Uislam uliingia tangu Karne ya 7( 7th century)
Je hawakuupata ujumbe? Au waliupata wakaapuuza?
 
Back
Top Bottom