Hivi mzazi anaweza kutoka na mtoto mmoja na kwenda nae matembezi na kuacha wengine.

Msulibasi

JF-Expert Member
Dec 2, 2014
5,837
7,499
Kwa mfano baba au mama anataka kutoka na mtoto mmoja katiks familia kwa ajili ya maongezi maalumu yanayomhusu huyu mtoto. Akaamua kuwa leo fulani tutaenda kutembelea chuo kikuu DSM nyie wengine bakini na mama au baba mama wakatoka na huyo mtoto mlengwa na kuwaacha hawa wengine na house girl itakuwa ni makosa?
 
Hapana si makosa na inawezekana kabisa hasa kama una watoto wa jinsia tofauti.Kwa baba kuspend quality time na mtoto peke ni vyema ili kujenga stronger bond kati yenu!Kwasababu kama mtoto ni mkubwa na kuna mambo mnataka kuongea faragha hatokuwa huru ukiwabeba wote!Mm nina rafiki yangu alikuwa na watoto wawili na nakumbuka kipindi hiko alijifungua si muda mrefu so akawa anatoka baadhi ya siku kuspend muda na mtoto wake wa kike aliyekuwa na umri wa miaka 5 kwasababu anasema attention kubwa inaenda kwa kichanga na yule wa kike anatakiwa asijisikie kama ametengwa au amesahaulika!Girls time ni muhim(mother and daughter) na boys time(father and son)!
 
Correction Fluid we unaonaje?thats a good starting point..

Ninanaona kuna wakati unapaswa kufanya hivyo lakini ni vigumu kulitekeleza hilo nahisi linaleta maswali mengi kwa hawa walioachwa hasa kama hawajazidiana sana umri ama wakati mwingine ni mzazi mmoja ameona anahitaji maongezi na mtoto yeye kama mama ama kama baba . Utanikubalia Tayta kuwa mazingira yanasaidia kuweza kumfanya mtoto aelewe na kuzingatia maelekezo. Mimi naona ni muhimu ila nashindwa kulitekeleza ndo maana nipo hapa . Wakati mwingine kutoka nao wote ni gharama na pia huwezi kudili na objective yako effectively
 
Hapana si makosa na inawezekana kabisa hasa kama una watoto wa jinsia tofauti.Kwa baba kuspend quality time na mtoto peke ni vyema ili kujenga stronger bond kati yenu!Kwasababu kama mtoto ni mkubwa na kuna mambo mnataka kuongea faragha hatokuwa huru ukiwabeba wote!Mm nina rafiki yangu alikuwa na watoto wawili na nakumbuka kipindi hiko alijifungua si muda mrefu so akawa anatoka baadhi ya siku kuspend muda na mtoto wake wa kike aliyekuwa na umri wa miaka 5 kwasababu anasema attention kubwa inaenda kwa kichanha na yule wa kike anatakiwa asijisikie kama ametengwa au amesahaulika!

Umenistua sana mana sababu ya hili swali ni exactly jambo kama hilo tofauti ni huyu mkubwa nikampeleka boarding baad ya ujio wa huyu mpya alipokuwa anarudi likizo alikuwa kama amepata uzubavu na kuchanganyikiwa hakuwa yule. Sasa ukitaka hata kumchangamsha alikuwa anakataa hata vitu alivokuwa anavipend sana nikuletee hiki anasema sitaki jibu lake sitaki ana kaa kimya ama anaenda kujifungia chumbani
 
Ninanaona kuna wakati unapaswa kufanya hivyo lakini ni vigumu kulitekeleza hilo nahisi linaleta maswali mengi kwa hawa walioachwa hasa kama hawajazidiana sana umri ama wakati mwingine ni mzazi mmoja ameona anahitaji maongezi na mtoto yeye kama mama ama kama baba . Utanikubalia Tayta kuwa mazingira yanasaidia kuweza kumfanya mtoto aelewe na kuzingatia maelekezo. Mimi naona ni muhimu ila nashindwa kulitekeleza ndo maana nipo hapa . Wakati mwingine kutoka nao wote ni gharama na pia huwezi kudili na objective yako effectively
si vigumu kutekeleza,kama mzazi kuna mambo magumu na mazito zaidi ya kuyafanyia maamuzi kuliko kuchagua leo utoke na nani na kwa malengo yapi.Usingozwe na hisia za juu ya wengine ulioawaacha watakufikiria nini juu yako.Kumbuka si jambo la kila siku na cha zaidi waliobaki watataka zaidi kufahamu aliyepelekwa kafaidika na nini kuliko anaenda kufanya nini.Ondoa shaka ,watoto wana mengi ya kutokukuelewa kuliko hata hili unalokuwa na wasiwasi nalo...
 
Ok nadhani haitakuwa tabu kwa mzazi anayebaki nyumbani kama mzazi mmoja ameamua kufanya hayo matembezi elekezi ama sivyo ili kama ni mama asimame kama mama na baba hivyohivyo.
 
Umenistua sana mana sababu ya hili swali ni exactly jambo kama hilo tofauti ni huyu mkubwa nikampeleka boarding baad ya ujio wa huyu mpya alipokuwa anarudi likizo alikuwa kama amepata uzubavu na kuchanganyikiwa hakuwa yule. Sasa ukitaka hata kumchangamsha alikuwa anakataa hata vitu alivokuwa anavipend sana nikuletee hiki anasema sitaki jibu lake sitaki ana kaa kimya ama anaenda kujifungia chumbani
Ok ni muhimu utoke nae faragha mkaongee kuna uwezekano ana matatizo huko boarding school kama bullying au even worse.. God forbid what im thinking...ndio maana anajitenga tafadhali ongea nae muhimu hasa watoto wanaokaribia uteengaer au wako kwenye umri wa miaka 10 na kuendelea wanaweza kuwa wanapitia mambo mazito na wanaficha na kukuepuka ww ni njia mojawapo ya kuficha yanayojiri!
 
Nieliweka hili jambo hapa maana ninauzoefu wa kuona jamaa zangu wakipata hii tabu na kusubiri mpaka mtoto anapofunga shule siku ya kwenda kumchukua utakuta mzazi anapita nae pahala ndo anampa yale mambo elekezi-ukiwa maeneo eneo utaona sa nyingine mama analia au mtoto analia baadae wanaingia garini wanaondoka ila shida nadhani ni hiyo ya tuageje nyumbani
 
Back
Top Bottom