BENEDICT BONIFACE
JF-Expert Member
- Aug 31, 2013
- 235
- 396
Kwa dini yangu naamini nikifa roho inaenda mbinguni kwa Mungu.. Mwili unarudi ardhini
hivi roho tumeipata wapi?
Kwa dini yangu naamini nikifa roho inaenda mbinguni kwa Mungu.. Mwili unarudi ardhini
afrika dini tumeletewa je waliokufa kabla ya dini kuja afrika na ambao walikua wanaabudu kwenye miamba walipokufa walienda wapi?
Mwagitho, naona majibu-mzaha yamekuwa mengi. Mie natoa jibu 'serious' ambalo pia ni 'practical', ila nitatumia kiswaenglish. A man has three parts. 1. Body/Mwili, 2. Soul/Nafsi (a soul is a seat of mind+affection+emotion) na 3. human Spirit.
Mwili ni nini?
- Unaufahamu-sihitaji kueleza; ila imeandikwa 'Bwana akafanya mtu toka katika udongo'. Mwili umetoka udongoni. Mtu akifa, Mwili unapelekwa kaburini, 'wewe ni mavumbi na mavumbini utarudi' Mwili ni mchanganyiko wa calcium - mifupani, water-ktk damu na nyama, madini ya chumvi za aina mbalimbali ambavyo vyote vinapatikana udongoni vilipotoka!
Human Spirit ni nini? Ni 'pumzi ya uhai' toka kwa Mungu. 'Bwana akampulizia 'pumzi ya uhai' huyo mtu aliyefanywa kwa udongo, na huyo mtu akawa NAFSI HAI'. Nafsi ni matokeo ya human spirit kuungana na human body.
- Pia 'a spirit' is a person. Huyu 'spirit' akipokea nguvu za ki-Mungu/ki-Yesu na Mungu akitaka, anaweza kumpa uwezo mara mojamoja (occassionally) wa kuona baadhi ya mambo ktk ulimwengu wa roho - the invisible spiritual world, lakini ni kwa lengo maalumu mfano- vita ya kiroho, kuchochea maombi maalumu, etc. Kwenye invisible spiritual world kuna spirits wengine ambao ni non-human; spirits hao ni 1. angels, 2 God (katika utatu wake) na 3 Satan and his demons (shetani na mapepo/majini yake).
Huyu human spirit akipokea nguvu za ki-shetani au ki-pepo-wabaya anakuwa na uwezo wa kuamua mwenyewe kufanya mambo kadhaa mfano: - kuruka usiku akiacha mwili wake kitandani, kinachoruka ni spirit na soul. Pia anakuwa na uwezo wa kusoma nyota, viganja, kutabiri - kwa maana ya fore-telling. Pia wengi wa wanao-advance sana katika Yoga, Kung-fu, Karate, Ninju-tsu, Witchcraft, Mazingaombwe, transcendental meditation, n.k. huwa wamepokea nguvu hizi za ki-pepo. The climax of all these demonic powers ndio akina ILLUMINATI, hasa wale INNER CIRCLE.
Soul/Nafsi ni nini?
Kulingana na bible, soul/nafsi ni matokeo ya kuunganika kwa human spirit na mwili wa udongoni. Bwana alipompulizia 'pumzi ya uhai' yule mtu wa udongo, ikatokea NAFSI. Nafsi nayo 'is a person' ila hawezi kufanya jambo independent of a spirit. Na anasukumwa na spirit mojawapo kati ya 'human spirit or God's spirit' au 'demonic/satanic spirit' Nafsi ndio wewe haswaaa! Nafsi ndio kiti cha 'mind, emotions na affection'. 1 toa 2 unapata ngapi? kinachojibu swali hilo ni soul-mind. Kama wee ni mwanaume unapenda mwanamke mnene au mwembamba? Anayejibu swali hilo ni soul-affection; swali jingine, mtu akikurushia maji machafu ya mvua kwa kuyakanyaga kwa gari lake kwa makusudi saa mbili asubuhi ukiwa njiani kuelekea ofisini/kibaruani, how angry do you become? hiyo hasira inatoka kwa soul-emotion. Ila kama nilivyosema hapo juu, chochote kitokacho kwa SOUL huwa kimeanzia kwa human spirit or demonic spirit or God's spirit.
Sasa baada ya 'definition' ndefu. Mtu akifa huenda wapi?
Mwili huzikwa kaburini ulikotoka
Nafsi ambayo ni wewe haswaaa hupotea mara baada ya human spirit kutengana na mwili. Nafsi ilitokea baada ya mwili kuungana na spirit/roho. Pia nafsi hupotea pale mwili unapotengana na human spirit. Pia Nafsi na mwili vitafufuliwa siku ya ufufuo/kiyama.
Human spirit never dies. Kwa mwanadamu aliyeshika njia ya Mungu wa Yesu Kristu hadi mwisho wa uhai wake, human spirit inarudi kwa Mungu na inaendelea kuishi huko. Sijui kama inakuwa idle ikingojea ufufuo wa mwili au kuna activity wanafanya. Hiyo experience sina.
Kwa mwanadamu aliyeenda kinyume na njia ya Yesu hadi mwisho wa maisha yake ya hapa, pia sina experience kuhusu human spirit yake huenda wapi - ila kwa mujibu wa maandiko inaenda mahali pa huzuni kubwa ikisubiri hukumu ya mwisho.
Kwa heri